Masogange kuagwa Leaders, kuzikwa nyumbani kwa.

Video queen maarufu Bongo Agnes Gerald maarufu Kama Masogange anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao jijini Mbeya ambako ndiko wazazi wake waliko.

Akizungumza na www.eatv.tv dada wa Agnes anayejulikana kama Emma Gerald, amesema mwili wa Agnes  utaagwa jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders,  na kisha kusafirishwa kuelekea mkoani Mbeya kwa mazishi

“Tutaaga kesho asubuhi saa 3 pale Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma Gerald.
Sambamba na  hilo muigizaji Steve Nyerere ambaye yuko karibu na familia ya Agnes amewataka wasanii kujitokeza kwa wingi leaders jioni ya leo, ili kujadili utaratibu wa mazishi na mengineyo.

Agnes Masogange amefariki jana April 20, kwenye hospitali ya Mama Ngoma baada ya kulazwa kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta kwa tatizo la pneumonia

Comments

Popular posts from this blog