Kashfa nzito
Wasomali wakiwa chini ya ulinzi.
WAMENASWA! Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa wa Machimbo, Kata ya Segerea, Ilala jijini Dar es Salaam wamewanasa watu 105 raia wa Somalia wakidaiwa kuwa safarini kwenda nchini Afrika Kusini, Uwazi linakupa kwa undani.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea saa 11 alfajiri ya Alhamisi iliyopita kwenye nyumba ya kigogo mmoja aliyekuwa mfanyabiashara mkubwa Dar (jina lipo) ambaye ni marehemu. Nyumba hiyo iliyopo Tabata Segerea kwa sasa inasimamiwa na mtoto wa marehemu aitwaye Mariam.
Polisi wakiwa katika eneo la tukio.
Waadishi wa habari hii walifika eneo la tukio muda mfupi baada ya kukamatwa kwa watu hao ambapo zoezi hilo lilikuwa likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kipolisi Buguruni, Ibrahim Nkindwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata Shule, Bakar Goti baada ya kutonywa kuwepo kwa watu hao katika nyumba hiyo iliyopangishwa kwa Zabibu Umwiza raia wa Burundi ambaye ndiye anadaiwa kuwahifadhi watu hao.
ainabu alikimbia baada ya polisi kufika na silaha za moto.
Kwa mujibu wa shuhuda mmoja, kugundulika kwa Wasomali hao kulifuatia kuwasili kwa lori moja kwenye nyumba hiyo usiku wa saa tisa.
….Wakiwa kwenye basi la polisi.
“Baada ya lori kufika usiku huo, geti likafunguliwa. Halafu kukaanza kusikika vishindo vya tii…tii…tii! Kumbe jamaa (Wasomali) walikuwa wakiruka chini mmojammoja kutoka kwenye lile lori na kuingia ndani.
“Ndipo jirani mmoja aliamua kutoa taarifa polisi ambao walifika na kuwakuta jamaa wamerundikana ndani kwenye vyumba tofauti. Mia moja na tano ni wengi sana,” alisema shuhuda huyo.
Comments
Post a Comment