Je, Wajua! Maganda ya chungwa tiba kwa ugonjwa wa Mba kichwani

ORANGE 
Watu wengi wanasumbuliwa na ugonjwa wa mba kichwani, awali nilishawahi kuandika kuhusu tiba nyingine, lakini ninaongeza na hii ili kuwasaidia.
Mara nyingi mba huwa wanatokea nyakati za baridi kwani kichwa huwa ni kikavu sana kama unasumbuliwa na hilo tatizo unatakiwa kuwa makini na mafuta unayotumia na kuhakikisha unatumia mafuta kila unapoosha nywele zako.
Jinsi ya kufanya
Chukua chungwa limenye upate maganda yake baada ya hapo chukua limao likamue kisha uweke kwenye Brenda usage upate mchanganyiko mmoja.
Matumizi
Osha nywele zako kwanza zitakate na baada ya hapo zikaushe kisha paka mchanganyiko wako kwenye ngozi acha kwa muda wa dakika 20-25 kisha osha kwa kutumia shampuu unayotumia ambayo unaamini ni nzuri.
Tumia tiba hii kwa wiki mara tatu utaona jinsi utakavyokomesha moja kwa moja tatizo la mba kichwani.

Comments

Popular posts from this blog