SERIKALI KUANZISHA BENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI.
Serikali
ya awamu ta Tano imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia
pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya
sasa.
Hayo
yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa
Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Rais
Magufuli amesema kuwa jambo hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi
yetu ina rasilimali zinazohitajika katika kujenga uchumi wa
viwanda.“Nafahamu kwamba tunakila aina ya rasilimali inayowezesha uwepo
wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa kutosha pamoja na malighafi zake
na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuifanya sekta ya
viwanda kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020
kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais Magufuli.
Aidha
Dkt. Magufuli aliwatoa wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la
uhakika kwa bidhaa zitakazozalishwa kwani Tanzania imezungukwa na nchi
zenye uhitaji wa bidhaa mbalimbali na pia ni Mwanachama wa jumuiya
mbalimbali ndani na nje ya Afrika.
Naye
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage aliwataka
wamiliki wa Viwanda Nchini kuunganisha nguvu katika uanzishaji na
uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini
hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa
watanzania.
Comments
Post a Comment