Posts

Nafasi Ya Kazi Kwa IT Kutoka Car & General Trading Limited

Image
Car & General Trading Limited is looking for well qualified and competent candidates for the following post: IT Person Qualifications: • Minimum 2 yrs experience in IT • Web graphic and animation design • Knowledge in database programming • Knowledge of Web and Mobile Applications • Good communication skills • Excellent diagnostic and problem solving • Knowledge in Software development • Technical Support Skills/IT Support Education Qualification: Degree in computer Science, Engineering or relevant field Persons with proven experience in IT are encouraged to apply before 20/712018. Package: An attractive salary to be offered to experience candidate. Apply to: HR Manager, Car & General Trading / Tanzania Limited. P.O. Box: 1552, Dar Es Salaam. Tanzania. Source: The Guardian July 11, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Jacob Kingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kailima Ramadhani kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Thomas Mihayo kuwa Kamishn

SALAMBA,KAGERE WAIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI YA KOMBE LA KAGAME CUP 2018

Image
Washambuliaji wapya wa  klabu ya Simba wameisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya APR  ya Rwanda Mchezo wa Michuano ya Kagame inayoendelea jijini Dar Salaam kwenye viwanja vya Chamazi na Taifa. Katika mchezo huo uliokuwa na mashambulizi ya zamu kwa zamu, ulimalizika dakika 45 za kwanza bila timu yoyote kuona bao. Mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote zilionesha kukamiana zikiwa na lengo la kucheka na nyavu ambapo mnamo dakika ya 66, Kinzingabo aliweza kuiandikia APR bao la kwanza. Ilichukua takribani dakika 6 baadaye Simba kuweza kusawazisha ambapo katika dakika ya 72, mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa, Adam Salama alifunga na kuufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1. Wakati mpira ukiwa katika dakika za nyongeza, straika hatari mpya, Meddie Kagere aliifungia Simba bao la pili na la ushindi kwa njia ya penati baada ya kiungo Said Ndemla kuangushwa katika eneo la hatari. Kwa Matokeo hayo Simba na Singida a

WIZARA YA AFYA YATANGAZA RASMI KUPOKEA HOSPITALI ZA RUFA ZA MIKOA

Image
WIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuanzia Juali 1 2018  imepokea Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa OR-TAMISEMI . Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala. “Hospitali ambazo tumezipokea zina jumla ya vitanda 7,474 na jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao Wauguzi ni 3,960, Madaktari 536, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni 182, na waliobakia ni watumishi wa kada zingine mbalimbali za Afya” alisema Waziri Ummy. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo juu ya matangazo yaliyo kwenye mbao mapema leo wakati alipofanya ziara ya kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala. Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ambazo Wizara imezipokea ni Hospit

Breaking News: Gari Lateketea kwa Moto Daraja la Kigamboni

Image
MOTO umewaka na kuteketeza gari dogo aina ya Toyota Ractics, leo Jumatatu, Julai 2, 2018 katika Daraja la Nyerere (Kigamboni) jijini Dar es Salaam huku mwenye gari akifanikiwa kutoka nje ya gari na kukimbilia sehem salama. Chanzo cha ajali hiyo imedaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme wa gari hiyo pindi limefika kwenye kukata ticket hitilafu hiyo imetoka na kuanza kuungua, juhudi za kuliokua gari hilo zilifanyika na kufanikiwa kuuzima moto huo hali likiwa limeshaungua mbele. Inadaiwa ajali hiyo imetokea wakati dereva wa gari hilo akilipia fedha ili avuke ng’ambo, lakini pia huku kukiwa hakuna taarifa ya majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo. Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.

Mshambuliaji wa Croatia atimuliwa Urusi, kisa kukataa kuivaa Nigeria

Image
Mshambuliaji timu ya taifa ya Croatia Nikola Kalinic amerudishwa nyumbani baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu. Kocha wake, Zlatko Dalic alimtaka mshambuliaji huyo kuingia katika dakika za mwisho katika mechi yao dhidi ya Nigeria, akagoma. Kalinic aligoma akidai alikuwa na maumivu ya mgongo. Hivyo akakataa kuinuka na kuingia kama kocha huyo alivyotaka. Pamoja na kwamba aliomba msamaha baada ya Croatia kushinda kwa mabao 2-0 katika mechi hiyo, Dalic alikataa katakata na kusisitiza, arejee nyumbani Croatia.

CHIDI BENZ ANASWA NA MZIGO WA BANGI DODOMA

Image
STAA wa Bongo Fleva, Rashidi Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ amekamtwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na mzigo wa bangi kiasi cha gramu tano. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Jumatatu, Juni 18, 2018 wakati akizungumza na wanahabari jijini humo baada ya kumtia mbaroni msanii huyo.   Hii ni mara ya pili kwa Chidi kukamatwa na madawa ya kulevya mwaka huu mkoani Dodoma huku akidai kuwa alishaacha kutumia madawa hayo na anaendelea na matibabu Sober House. Hii ni sehemu ya taarifa ya polisi kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa mbaliombali akiwemo Chidi.

Mbowe Apata Pigo, Aanguka Ghafla, Akimbizwa Muhimbili

Image
MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuanguka ghafla alfajiri ya leo Jumatatu, Juni 18, 2018, hii ni kwa mujibu wa wakili wake Jeremiah Mtobesya. Wakili Mtobesya, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mteja wake alianguka leo akiwa nyumbani kwake, hivyo asingeweza kufika mahakamani kwa siku ya leo. Akiwasilisha taarifa hiyo, Wakili Mtobesya ameeleza kuwa Mbowe ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi namba 112 ya 2018 amefiwa na kaka yake Henry Mbowe usiku wa kuamkia leo. Naye Msemaji wa Chadema, Makene amesema; “Ni kweli Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mh. Freeman Mbowe amepatwa na shida ya kiafya asubuhi ya leo akiwa nyumbani kwake, na amelazwa Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Dharura. Tutaenelea kuwajuza.” Aidha, awali Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliiambia mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa Mbowe na wenzake w

BREAKING: BAJETI YA UPINZANI YAZUIWA BUNGENI, WENYEWE WASUSA

Image
#GLOBALHABARI: Hotuba ya Bajeti mbadala ya Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imekataliwa bungeni kutokana na kuwasilishwa nje ya utaratibu. Wabunge wa upinzani (isipokuwa wanaomuunga mkono Prof Lipumba ) wameondoka kwenye ukumbi wa Bunge.

Messi ataweza Kujibu mabao HAT-TRICK za Ronaldo leo dimbani?

Image
Cristiano Ronaldo jana alifanikiwa kufunga mabao matatu pekee 'Hat-trick' katika mchezo wake wa kwanza wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu dhidi ya Spain nchini Urusi. Mabao hayo yaliisaidia Ureno kwenda sare ya 3-3 dhidi ya mabingwa hao wa Kombe la Dunia kwa mwaka 2010 huko Afrika Kusini. Hattrick hiyo imekuwa ya 51 kwa Ronaldo katika soka la ushindani huku akiifunga akiwa na umri wa miaka 33, moja ya wachezaji wenye umri mkubwa katika mashindano hayo. Rekodi hizo kadhaa za Ronaldo zinamfanya Messi ambaye hajawahi kutwaa ubingwa wa taji hilo kujipanga kwa ajili ya kulipiza mapigo. Mara nyingi wawili hawa wakiwa viwanjani wamekuwa ni watu wa kuvunja na kuandika rekodi za aina yake na kipekee. Messi atakuwa anashuka dimbani kuingoza Argentina kucheza kibarua chake cha kwanza leo dhidi ya Iceland. Pengine anaweza akajibu kwa kufunga pia mabao kama aliyofunga mpinzani wake ingawa huu ni mchezo wa soka mambo yanaweza kuwa tofauti. Tusubiri tuone n

Zitto amsifu Peneza kubadili taswira ya bajeti

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amempongeza Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Kigoma Upendo Peneza (CHADEMA) kuwa amefanikiwa kuacha alama ndani ya bunge la Tanzania akiwa na muda mfupi ndani ya bunge. Zitto ametoa pongezi hizo ambapo amesema Peneza anaingia katika rekodi za Wabunge waliotumia nafasi yao kushawishi jambo lenye faida kubwa kwa jamii na likafanikiwa ikiwa ni baada ya Serikali kutangaza kuondoa kodi ya VAT kwenye Taulo za Kike zinazotumika na Wanawake kipindi cha hedhi. “Kumekuwa na juhudi za kuleta mabadiliko haya miaka mingi kutokana na kazi za Mashirika kama TGNP Mtandao, SNV, Msichana Initiative nk. Upendo, licha ya kuwa na miaka 2 tu Bungeni aliweza kubeba hoja hii na kuiingiza Bungeni na kuunganisha Wabunge wote kutoka Vyama vyote.” ameandika Zitto Ameongeza “Licha ya kwamba kampeni yake ilikuwa ni Watoto wa shule wapewe Taulo hizi bure ( litafika tu hilo kupitia mamlaka za Serikali za Mitaa ), amepata mafanikio

ZARI: Nilikutana na Diamond ‘DM’

Image
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ H AKUNA ufalme unaodumu milele hapa duniani kwa sababu unaambiwa hata ile iliyokuwa ‘kapo’ matata Afrika Mashariki ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ bado hali ni tete. Karibu mpenzi msomaji wa Gazeti la Ijumaa katika safu yetu hii mpya ya The First We Met (Tulivyokutana Siku Siku ya Kwanza) ambapo utawasikia wanandoa mbalimbali wakiwemo mastaa na wasiokuwa mastaa wakielezea namna walivyokutana na kuunda muungano wa kimapenzi. Hii itakupa uzoefu wewe msomaji juu ya namna watu wanavyokutana na kuyajenga maisha. “Bado nakumbuka siku ya kwanza tulipokutana, kila mmoja alikuwa na aibu kumsemesha mwenzake,” hivyo ndivyo alivyoanza kusimulia Zari juu ya namna alivyokutana na Diamond kisha kufurahia maisha kabla ya hivi karibuni jahazi kwenda mrama. Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini mwake, Uganda alikozaliwa mwanamama

MZEE MWINYI AONGOZA SWALA YA EID EL FITR DAR

Image
Mzee Ali Hassan Mwinyi akitoa nasaha zake kwa waumini wa dini ya Kiislamu. Mzee Ali Hassan Mwinyi (kulia) akijumuika na waumini wengine wa Dini ya Kiislam katika  swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar esa Salaam. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum akitoa nasaha zake kwa waumini  wa dini ya Kiislamu. Taswira ya baadhi ya waumini waliojitokeza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ilivyoonekana. Meneja wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akiwa ameungana na  waumini wengine wa Dini ya Kiislam katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye Viwanja  vya Mnazi Mmoja jijini Dar esa Salaam. Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (katikati) akisalimiana na mmoja wa waumini  baada ya kumalizika kwa swala ya Eid El Fitr. Sehemu ya waumini akinamama waliojitokeza katika swala hiyo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja. Waumini wakiomba dua. RAIS Mstaafu wa Awamu ya P

Phars blogspot Inawatakia Eid Njema

Image
Wafanyakazi wote wa Kampuni ya Global Publishers & Ent. Ltd inayochapisha Magazeti ya Amani, Championi, Ijumaa, Risasi na Uwazi na Spoti Xtra tunawatakia heri ya   Sikukuu ya Eid El Fitr wadau na wasomaji wetu wote. Aidha tunawashukuruni sana sana wadau wetu wote kwa sapoti yenu kubwa mnayotupatia na kutufanya tuendelee kuwa namba moja kwenye tasnia ya habari za magazeti pendwa na michezo hapa nchini. Nasi tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi kwa asilimia zote.

MO SALAHA YUKO FITI KUWAVAA URUGUAY LEO

Image
HATIMAYE Kocha Mkuu wa Misri,Hector Cuper amesema mshambuliaji wa timu hiyo Mohamed Salah yupo kamili kwa takribani asilimia 100 kucheza mechi yao ya kwanza ya fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay leo Ijumaa, Juni 15, 2018. “Ninaweza kusema karibu asilimia 100 mchezaji Mo Salah yuko vizuri kucheza mchezo wa wetu dhidi ya Uruguay, yeye binafsi yupo tayari kucheza tunachojaribu sisi ni kumpa ujasiri tu”, amesema Cuper. Mohemed Salah aliumia bega kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Mei 26, kufuatia kukumbana na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos. Awali ilihofiwa kuwa huenda akakosa fainali hizo lakini sasa inaonekana yupo vizuri kuiwakilishi nchi yake. Misri ambayo ipo Kundi A na timu za Russia, Saudi Arabia na Uruguay leo itaanza rasmi kampeni ya kusaka ubingwa wa dunia ambapo haikupata nafasi ya kucheza fainali hizi tangu mwaka 1990 ambapo Salah alikuwa hajazaliwa. Mechi hiyo itachezwa majira ya saa 9:00 Mchana kwa saa za Afrika Mashariki, kwen

Wanawake Urusi watakiwa kutofanya mapenzi na raia wa kigeni

Image
Mbunge mmoja nchini Urusi anasema kuwa wanawake hawafai kufanya mapenzi na wageni wakati wa kombe la dunia huku akionya kuhusu watoto wanaozaliwa kutoka rangi tofauti. Tamara Plentyova mkuu wa kamati ya familia, wanawake na masuala ya watoto bungeni, alisema kuwa hata iwapo uhusiano huo utasababisha kufanyika kwa harusi, wanawake au watoto wao watachukuliwa na nwanamume huyo ambaye atakuwa raia wa kigeni. Mbunge huyo ni wa chama cha Kikomunisti, ''Hata wakiolewa, watawachukua, halafu watashindwa namna ya kurudi," Bi Pletnyova alisema katika kituo cha Govorit Moskva. "Baadaye watakuja kwangu, wasichana wakilia kwamba watoto wao wamechukuliwa''. Alisema kuwa wanawake waliopata watoto na raia wa kigeni wakati wa michezo ya Olimpiki ya 1980 mjini Moscow walisalia kuwa wanawake wasio na wanaume. ''Ni vyema iwapo ni mtu wa rangi inayofanana na yako lakini iwapo ni mtu wa rangi tofauti basi kunakuwa na shida''. ''

Ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh awamu ya pili waendelea kutekelezwa kwa zaidi ya aslimia 80- Mbulu

Image
muonekano wa jengo la wodi ya mama na mtoto kituo cha Afya Dongobesh likiwa katika hatua ya ukamilishaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu inategemea kukamilisha ujenzi wa majengo matano ya kituo cha Afya Dongobesh ifikapo Juni 30 2018, hatua hii imefikiwa ikiwa ni utekelezaji wa   kiwango cha aslimia 80 kilichobainishwa baada ya kufanyika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh,tathimini hiyo ilitolewa na   timu ya Wataalam toka Tamisemi, wakilishirikiana na wataalam toka   Mkoa wa Manyara .   Timu ya wataalam wakiwa katika moja ya majengo mapya ya kituo cha afya wakiendelea na ukaguzi. Timu hizo ziliweza kufanya ukuaguzi wa majengo hayo mapya yanayoendelea kukamilishwa kabla ya Mwezi Juni kukamilika ili kubaini kama   kiasi cha fedha Tsh.   Milioni 400   zilizotolewa   na Serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo unakamilika kwa wakati. Mgawao huo wa fedha uliotolewa ikiwa na mgawao awamu ya pili baada ya maeneo mbalimbali

Breaking News: Moto Mkubwa Waibuka Kariakoo

Image
Moto ukitekeleza ghorofa ya juu ya jengo hilo eneo la Kariakoo. MOTO mkubwa umeibuka Kariakoo katika mitaa ya Livingstone na Aggrey na unaendelea kuteketeza maduka. Tayari vikosi vya zimamoto vipo eneo la tukio kupambana na moto huo unaoendelea kuteketeza jengo la ghorofa ambalo lina maduka katika ghorofa ya chini. Moto huo ulianzia kwenye ghorofa ya kwanza katika jengo hilo lenye ghorofa mbili ambako kulikuwa na stoo ya vitu mbalimbali ambavyo vimeteketea kwa moto huo ambao moto huo ulielekea katika ghorofa ya juu. Chanzo cha moto huo hadi tunakwenda mitamboni kilikuwa hakijajulikana. Vikosi vya Zimamoto vikiendelea na kazi Wakazi wa Dar es Salaam wakishuhudia moto huo.