Posts

JK AOMBELEZA MSIBA WA RAIS WA SAHARA MAGAHARIBI

Image
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mama Salma Kikwete. Mke wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikete. Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa nchi ya Sahara Magharibi Brahim Salem Buseif mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI PAPOA NEW GUINEA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea Baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Picha yenye Nembo inayotumika Nchini Papua New Guinea kutoka kwa Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea baada ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific u

Rich Mavoko Asajiliwa Rasmi Lebo ya WCB

Image
Msanii wa Bongo fleva, Rich Mavoko (kushoto)  akisaini Mkataba wa kujiunga na lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyopo chini ya staa wa tasnia hiyo, Diamond Platnumz (kulia). Diamond (kushoto) akipongezana na Rich Mavoko mara baada ya kusaini mkataba huo. Habari ikufikie popote ulipo wewe mpenda burudani na mdau wa muziki wa bongo fleva kuwa, leo June 2, 2016 lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na staa wa tasnia hiyo Diamond Platnumz inaingia kwenye headlines za Bongo Fleva baada ya kumtambulisha rasmi  msanii  wao mpya  Rich Mavoko ambaye anakuwa ni msanii wa nne atakayesimamiwa kazi zake katika lebo ya WCB. Kwa mujibu wa CEO wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz amesema… ’ Kwasasa Label yangu inakuwa na jumla ya wasanii nne ukiachana na Rich Mavoko kuna Dada yangu Queen Darling ambaye sijawahi kumtambulisha lakini anakuwa ni msichana wa kwanza katika label yangu kwahiyo tutakuwa na jumla ya wasanii nne Raymond, Harmonize, Rich Mavo

AHADI YA RAIS MAGUFULI KWA WAFANYABIASHARA WAKUBWA YAANZA KUTIMIA

Image
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda  (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda 2015 (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana. Na Mwandishi wetu Nia serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuanza kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa nchini ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kusaidia kuinua uchumi wa nchi lakini pia kutoa ajira kwa watanzania katika viwanda vinavyoilikiwa na matajiri hao. Hilo limenza kuonekana siku moja baada ya Rais Magufuli kuweka wazi nia yake hiyo ambapo

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MSITU WA MAPANGOPORI YA AMBONI

Image
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyotoa ulinzi katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga.   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo (kulia)

Mume, Mke Wachinjwa Kinyama.

Image
Majeneza yenye miili ya marehemu hao. Na Gregory Nyankaira, RISASI MCHANGANYIKO MARA: Hali mbaya! Wanandoa Said Somba (48) na Kadogo Ehijo (47), wakazi wa Kitongoji cha Rugala, Kijiji cha Mazami, Kata ya Bukabwa wilayani Butiama mkoani hapa wameuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana, Risasi Jumatano lina kila kitu. Marehemu Somba (kushoto) na marehemu Kadogo kulia. Diwani wa Kata ya Bukabwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rugala, Jonas Maswe aliliambia gazeti hili kuwa, tukio hilo lilijiri usiku wa Mei 25, mwaka huu ambapo watu hao wakiwa na mapanga walivamia nyumbani kwa Somba akiwa amelala na mkewe na kuwachinja. Baadhi ya watoto wa marehemu wakilia juu ya jeneza la baba yao Alisema wakati wanachinjwa, wanandoa hao hawakupiga kelele na baada ya ukatili huo  wauaji hao waliifunika miili yao kitandani kisha wakatokomea kusikojulikana.  Alisema mauaji hayo yalifanyika kimyakimya kwani hata  watoto wa marehemu waliokuwa wamelala nyumba ya

Je, Wajua! Maganda ya chungwa tiba kwa ugonjwa wa Mba kichwani

Image
  Watu wengi wanasumbuliwa na ugonjwa wa mba kichwani, awali nilishawahi kuandika kuhusu tiba nyingine, lakini ninaongeza na hii ili kuwasaidia. Mara nyingi mba huwa wanatokea nyakati za baridi kwani kichwa huwa ni kikavu sana kama unasumbuliwa na hilo tatizo unatakiwa kuwa makini na mafuta unayotumia na kuhakikisha unatumia mafuta kila unapoosha nywele zako. Jinsi ya kufanya Chukua chungwa limenye upate maganda yake baada ya hapo chukua limao likamue kisha uweke kwenye Brenda usage upate mchanganyiko mmoja. Matumizi Osha nywele zako kwanza zitakate na baada ya hapo zikaushe kisha paka mchanganyiko wako kwenye ngozi acha kwa muda wa dakika 20-25 kisha osha kwa kutumia shampuu unayotumia ambayo unaamini ni nzuri. Tumia tiba hii kwa wiki mara tatu utaona jinsi utakavyokomesha moja kwa moja tatizo la mba kichwani.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMWAKILISHA RAIS DKT JOHN MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA, NCHINI PAPUA NEW GUINEA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Mhe. Peter O Neil Alipowasili Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe walipokutana Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama

Hatimaye Siwema wa Nay Atoka Gerezani!

Image
Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Siwema Edson. Na Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO HABARI njema! Mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson aliyehukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kutishia kwa njia ya mtandao, hatimaye ametoka jela. Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko , Nay wa Mitego alisema katika harakati za kushughulikia ili mzazi mwenzake huyo atoke alifanikiwa kupata mawakili wawili ambao mpaka Jumamosi iliyopita walifanikisha zoezi la Siwema kutoka na sasa atatumikia kifungo cha nje. Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mzazi mwenzake,  Siwema Edson Nay wa Mitego alisema alilazimika kupambana kwa nguvu zote si kwa sababu anataka kuwa naye isipokuwa kama mzazi hakujisikia vizuri kuona mama wa mwanaye yuko jela wakati yeye anao uwezo wa kufanya kitu kwa ajili ya kumsaidia. “Kulikuwa kuna njia mbili za kufanya, kukata rufaa au kubadilishiwa kifungo, mawakili wangu waliniambia niwaachie wao watamaliz

Hii Ndiyo Sababu ya Wanafunzi 7802 UDOM Kurudishwa Nyumbani

Image
JUMUIYA ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) imesema kilichotokea si walimu kugoma kufundisha programu ya Stashahada Maalumu ya Elimu, Sayansi, Hisabati na Tehama, bali tatizo ni kutoelewana na Menejimenti ya chuo kutokana na mazingira mabovu ya uendeshaji wa programu hiyo chuoni hapo. Aidha, imelaani kitendo cha wanafunzi 7,802 wa Programu Maalumu ya Ualimu wa Msingi na Sekondari, waliorudishwa nyumbani bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa kwa kuzingatia umri wao na mazingira waliyokuwa wanaishi, hali inayofanya wazagae mitaani huku wakiwa hawana pa kwenda. Hayo yako kwenye tamko lililotolewa jana na Katibu wa jumuiya hiyo, Lameck Thomas, ambalo lilieleza kuwa lawama zimekuwa zikitupwa kwa walimu kutokana na taarifa hizo kutolewa na upande mmoja, ambao ni Menejimenti ya chuo kwenda serikalini bila kuwepo na taarifa yoyote kutoka kwa walimu kupitia jumuiya yao. Thomas alisema si kweli kama walimu waligoma kufundisha lakini tatizo kubwa ni kutoel

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA HAFLA YA UTOAJI WA TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA KWA MWAKA 2015.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na washindi mbalimbali waliopata tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa viwanda kwa mwaka 2015.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda    PMAYA  The President’s Manufacure of the Year    pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rai

SERIKALI KUANZISHA BENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI.

Image
Na Lilian Lundo-MAELEZO. Serikali ya awamu ta Tano imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya sasa. Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli amesema kuwa jambo hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi yetu ina rasilimali zinazohitajika katika kujenga uchumi wa viwanda.“Nafahamu kwamba tunakila aina ya rasilimali inayowezesha uwepo wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa kutosha pamoja na malighafi zake na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuifanya sekta ya viwanda kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais Magufuli. Aidha Dkt. Magufuli aliwatoa wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la uhakika kwa bidhaa zitakazozalishwa kwani Tanzania im

BOSI WA ZAMANI WA TRA KITILYA NA WENZAKE WAZIDI KUSOTA MAHAKAMA YA RUFAA

Image
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya akienda kupanda gari litakalompeleka rumande. Sioi Sumari akiwa na askari wa magereza. Shose Sinare naye akiongozana na askari magereza kuelekea kwenye gari lililompeleka rumande. Baadhi ya mawakili na wananchi wakitoka mahakamani. LEO katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, jijini Dar es Salaam Kamishna Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake  waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya Stanbic Tanzania, Sioi Sumari na Shose Sinare walifikishwa mahakamani hapo kusikiliza rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri. Jamhuri imekata rufaa kupinga kufutwa shitaka namba 8 linalowakabili wote kwa pamoja la utakatishaji fedha linalowakabili. Hata hivyo, mahakama hiyo itapanga tarehe ya kusikilizwa shauri hilo siku itakayotangazwa. Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la kula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na sheria na walifikishwa mahakamani kwa mara

Shilole, Vanessa Wamaliza Bifu Lao

Image
      Shilole (kulia)  akipashana jukwaani na Vanessa kabla ya shoo hiyo kuanza. Vanessa na Shilole wakijaribu kuelezea juu ya bifu lao. Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM, Hamisi Mandi ‘B12’, akiwakaribisha Shilole na Vanessa Mdee tayari kwa kufanya shoo hiyo. Shilole akifanya makamuzi. Vanessa akikamua jukwaani. Baadhi ya mashabiki wakifuatilia shoo hiyo. WAREMBO wanaofanya vyema kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Vanessa Mdee, usiku wa kuamkia leo wameweza kuvunja bifu lao ambalo limekuwa likivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukamua kwenye steji moja ndani ya ukumbi wa Bilicanas. Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

BREAKING NEWZ:Vurugu Tena Bungeni, Ni Kuhusu Wanafunzi 7000 wa UDOM Waliotimuliwa.

Image
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali itikadi ya vyama vyao, leo wametoka nje ya ukumbi wa bunge hilo baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kukataa kujadiliwa kwa kauli ya serikali kuhusu wanafunzi 7000 wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) waliosimamishwa. Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kutekeleza agizo la Maziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako hivi karibuni kiliwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke chuoni hapo mara moja. Wabunge waliwasilisha hoja kwa Naibu Spika, Tulia Ackson ili kulishinikiza bunge kuijadili kauli ya serikali kuhusu wanafunzi hao waliotimuliwa ambapo Naibu Spika alikataa kusikilizwa hoja hayo ndipo vurugu zikaanza na kumlazimu Naibu Spika kufunga Kikao cha Bunge kilichokuwa kikiendelea na kuwaamuru wabunge wote watoke nje. Juzi, lilitolewa tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kuondoka chuoni hapo. Tangazo hilo lilieleza kuwa k

Lungi alinanga penzi la Wolper, Harmonize

Image
Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ STORI: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA MSANII wa filamu wa kitambo, Lungi Maulanga amelinanga penzi na Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ akisema kuwa, anachoona ni kama Wolper anatembea na mdogo wake. Lungi Maulanga Akiuzungumzia uhusiano wa mastaa hao, Lungi alisema alijisikia vibaya sana kuona shosti wake Wolper kafa, kaoza kwa Harmonize kutokana na tofauti kubwa iliyopo kati yao. “Unajua Wolper ni kama mdogo wangu na shosti wangu hivyo siwezi kumuacha apotee, mimi nitamuita tutaongea kwa kina, kama atashikilia msimamo wake nitamuacha kwa sababu si unajua mtu akishapenda, lakini kiukweli hawajaendana,” alisema Lungi.