KILA WAZIRI ATASAINI MKATABA KABLA AJAANZA KAZI - MAGUFULI
Kusuasua kwa Rais John Magufuli, kutangaza Baraza la Mawaziri kunatokana na msimamo wake wa kuwachambua watu anaotarajia kuteua katika nafasi hiyo huku akiaandaa mikataba ya makubaliano itakayokuwa mwongozo kwa mawaziri hao. Nia ya Rais, hadi kufikia hatua hiyo imetafsiriwa kwamba anataka kupata mawaziri ambao wataweza kwenda sambamba na kasi yake pamoja na wawajibikaji. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaeleza kwamba kwa sasa Rais Magufuli, anasuasua kutangaza baraza lake kutokana na kile kinachodaiwa ni kuandaa mikataba ambayo mawaziri baada ya kuteuliwa watalazimika kuisoma kwa muda wa siku mbili kabla ya kukubali uteuzi huo. Chanzo hicho, kilieleza kwamba wale watakaokubali itabidi wasaini mkataba huo ili kukukabiliana na matakwa ya mkataba huo. “Kwa sasa huyu jamaa anaandaa mikataba kwa ajili ya kuwapatia Mawaziri na Manaibu wake na wanatakiwa kuisoma ndani ya siku mbili na yeyote atakayekubaliana na mkataba huyo atalazimika kuisaini. “Mikataba...