HUYU NDO GAIDI ALIYE FANYA MASHABULIZI YA NCHINI UFARANSA
Mtuhumiwa namba aliyepanga mashambulizi ya Paris, Abdelhamid Abaaoud ‘Mastermind’ enzi za uhai wake.Abdelhamid Abaaoud akifanya mazoezi ya kulenga shabaha.
…Akiwafunga na kuwaburuza kwenye gari mateka aliowaua tayari.Jinsi oparesheni ya kuwasaka watuhumiwa kwenye Kitongoji cha Saint-Denis, Paris yalivyofanyika jana.Mmoja wa watuhumiwa akiwa amepigwa risasi na kuuawa.
Polisi na kikosi cha uokoaji wakiwa kazini kwenye oparesheni ya jana.Mtuhumiwa namba mbili wa mashambulizi ya Paris, Hasna Ait Boulahacen “The Cow Girl’.
Hasna Ait Boulahacen alivyopishana na askari kwenye lango la nyumba waliyokuwa wakiishambulia askari kuwasaka watuhumiwa.Uvamizi wa askari katika Kitongoji cha Saint Denis, jana.Polisi walivyojipanga kukivamia Kitongoji cha Saint Denis, Paris jana.
Watu walivyouawa kwenye shambulio la Ijumaa, Paris, Ufaransa.
Paris, Ufaransa
MWENDESHA mashtaka
nchini Ufaransa amethibitisha kwamba, mtuhumiwa namba aliyepanga
mashambulizi ya Paris, Abdelhamid Abaaoud ameuawa kwenye operesheni
maalum ya kumsaka ilioyoanza jana.
Abaaoud ndiye alikuwa
akisakwa na polisi waliovamia nyumba moja katika Kitongoji cha Saint
Denis kilichopo Kaskazini mwa Paris, Ufaransa.
Awali, mwendesha mashtaka
wa Paris Francois Molins alikuwa amesema Abaaoud na mshukiwa mwingine
Salah Abdeslam hawakuwa miongoni mwa watu wanane waliokamatwa.
Hata hivyo, miili ya watu wawili waliouawa ilikuwa bado haijatambuliwa na baada ya uchunguzi imebainika kwamba Abooud aliuawa.
Hayo yakijiri, wabunge nchini Ufaransa wanatarajiwa kupiga kura kuongeza muda wa kutekelezwa kwa hali ya hatari.
Wapiganaji wa Islamic State
(IS), ambao wanadhibiti maeneo ya Syria na Iraq walisema ndio
waliohusika katika mashambulio hayo yaliyoua watu 129 na wengine 400
kujeruhiwa Ijumaa iliyopita
Comments
Post a Comment