Glory Gideon Atwaa Taji la Miss IFM 2016
USIKU wa kuamkia leo warembo
zaidi ya 17 kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar,
walipanda kwenye jukwaa moja kwa lengo la kumsaka mrembo mmoja atakaye
vaa taji la Miss IFM 2016 akimrithi Sophia Macha aliyekuwa akilishikiria
taji hilo kwa mwaka uliyopita wa 2015.
Katika harakati hizo Glory Gideon ndiye
aliyeibuka kidedea kwa kutwaa taji hilo akifuatiwa na Nasra Muna
aliyetwaa taji namba mbili huku Neema Micha akikamilisha nafasi ya taji
la mshindi wa tatu.
Tano Bora ya mashindano hayo ilitangazwa
na majaji wote ambapo Jackline Evernest akianza kutajwa na kufuatiwa na
Glory Gideon, Nasra Muna ambaye alitajwa sambamba na Neema Michael huku
Happiness Mkabiba akifunga pazia la washindi watano bora kwenye
kinyang’anyiro hicho kilichofanyika ndani ya Ukumbi wa King Solomoni
uliyopo Namanga jijini Dar es Salaam usiku wa kumkia leo.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL
Comments
Post a Comment