AHADI YA RAIS MAGUFULI KWA WAFANYABIASHARA WAKUBWA YAANZA KUTIMIA
Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza
jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Tanzania (TPSF), Dk.
Reginald Mengi wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji
Bora wa Viwanda (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda
Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya utoaji Tuzo
za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda 2015 (PMAYA) iliyoandaliwa na
Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.
Na Mwandishi wetu
Nia
serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuanza kushirikiana na
wafanyabiashara wakubwa nchini ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja na
kusaidia kuinua uchumi wa nchi lakini pia kutoa ajira kwa watanzania
katika viwanda vinavyoilikiwa na matajiri hao.
Hilo
limenza kuonekana siku moja baada ya Rais Magufuli kuweka wazi nia yake
hiyo ambapo Mo Blog ilifanikiwa kupata picha ambayo ilimwonesha Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akizungumza mambo
mbalimbali na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Taznzania (TPSF),
Dk. Reginald Mengi mara baada ya kumalizika kwa halfa ya utoaji wa Tuzo
za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) zilizoandaliwa na
Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).
Kutokana
na muonekano wa viongozi hao wawili wa serikali na sekta binafsi ni
wazi kuwa serikali ya Rais Magufuli imejipanga kushirikiana na
wafanyabiashara ili kufanya kazi kwa pamoja na kuiwezesha Tanzania kuwa
nchi ya viwanda jambo ambalo litachangia ukuaji wa kasi wa uchumi na
upatikanaji wa ajira kwa Watanzania.
Comments
Post a Comment