MERCY KITOMARI, MJASIRIAMALI KIJANA ANAYETAKA KUMUONA ‘ROLE MODEL’ WAKE RAIS MAGUFULI
Mjasiriamali kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari wakati akizungumza na Meneja Uendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige (hayupo pichani).
MJASIRIAMALI
kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari amesema anatamani
kukutana na Rais John Pombe Magufuli kumwelezea haja ya kukutana na
wanawake wajasiriamali vijana wamweleze matatizo yao.
Amesema
Rais baada ya kukutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara ,
inafaa akutane na wajasiriamali wanawake vijana ambao wanapita katika
magumu mbalimbali .
Alisema
katika mahojiano hivi karibuni ambayo sehemu yake itachapishwa katika
mtandao wa Modewjiblog muda wowote kwamba, rais Magufuli akiwa kama
‘Role Model wake’ katika kujituma, anaweza kuwasikiliza wanawake hao
vijana na kusaidia kuwasukuma juu zaidi katika kampeni ya kuiweka
Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
“Nimekuwa
nikikutana na wanawake wenzangu ambao wamekata tamaa na wamekuwa
wakiniuliza ninawezaje kuendelea, nikawambia wasi-give up (wasikate
tama) na kwamba serikali hii ni ya viwanda na kuchapa kazi “ alisema na
kufafanua kwamba wanachohitaji wanawake hao ni mazingira mazuri ya
kufanya ujasiriamali.
Mercy
ambaye anatengeneza ‘ice cream’ zinazotumia matunda yote ya kitanzania
kama vile fenesi, nanasi, bungo, ndizi, embe ana ndoto ya kumiliki
kiwanda kikubwa kinachoweza kutengeneza na kufikisha ashkrimu kwa
Tanzania na Afrika Mashariki ifikapo mwaka 2020.
Akiwa
ameanza kazi hiyo mwaka 2010 kutoka ‘jiko’ la nyumbani Mercy
amefanikiwa kutambua wigo wake wa biashara ambayo amesema ina changamoto
nyingi hasa mifumo ya vibali na ulipaji kodi na ushuru.
Muonekano
wa nje wa duka la Ice Cream la Nelwa’s Gelato lililopo ndani ya Petrol
Station ya SOPCO barabara ya Morogoro-Magomeni Mwembechai karibu na kwa
Sheikh Yahya.
Alisema
uwapo wa kodi nyingi zenye viwango sawa kati ya anayeanza na
aliyekuwepo; anayeingiza kidogo na kikubwa kunaleta athari kubwa kwa
wajasiriamali wanaotaka kuchomoza.
“To
be honest (nikiwa mkweli) zinavunja moyo… nyingi zinakwamisha kwani
sisi waelewe tu kwamba tunatengeneza ajira na tunatengeneza soko kama
mimi nanunua matunda natengeneza soko la mkulima.,.. natengeneza
ashkrimu (Ice Cream) natengeneza ajira.. ipo haja ya kuangalia mambo
mengi na hasa hili la kodi na ushuru” alisema.
Alisema ana mambo mengi ya kumwambia Rais Magufuli kama mjasiriamali mwanamke kijana.
“Atupe
nafasi tukutane naye wanawake wajasiriamali vijana kisha tutamweleza
mengi yakiwemo ya kodi na mifumo yake, mimi ningemweleza haja ya vyombo
vyote vya huduma kutumia mtandao, kutoa huduma ,ningemweleza haja ya
halmashauri na taasisi kutoa mafunzo mbalimbali ili kuinua wajasiriamali
hawa na kuwasapoti si tu kuchukua kodi na ushuru” anasema Mercy.
Anasema wajasiriamali wengi wadogo hawaendelei kwa kukosa sapoti ya mafunzo na namna ya kufanya biashara zao zikue.
“Wasiwe
wanachukua kodi na ushuru tu, halmashauri hizi lazima zianze kufikiria
kukuza wajasiriamali kwa kuwapa elimu inayostahili katika biashara zao”
anasisisitiza Mercy ambaye amesema angelipenda kumuona Role Model wake
(Rais Magufuli) kumweleza mengi yanayohusu wanawake vijana na viwanda
vidogo kuelekea viwanda vikubwa na hamu ya wajasiriamali wanawake vijana
kuchangia pato la taifa na kulipa heshima.
Anasema
anapokutana na wajasiriamali wa Uganda, Rwanda anaona jinsi serikali
zao zinavyowasaidia kunyanyuka na anaona serikali ya awamu ya tano
inaweza kuwasikia na wao wakanyanyuka.
Comments
Post a Comment