Posts

Mume, Mke Wachinjwa Kinyama.

Image
Majeneza yenye miili ya marehemu hao. Na Gregory Nyankaira, RISASI MCHANGANYIKO MARA: Hali mbaya! Wanandoa Said Somba (48) na Kadogo Ehijo (47), wakazi wa Kitongoji cha Rugala, Kijiji cha Mazami, Kata ya Bukabwa wilayani Butiama mkoani hapa wameuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana, Risasi Jumatano lina kila kitu. Marehemu Somba (kushoto) na marehemu Kadogo kulia. Diwani wa Kata ya Bukabwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rugala, Jonas Maswe aliliambia gazeti hili kuwa, tukio hilo lilijiri usiku wa Mei 25, mwaka huu ambapo watu hao wakiwa na mapanga walivamia nyumbani kwa Somba akiwa amelala na mkewe na kuwachinja. Baadhi ya watoto wa marehemu wakilia juu ya jeneza la baba yao Alisema wakati wanachinjwa, wanandoa hao hawakupiga kelele na baada ya ukatili huo  wauaji hao waliifunika miili yao kitandani kisha wakatokomea kusikojulikana.  Alisema mauaji hayo yalifanyika kimyakimya kwani hata  watoto wa marehemu waliokuwa wamelala nyumba ya

Je, Wajua! Maganda ya chungwa tiba kwa ugonjwa wa Mba kichwani

Image
  Watu wengi wanasumbuliwa na ugonjwa wa mba kichwani, awali nilishawahi kuandika kuhusu tiba nyingine, lakini ninaongeza na hii ili kuwasaidia. Mara nyingi mba huwa wanatokea nyakati za baridi kwani kichwa huwa ni kikavu sana kama unasumbuliwa na hilo tatizo unatakiwa kuwa makini na mafuta unayotumia na kuhakikisha unatumia mafuta kila unapoosha nywele zako. Jinsi ya kufanya Chukua chungwa limenye upate maganda yake baada ya hapo chukua limao likamue kisha uweke kwenye Brenda usage upate mchanganyiko mmoja. Matumizi Osha nywele zako kwanza zitakate na baada ya hapo zikaushe kisha paka mchanganyiko wako kwenye ngozi acha kwa muda wa dakika 20-25 kisha osha kwa kutumia shampuu unayotumia ambayo unaamini ni nzuri. Tumia tiba hii kwa wiki mara tatu utaona jinsi utakavyokomesha moja kwa moja tatizo la mba kichwani.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMWAKILISHA RAIS DKT JOHN MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA, NCHINI PAPUA NEW GUINEA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Mhe. Peter O Neil Alipowasili Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe walipokutana Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama

Hatimaye Siwema wa Nay Atoka Gerezani!

Image
Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Siwema Edson. Na Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO HABARI njema! Mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson aliyehukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kutishia kwa njia ya mtandao, hatimaye ametoka jela. Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko , Nay wa Mitego alisema katika harakati za kushughulikia ili mzazi mwenzake huyo atoke alifanikiwa kupata mawakili wawili ambao mpaka Jumamosi iliyopita walifanikisha zoezi la Siwema kutoka na sasa atatumikia kifungo cha nje. Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mzazi mwenzake,  Siwema Edson Nay wa Mitego alisema alilazimika kupambana kwa nguvu zote si kwa sababu anataka kuwa naye isipokuwa kama mzazi hakujisikia vizuri kuona mama wa mwanaye yuko jela wakati yeye anao uwezo wa kufanya kitu kwa ajili ya kumsaidia. “Kulikuwa kuna njia mbili za kufanya, kukata rufaa au kubadilishiwa kifungo, mawakili wangu waliniambia niwaachie wao watamaliz

Hii Ndiyo Sababu ya Wanafunzi 7802 UDOM Kurudishwa Nyumbani

Image
JUMUIYA ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) imesema kilichotokea si walimu kugoma kufundisha programu ya Stashahada Maalumu ya Elimu, Sayansi, Hisabati na Tehama, bali tatizo ni kutoelewana na Menejimenti ya chuo kutokana na mazingira mabovu ya uendeshaji wa programu hiyo chuoni hapo. Aidha, imelaani kitendo cha wanafunzi 7,802 wa Programu Maalumu ya Ualimu wa Msingi na Sekondari, waliorudishwa nyumbani bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa kwa kuzingatia umri wao na mazingira waliyokuwa wanaishi, hali inayofanya wazagae mitaani huku wakiwa hawana pa kwenda. Hayo yako kwenye tamko lililotolewa jana na Katibu wa jumuiya hiyo, Lameck Thomas, ambalo lilieleza kuwa lawama zimekuwa zikitupwa kwa walimu kutokana na taarifa hizo kutolewa na upande mmoja, ambao ni Menejimenti ya chuo kwenda serikalini bila kuwepo na taarifa yoyote kutoka kwa walimu kupitia jumuiya yao. Thomas alisema si kweli kama walimu waligoma kufundisha lakini tatizo kubwa ni kutoel

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA HAFLA YA UTOAJI WA TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA KWA MWAKA 2015.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na washindi mbalimbali waliopata tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa viwanda kwa mwaka 2015.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda    PMAYA  The President’s Manufacure of the Year    pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rai

SERIKALI KUANZISHA BENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI.

Image
Na Lilian Lundo-MAELEZO. Serikali ya awamu ta Tano imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya sasa. Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli amesema kuwa jambo hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi yetu ina rasilimali zinazohitajika katika kujenga uchumi wa viwanda.“Nafahamu kwamba tunakila aina ya rasilimali inayowezesha uwepo wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa kutosha pamoja na malighafi zake na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuifanya sekta ya viwanda kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais Magufuli. Aidha Dkt. Magufuli aliwatoa wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la uhakika kwa bidhaa zitakazozalishwa kwani Tanzania im

BOSI WA ZAMANI WA TRA KITILYA NA WENZAKE WAZIDI KUSOTA MAHAKAMA YA RUFAA

Image
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya akienda kupanda gari litakalompeleka rumande. Sioi Sumari akiwa na askari wa magereza. Shose Sinare naye akiongozana na askari magereza kuelekea kwenye gari lililompeleka rumande. Baadhi ya mawakili na wananchi wakitoka mahakamani. LEO katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, jijini Dar es Salaam Kamishna Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake  waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya Stanbic Tanzania, Sioi Sumari na Shose Sinare walifikishwa mahakamani hapo kusikiliza rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri. Jamhuri imekata rufaa kupinga kufutwa shitaka namba 8 linalowakabili wote kwa pamoja la utakatishaji fedha linalowakabili. Hata hivyo, mahakama hiyo itapanga tarehe ya kusikilizwa shauri hilo siku itakayotangazwa. Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la kula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na sheria na walifikishwa mahakamani kwa mara

Shilole, Vanessa Wamaliza Bifu Lao

Image
      Shilole (kulia)  akipashana jukwaani na Vanessa kabla ya shoo hiyo kuanza. Vanessa na Shilole wakijaribu kuelezea juu ya bifu lao. Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM, Hamisi Mandi ‘B12’, akiwakaribisha Shilole na Vanessa Mdee tayari kwa kufanya shoo hiyo. Shilole akifanya makamuzi. Vanessa akikamua jukwaani. Baadhi ya mashabiki wakifuatilia shoo hiyo. WAREMBO wanaofanya vyema kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Vanessa Mdee, usiku wa kuamkia leo wameweza kuvunja bifu lao ambalo limekuwa likivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukamua kwenye steji moja ndani ya ukumbi wa Bilicanas. Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

BREAKING NEWZ:Vurugu Tena Bungeni, Ni Kuhusu Wanafunzi 7000 wa UDOM Waliotimuliwa.

Image
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali itikadi ya vyama vyao, leo wametoka nje ya ukumbi wa bunge hilo baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kukataa kujadiliwa kwa kauli ya serikali kuhusu wanafunzi 7000 wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) waliosimamishwa. Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kutekeleza agizo la Maziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako hivi karibuni kiliwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke chuoni hapo mara moja. Wabunge waliwasilisha hoja kwa Naibu Spika, Tulia Ackson ili kulishinikiza bunge kuijadili kauli ya serikali kuhusu wanafunzi hao waliotimuliwa ambapo Naibu Spika alikataa kusikilizwa hoja hayo ndipo vurugu zikaanza na kumlazimu Naibu Spika kufunga Kikao cha Bunge kilichokuwa kikiendelea na kuwaamuru wabunge wote watoke nje. Juzi, lilitolewa tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kuondoka chuoni hapo. Tangazo hilo lilieleza kuwa k

Lungi alinanga penzi la Wolper, Harmonize

Image
Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ STORI: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA MSANII wa filamu wa kitambo, Lungi Maulanga amelinanga penzi na Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ akisema kuwa, anachoona ni kama Wolper anatembea na mdogo wake. Lungi Maulanga Akiuzungumzia uhusiano wa mastaa hao, Lungi alisema alijisikia vibaya sana kuona shosti wake Wolper kafa, kaoza kwa Harmonize kutokana na tofauti kubwa iliyopo kati yao. “Unajua Wolper ni kama mdogo wangu na shosti wangu hivyo siwezi kumuacha apotee, mimi nitamuita tutaongea kwa kina, kama atashikilia msimamo wake nitamuacha kwa sababu si unajua mtu akishapenda, lakini kiukweli hawajaendana,” alisema Lungi.

WANAWAKE WAANDAMANA WAKIDAI KUKOSA WANAUME WA KUWAPA UJAUZITO

Image
Wanawake katika jimbo la Ndeiya nchini Kenya walifahamisha kuwa waume zao wanashindwa kuwapa ujauzito kutokana na mwenendo wa unywaji wa pombe haramu ambazo zinaathiri nguvu za kiume. Katika maandamano ya amani yaliofanyika katika kituo cha biashara cha Thigio, wanawake walioandamana Alhamisi walifahamisha kukerwa na wanaume wanaojihusisha na ulevi kupita kiasi. Nancy Wangare alifahamisha kuwa katika kijiji hicho wanawake wachache walioolewa wamevumilia kwa kiasi kikubwa kutokana na upungufu wa nguvu za kiume kwa waume zao kutokana na pombe wanazokunywa. Mmoja miongoni mwa wanawake walikuwa wakiandamana alifahamisha kuwa iwapo tabia hiyo ya ulevi haitorekebishwa basi itawalazimu kutoka nje ya ndoa zao na bila wao kujua lolote na kuwahudumia watoto wasiokuwa wao

Nyongeza ya Majina Kidato cha 6 Walioteuliwa Kujiunga JKT

Image
NYONGEZA YA MAJINA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2016. VIJANA WAFUATAO WAMEONGEZWA KUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KATIKA MAKAMBI MBALIMBALI KAMA INAVYOONEKANA HAPO CHINI. PIA BAADHI YA VIJANA WAMEHAMISHWA MAKAMBI KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI WARIPOTI KWENYE MAKAMBI KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI KABLA YA TAREHE 05 JUNI 2016. S/NO JINA SHULE KIKOSI 1 ABDILLAH RAMADHANI HAJI LILIAN KIBO MGAMBO JKT 2 ABDUL M. MTEKETA BENJAMIN WILLIAM MKAPA MGAMBO JKT 3 ABDULAZIZ SALUM AHMAD PIUS SEC.SCHOOL MARAMBA JKT 4 AGNES PETER MAGANGA FLORIAN SEC RUVU JKT 5 AGNESS EMMANUEL KITANDU ST. MARY GORETI RUVU JKT 6 AGNESS PETER MAGANGA MARAMBA JKT 7 AJUAE DAVIS AMINIELI KANEMBWA JKT 8 ALEX MLOSO BINZA HIGH SCHOOL MARAMBA JKT 9 ALFRED AIDAN MBANO KIGONSELA HIGH SCHOOL RUVU JKT 10 ALLY KAFERA ALLY MBEZI BEACH SEC. KANEMBWA JKT 11 ALVIN ISMAEL MAKUNDI ST JOSEPH CATHEDRAL HIGH SCHOOL RUVU JKT 12 AMBWENE FRANK MWAKANEMA UWEMBA SEC MARAMBA JKT 13 AMOS ASEGE NSUMBA RUVU JKT 14 AMOS KINGU OLD M

Glory Gideon Atwaa Taji la Miss IFM 2016

Image
Miss IFM 2016 Groly Gideon (katikati), akiwa kwenye pozi na mshindi namba mbili Nasra Muna (kushoto), huku kulia akiwa amepozi Neema Michael ambaye alinyakulia taji namba tatu. Miss IFM 2016 Glory Gideon (katikati), akiwa kwenye pozi na washindi wenzake wa pili hadi wa tano muda mfupi baada ya kutawazwa kushikilia taji hilo ndani ya Ukumbi wa King Solomon Namanga jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Mshindi namba mbili wa mashindano hayo Nasra Muna (katikati), akicheza staili ya shock ikiwa ni ishara ya kushngilia ushindi huo. Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo wakitumbuiza kwenye mashindano hayo. Mamiss wote waliyoshiriki mashindano hayo wakiwa kwenye pozi la pamoja kabla ya majaji kutaja washindi watano wa kinyang’anyiro hicho. Majaji wa shindano hilo wakiongozwa na Martin Kadinda wa kwanza kushoto wakijadiliana namna ya kumpata mshindi wa taji hilo. Mgeni rasmi wa mashindano hayo ambaye ni Mwenyekiti wa Vyuo Vikuu Tanzania, Zainabu Abdalah Issa