Jinsi ya Kupika Pilau ya Zabibu Kavu

KWENYE ukurasa huu wa Mapishi ya Amani tutaona jinsi ya kupika pilau ya zabibu kavu ambayo ni tamu sana.
MAHITAJI:
-Mchele
-Viungo vya pilau
-Mafuta ya kupikia
-Nyama
-Vitunguu swaumu
-Vitunguu maji
JINSI YA KUPIKA:
Andaa mchele wako uoshe kisha weka pembeni, baada ya hapo chemsha nyama yako na yenyewe iweke pembeni, ukimaliza weka sufuria kwenye moto na mafuta, anza kukaanga vitunguu. Weka kitunguu swaumu, ukimaliza kaanga weka viungo vikaangike vizuri kisha weka mchele ukaange sana mpaka uive wakati unakaanga weka na nyama ili vikaangike kwa pamoja ukimaliza weka maji na chuvi pika pilau lako taratibu.
Wengine hupendelea kuweka viazi pia ambapo huvikaanga na mafuta na viungo lakini sio lazima sana unaweza kupika pilau la nyama tu.  Pilau likishaiva sasa chukua zabibu zako kavu ziweke kwenye chakula, geuzageuza kisha funikia liache kidogo kwanza. Baadaye pakua pilau lako litakuwa tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog