Video ya aibu ya Wema yavuja!
Stori: Andrew Carlos, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Video ya aibu
inayomuonesha msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’
akicheza kihasara mbele ya mwanaume imevuja, Risasi Jumamosi linayo
kibindoni.
‘Klipu’ hiyo ambayo Wema anaonekana
akikata mauno huku suruali aliyokuwa amevaa ikimvuka na kuacha wazi
sehemu ya makalio yake, ilivujishwa hivi karibuni na mdau mmoja wa
burudani ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
“Hii video niliichukua siku ya ile
eventi ya Christian Bella ya kutimiza miaka 10 pale Escape One. Wakati
akicheza na msanii wa Kundi la Pah One aitwaye Igwe, Wema alionekana
kama alikuwa amelewa, alikuwa akikata mauno lakini aibu zaidi ilikuwa
pale ambapo ile suruali yake ilipomvuka na sehemu ya makalio yake kubaki
wazi.
“Sidhani kama alikuwa kavaa kufuli,
baadhi ya watu waliokuwa wakimkodolea macho walishindwa kuamini kama ni
Wema yule wanayemjua,” alisema mnyetishaji huyo.
Baada ya mwandishi wetu kupata nafasi ya
kuiangalia mwanzo mpaka mwisho, alijiridhisha kuwa aliyekuwa akionekana
kwenye video hiyo ni Wema na kweli alichokuwa akifanya ni aibu tupu.
Aibu yake ni pale ambapo suruali
inamvuka na kuacha sehemu zake za siri wazi lakini pia staili ya
kumkatikia msanii aliyekuwa akicheza naye kwani jamaa alikuwa
‘akikamatia chini’ huku naye akionekana kutokwa na udenda.
Paparazi wetu alijaribu kumtafuta Wema ili kuizungumzia ‘klipu’ hiyo lakini simu yake kila ilipopigwa ilikuwa haipokelewi.
Comments
Post a Comment