Chanzo Lulu Kutodumu na Wanaume Chatajwa

Chanzo Lulu Kutodumu na Wanaume Chatajwa
 Ubuyu! Licha kujaliwa umbo matata na mvuto wa aina yake, staa wa Bongo Movies Elizabeth Michael ‘Lulu’, anadaiwa kutodumu na mwanaume, Ijumaa Wikienda limetajiwa chanzo cha hali hiyo.
Kwa mujibu wa sosi wa ndani wa familia ya staa huyo, chanzo kikubwa cha Lulu kutodumu na mwanaume anayempata kama mwandani wake ni mama yake, Lucresia Karugila.
Ilidaiwa kwamba, kama ilivyokuwa kwa Wema Sepetu zamani, mama yake, Miriam Sepetu alidaiwa kumwekea ‘patroo’ mrembo huyo kwa kumchagulia mwanaume wa kuwa naye, jambo lililomfanya Wema ashindwe kudumu na mwanaume mmoja.
“Hiyo ndiyo hali halisi inayomkuta Lulu. Yaani ni kama Wema zamani,” kilisema chanzo hicho.
“Unajua mama Lulu anataka mwanaye awe na mwanaume mwenye fedha ili amsaidie kuhudumia familia.
“Inapotokea mwanaume anashindwa kuhimili matumizi, basi mama huyo humtaka mwanaye kusitisha uhusiano huo mara moja kwani unakuwa si wa masilahi,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilitinga nyumbani kwa Lulu na mama yake, Mbezi-Tangibovu jijini Dar ambapo mwandishi wetu alimkuta mama Lulu kisha kumsomea ‘mashtaka’ hayo;
Ijumaa Wikienda: Maisha unayaonaje kwa sasa mama?
Mama Lulu: Si kama hivi unavyoona wewe!
Ijumaa Wikienda: Yapo madai kuwa wewe umekuwa ‘stelingi’ wa Lulu hadi kwenye uhusiano wake na wanaume, hili likoje?
Mama Lulu: (kwa uso wa kishari kidogo) mimi ni mama yake, ni mzazi gani anaweza kumwacha mwanaye hata kama anaona kabisa aendako anapotea?
Ijumaa Wikienda: Madai ni kwamba umekuwa ukimchagulia wanaume wa kuwa naye, lakini lazima awe na fedha ya kutosha, ni kweli?
Mama Lulu: Nimesema yule ni mwanangu, lazima nimuongoze katika mstari mnyoofu.
Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo mtu yeyote mwenye fedha nzuri, akija hata sasa hivi ni ruksa?
Mama Lulu: (kicheko) teh…teh…teh…Ijumaa Wikienda bwana….!
Baada ya kuzungumza na Mama Lulu, mwandishi wetu alimtafuta Lulu ili kusikia kauli yake lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Chanzo: GPL

Comments

Popular posts from this blog