UKWELI KUHUSU WANAFUNZI UDSM WALIOFARIKI DUNIA AJALINI
TAARIFA zinazosambaa mitandaoni zikisema mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Maria Godian Soko amefariki dunia kwa ajali usiku wa kuamkia leo maeneo ya Ubungo Riverside, Dar es Salaam, akiwa anakimbizwa hospitali kwa matatizo ya ujauzito, zimekanushwa na Katibu Mteule wa Serikali ya Wanafunzi Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika chuo hicho, Hussein Amri Aman, aliyesema kwamba kwamba marehemu hakuwa na tatizo hilo. Amri amesema marehemu Soko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya pumu kwa muda mrefu, hali iliyokuwa ikisababisha apoteze fahamu, na ndiyo sababu kuu iliyomfanya awe anakimbizwa hospitali kwa gari la wagonjwa (ambulance). “ Marehemu Maria alikuwa na matatizo ya pumu ambayo yalimsababishia kifua kubana hadi kuzimia, majira ya saa mbili kasoro usiku tulifanya utaratibu wa kuita ambulance ya chuo na kumchukua hapa Mabibo hostel kumpeleka hospitali ya chuo kwa matibabu zaidi” Ameongeza: “ Wakati taratibu za kumpeleka hospitali ya c