Mwalimu Afungwa Jela Miaka 90 kwa kuwanajisi wanafunzi
Mwalimu John Gichia Mugi.
Nairobi, Kenya
Mwalimu
mmoja wa shule ya msingi aliyetambulika kwa jina la John Gichia Mugi
mwenye umri wa miaka 23 nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 90
jela kwa kuwanajisi wanafunzi wake wenye umri kati ya miaka 13 hadi 16.
Hii ni moja kati ya vifungo vya muda mrefu zaidi kuwahi kutolewa kwa watu wanaowaingilia watoto kijinsia nchini Kenya.
Mwalimu John Gichia alishtakiwa kwa
kuwabaka wavulana 9 wa shule ya msingi ya Muthiria iliyopo Muran’ga
takriban kilomita 120 Magharibi mwa Nairobi nchini humo mnamo Januari na
Mei mwaka 2015.
Mwalimu huyo atatumikia kifungo cha
miaka 10 kwa kila kosa alilotenda yaani kubaka watoto 9, hivyo kufanya
jumla ya miaka atakayotumikia jela kufikia 90.
Jaji alisema mwalimu walikuwa amesaliti
dhamana na imani aliyopewa na wazazi wa wanafunzi hao wachanga ambao
alipaswa kuwatunza, inasemekana alikuwa akiwafanyia vitendo hivyo viovu
watoto hao baada ya muda wa masomo wa usiku (preps).
Wavulana hao walikuwa na ushahidi kuwa
Mugi aliwaguswa sehemu zao za siri na wakati mwingi anawabusu. Wakati
huo alikuwa akihudumu kama mwalimu anayesimamia maswala ya bweni katika
shule hiyo.
Kifungo hicho cha miaka 90 ni ishara tu
kuwa sera za serikali ya Kenya imeanza kuchukua hatua kali dhidi ya wale
wanaowadhulumu watoto nchini kenya. Ikiwa atajaaliwa na maiasha marefu,
Mugi ataachiliwa akiwa na umri wa miaka 113.
Comments
Post a Comment