Posts

Nafasi ya Kazi Stamigold

Image
STAMIGOLD COMPANY LIMITED EMPLOYMENT OPPORTUNITY ‘STAMIGOLD Company Limited -Biharamulo Mine is a subsidiary company of the State Mining Corporation (STAMICO) operating a gold mine. The Mine is located in the Biharamulo Forest Reserve South West of Mwanza in Kagera Region. In order to run the mine effectively and efficiently, the Company invites applications from qualified candidates to fill the existing vacancy as detailed below THE ROLE: Work Station: Biharamulo Mine Site Work Roster: 6/3 (42 days on, 21 days off) Contract Duration: Not exceeding two years, subject to renewal SENIOR SUPPLIES OFFICER (01) The Senior Supplies Officer-will be reporting to the Procurement Superintendent and should ensure effective supplying of goods and services in response to internal needs by providing support, ,guidance and professional advice within the requirements of the Procurement and Supplies Professionals and Technician Board (PSPTB) and Public Procurement Regulatory A

Mahakama Yagomea Pingamizi la Mbowe kwa Jeshi la Polisi

Image
KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali. Mbowe alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni Jeshi la Polisi  kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali ya usalama nchini si salama. Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo, aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Mbowe ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya oparesheni iliopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata katiba ya nchi. Hata hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya M

Mdosi mbaroni kwa ujambazi Moshi

Image
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Wilbroard Mtafungwa. Issa Mnally na Richard Bukos, UWAZI DAR ES SALAAM: Watu watatu akiwemo mmoja mwenye asili ya Kiasia ‘Mdosi,’ wametiwa mbaroni na polisi Moshi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za ujambazi, Uwazi limeezwa. Akizungumza na waandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Wilbroard Mtafungwa alisema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukamatwa kutokana na ushirikiano wa polisi na raia wema. Akielezea jinsi polisi walivyowanasa watuhumiwa hao, Kamanda Mtafungwa alisema kuwa walimkamata kwanza mmoja Fredil Guston maarufu kwa jina la Chedieli ambaye ni mkazi wa Majengo, Moshi. Aidha, alisema Chedieli aliwataja wenzake ambao ni Frank Nkya maarufu kwa jina la Chabufa na Frank Mbesanyo Domani ‘Ausho’ mkazi wa Pasua na walipopekuliwa walikutwa na vitu kadhaa vya wizi. “Sasa hawa wakamtaja bosi wao ambaye ni kiongozi wao mkuu wa

Majibu ya Hoja za Wabunge Yaliyotolewa Jana na Waziri wa Fedha

Image
JUNI 20, 2016 DODOMA UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kukushukuru wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha vizuri majadiliano kuhusu Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa 2015 na Mpango wa Maendeleo wa 2016/17 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2016/17, niliyowasilisha tarehe 8 Juni, 2016. Mheshimiwa Spika, Kipekee, ninampongeza sana Mhe. Naibu Spika kwa umahiri na weledi wa hali ya juu alioonesha katika kusimamia Kanuni za Bunge wakati wote wa kikao hiki cha Bunge la bajeti. Hakika viwango vyake ni vya kimataifa. Japokuwa Mhe. Joseph Kakunda, mwanafunzi wangu Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam alichomekea sehemu fulani akidai kwamba mimi ni bahiri, (nadhani alimaanisha bahiri wa kutoa maksi za upendeleo!), nataka niliambie Bunge lako tukufu kwamba kwa viwango ambavyo Mhe. Naibu Spika alivyoonesha humu ndani, hakika ningempa maksi za haki asilimia 100 kama walivyofanya maprofesa

Wabongo wafungukia simu feki kuzimwa

Image
Stori:  Gladness Mallya, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ kutangaza kuzima simu feki usiku wa Juni 16, mwaka huu, wananchi mbalimbali wa Jiji la Dar, wamefunguka ya moyoni: BARIKI GASTON (MWENGE) “Kuzimwa simu feki kumeniumiza sana na siyo mimi tu wapo wengi hasa wenye hali ya chini japokuwa zina madhara wangetuachia kwa muda mrefu kidogo ili tujipange kwanza.” HIDAYA SAID (MWANANYAMALA) “Serikali ilivyofanya siyo vizuri kwa sababu hali ya maisha ni ngumu, nafanya mama ntilie hapa sina uwezo wa kununua simu orijino, wangetuangalia sisi watu wa vipato vya chini wasingezima ila wangezuia zile zinazoingia nchini lakini hizi tunazomiliki tubaki nazo.” JOSEPH VENANCE (MWENGE) “Suala la simu feki kuzima limetuchanganya sana maana tulishazoea kununua kwa bei rahisi lakini sasa haya ni majanga kwa sababu mpaka upate hela ya kununua simu orijino ni kazi sana lakini inabidi tukubaliane tu hali halisi maana zina madh

Video ya aibu ya Wema yavuja!

Image
Wema Sepetu (kulia) wakati wa hafla hiyo. Stori: Andrew Carlos, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Video ya aibu inayomuonesha msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ akicheza kihasara mbele ya mwanaume imevuja, Risasi Jumamosi linayo kibindoni. ‘Klipu’ hiyo ambayo Wema anaonekana akikata mauno huku suruali aliyokuwa amevaa ikimvuka na kuacha wazi sehemu ya makalio yake, ilivujishwa hivi karibuni na mdau mmoja wa burudani ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini. Wema na Igwe wa Pah One wakiyarudi. “Hii video niliichukua siku ya ile eventi ya Christian Bella ya kutimiza miaka 10 pale Escape One. Wakati akicheza na msanii wa Kundi la Pah One aitwaye Igwe, Wema alionekana kama alikuwa amelewa, alikuwa akikata mauno lakini aibu zaidi ilikuwa pale ambapo ile suruali yake ilipomvuka na sehemu ya makalio yake kubaki wazi. “Sidhani kama alikuwa kavaa kufuli, baadhi ya watu waliokuwa wakimkodolea macho walishindwa kuamini kama ni Wema yule wanayemju

Shamsa Ford: Vimini vyangu havimuathiri mtoto

Image
Shamsa Ford Boniphace Ngumije, Risasi Jumamosi DIVA mwenye ‘title’ kubwa Bongo, Shamsa Ford amesema kuwa tangu awe mzazi anajitahidi kuishi maisha ya kistaarabu sana kiasi kwamba hahitaji kuwa na skendo ili kuitunza heshima yake kwa mwanaye wa kiume aitwaye Terry pale ambapo atakuwa kijana. Shamsa na mwanaye. Shamsa alisema hayo wakati akipiga stori mbili-tatu na gazeti hili, alipoulizwa kwa nini anapendelea kuvaa mavazi mafupi alisema kuwa hiyo ni ‘hobby’ yake tangu utotoni, kila mmoja kwenye familia yake anafahamu hilo na wala haihusiani kabisa na malezi ya mtoto. “Mimi nililelewa na mama yangu mkubwa ambaye ameolewa na Mzungu, tangu udogoni alikuwa ananivalisha nguo fupi pamoja na watoto wake. Kwenye familia yetu suala hilo si tatizo wala halihusiani na malezi ya mtoto, ninaimani hata Terry akikua ataliona kuwa ni jambo la kawaida kabisa,” alisema Shamsa.

ALIYEKUWA BEKI WA TP MAZEMBE ATUA SIMBA

Image
Kweli Simba wameamua, tayari beki Janvier Besala Bokungu raia wa DRC, ametua Dar es Salaam kimyakimya ili kumalizana na uongozi wa Msimbazi. Bokungu ni beki wa zamani wa TP Mazembe, kama unakumbuka vizuri ndiye walimchezesha katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ikakata rufaa kwenye Shirikisho la Soka Afrika (Caf), TP Mazembe wakaondolewa mashindanoni na Simba kupata nafasi ya kucheza na Wydad Casablanca ya Morocco.  “Tayari wametua hapa nchini na wataanza mazungumzo na taratibu nyingine, maana Bokungu alikuwa Esperance ya Tunisia. Mimi ninaamini atasajiliwa Simba maana kiwango chake kipo juu tu,” kilieleza chanzo. Caf, ilitangaza uamuzi wa kuiondoa TP Mazembe Mei 14, 2011 na mechi ikachezwa kwenye uwanja huru wa Petrojet jijini Cairo, Misri, Simba ikatandikwa mabao 3-0, hiyo ilikuwa Mesi 28, 2011.  Bokungu yuko jijini Dar es Salaam pamoja  na kiungo mwingine raia wa DR Congo pia wakisubiri ‘kuonwa’ na makocha au watu maalum kabla ya kusaini mkataba

Mwalimu Afungwa Jela Miaka 90 kwa kuwanajisi wanafunzi

Image
  Mwalimu John Gichia Mugi. Nairobi, Kenya Mwalimu mmoja wa shule ya msingi aliyetambulika kwa jina la John Gichia Mugi mwenye umri wa miaka 23 nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwa kuwanajisi wanafunzi wake wenye umri kati ya miaka 13 hadi 16. Hii ni moja kati ya vifungo vya muda mrefu zaidi kuwahi kutolewa kwa watu wanaowaingilia watoto kijinsia nchini Kenya. Mwalimu John Gichia alishtakiwa kwa kuwabaka wavulana 9 wa shule ya msingi ya Muthiria iliyopo Muran’ga takriban kilomita 120 Magharibi mwa Nairobi nchini humo mnamo Januari na Mei mwaka 2015. Mwalimu huyo atatumikia kifungo cha miaka 10 kwa kila kosa alilotenda yaani kubaka watoto 9, hivyo kufanya jumla ya miaka atakayotumikia jela kufikia 90. Jaji alisema mwalimu walikuwa amesaliti dhamana na imani aliyopewa na wazazi wa wanafunzi hao wachanga ambao alipaswa kuwatunza, inasemekana alikuwa akiwafanyia vitendo hivyo viovu watoto hao baada ya muda wa masomo wa usiku (preps). Wavulana

Mastaa hawa wameachiwa chata, hakijaelewaka!

Image
    Rose Ndauka Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi MPANGO au matarajio ya kila mwanadamu ni kuishi katika uchumba, kuolewa kisha kupata watoto! Wapo ambao wamefanikiwa hilo, wapo ambao wamepata kwanza mimba baadaye wakaolewa lakini wapo pia waliopata mimba kabla ya ndoa kisha wakatofautiana na waliowapa, kila mmoja anaishi kivyake. Katika ulimwengu wa mastaa wa kike Bongo, leo nakuletea baadhi ya mastaa ambao wamepata watoto lakini kwa namna moja au nyingine safari yao na waliowapa ujauzito haikufika mbali, ikavunjika. Wapo ambao walipata kabla na wengine baada ya ndoa. Wengi wao huwanadi watoto hao mitandaoni kwa maneno mazuri wakionesha kwamba ndiyo faraja yao baada ya kuachana na wapenzi au waume wao; ROSE NDAUKA Aliingia katika uchumba na Malick Bandawe. Wakafanikiwa kupata mtoto mmoja, uchumba ukayeyuka wakati wawili hao wakiwa katika mchakato wa kuelekea kwenye ndoa. SNURA MUSHI Amefanikiwa kupata watoto wawili; wa kike na wa kiume kwa baba tofauti.

KIKWETE ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA

Image
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho  Kikwete akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho   Kikwete akizungumza na  Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba

MERCY KITOMARI, MJASIRIAMALI KIJANA ANAYETAKA KUMUONA ‘ROLE MODEL’ WAKE RAIS MAGUFULI

Image
Mjasiriamali kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari wakati akizungumza na Meneja Uendeshaji wa mtandao wa Habari wa  Modewjiblog , Zainul Mzige (hayupo pichani). MJASIRIAMALI kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari amesema anatamani kukutana na Rais John Pombe Magufuli kumwelezea haja ya kukutana na wanawake wajasiriamali vijana wamweleze matatizo yao. Amesema Rais baada ya kukutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara , inafaa akutane na wajasiriamali wanawake vijana ambao wanapita katika magumu mbalimbali . Alisema katika mahojiano hivi karibuni ambayo sehemu yake itachapishwa katika mtandao wa Modewjiblog muda wowote kwamba, rais Magufuli akiwa kama ‘Role Model wake’ katika kujituma, anaweza kuwasikiliza wanawake hao vijana na kusaidia kuwasukuma juu zaidi katika kampeni ya kuiweka Tanzania kuwa nchi ya viwanda. “Nimekuwa nikikutana na wanawake wenzangu ambao wamekata tamaa na wamekuwa wakiniuliza ninawezaje kuendelea,