Mastaa hawa wameachiwa chata, hakijaelewaka!
Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi
MPANGO au matarajio ya kila
mwanadamu ni kuishi katika uchumba, kuolewa kisha kupata watoto! Wapo
ambao wamefanikiwa hilo, wapo ambao wamepata kwanza mimba baadaye
wakaolewa lakini wapo pia waliopata mimba kabla ya ndoa kisha
wakatofautiana na waliowapa, kila mmoja anaishi kivyake.
Katika ulimwengu wa mastaa wa kike
Bongo, leo nakuletea baadhi ya mastaa ambao wamepata watoto lakini kwa
namna moja au nyingine safari yao na waliowapa ujauzito haikufika mbali,
ikavunjika. Wapo ambao walipata kabla na wengine baada ya ndoa.
Wengi wao huwanadi watoto hao mitandaoni
kwa maneno mazuri wakionesha kwamba ndiyo faraja yao baada ya kuachana
na wapenzi au waume wao;
ROSE NDAUKA
Aliingia katika uchumba na Malick
Bandawe. Wakafanikiwa kupata mtoto mmoja, uchumba ukayeyuka wakati
wawili hao wakiwa katika mchakato wa kuelekea kwenye ndoa.
SNURA MUSHI
Amefanikiwa kupata watoto wawili; wa
kike na wa kiume kwa baba tofauti. Wote wameingia mitini. Akapata
mchumba mpya, naye wakamwagana kabla ya kufanikiwa kuolewa wala kuzaa.
ZUWENA MOHAMMED ‘SHILOLE’
Ana watoto wawili wa kike ambao alizaa
na wanaume wawili tofauti kwa nyakati tofauti. Kwa sasa wamemuachia
chata ya watoto hao wa kike ambao anawadi mitandaoni.
KAJALA MASANJA
Aliingia kwenye ndoa na Faraji Agustino
akiwa tayari ameachiwa chata moja ya kike na Prodyuza, Paul Matthysse
‘P Funk’. Bahati mbaya mumewe hakufanikiwa kuzaa naye, akafungwa kwa
msala wa kutakatisha fedha haramu. Hadi sasa ana furaha kuwa na binti
yake huyo.
HAMISA MOBETO
Alikuwa kwenye uchumba na bosi wa redio
moja maarufu, akafanikiwa kupata mtoto mmoja na uchumba ukaishia hapo.
Kila mtu yupo kivyake kwa sasa Mobeto anajifariji na chata yake ya kike
aliyoachiwa.
JENIFFER KYAKA ‘ODAMA’
Inasemekana amezaa na kigogo mmoja
ambaye ana familia yake. Inadaiwa kuwa kigogo huyo ameelekeza nguvu zake
kwa mkewe hivyo Odama kubaki na chata yake ambayo anainadi kwenye
mitandao ya kijamii mara kwa mara.
IRENE UWOYA
Aliingia kwenye ndoa na mshambuliaji wa
zamani wa Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’. Akafanikiwa
kupata mtoto mmoja wa kiume (Krish) kisha ndoa ikasambaratika na sasa
anafarijika kwa kuachiwa kopi yake.
WENGINE
Masta wengine ambao kwa namna moja au
nyingine wamezalishwa na kuachiwa watoto ni pamoja na Shamsa Ford, Faiza
Ally aliyezaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Siwema
Edson (aliyekuwa demu wa Nay wa Mitego) na Riyama Ally ambaye ameachiwa
chata ya kike.
Comments
Post a Comment