Kajala amkimbiza mke wa P Funk
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amedaiwa kusababisha mke wa prodyuza mahiri Bongo, Paul Matthysse, Samira afungashe virago vyake tayari kwa kurudi kwao. Mke huyo wa P Funk amedaiwa kufikia uamuzi huo baada ya mwanaume huyo kuonekana kurudisha majeshi kiaina kwa Kajala aliyewahi kuwa mchumba’ke zamani huku picha na video mbalimbali za kimalovee zikivuja. Mtu wa karibu na mke wa P Funk alivujisha kuwa, Samira amefikia hatua hiyo baada ya kushuhudia matukio mbalimbali ya P Funk na Kajala na kukosa majibu yaliyonyooka. “Unajua P Funk kila alipokuwa akielezwa kuhusu Kajala alikuwa hanyooshi maelezo ingawa machoni alionesha kumpenda Kajala. “Mkewe ambaye kwa sasa ni mjamzito, ameishi kwenye kipindi kigumu sana. Anashindwa kumuelewa P Funk kwani watu kibao wanampigia na kumuambia wamemuona mumewe akiwa na Kajala,” alidai mtu huyo wa karibu. Akizidi kushusha data, mtu huyo wa karibu na Samira alidai kuwa, mara kadhaa P Funk amekuwa akielezwa kuh