Zitto Kabwe: Nipo tayari kwa lolote

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa yupo tayari kukamatwa na polisi lakini pia yupo tayari hata kuuwawa kwa ajili ya kuisemea trilioni 1.5 ambayo CAG amesema haijatolewa maelezo imetumikaje.

Zitto Kabwe amesema hayo leo April 18, 2018 baada ya Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole kusema kuwa wapo viongozi wa upinzani wanasema uongo juu ya ripoti Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutaka watu hao wachukuliwe hatua. Kufuatia kauli hiyo Zitto Kabwe amesema kuwa anauhakika kuwa serikali ya awamu ya tano imeshindwa kuonyesha matumizi ya trilioni moja na bilioni mia tano.

"Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG. Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, naapa kwamba Serikali ya CCM ya awamu ya tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni moja na bilioni mia tano. Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo"

Aidha Zitto Kabwe amekwenda mbali na kusema kuwa yupo tayari hata kufa kwa kuwa anaamini mawazo yake hayawezi kufa hata kidogo "nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo kwani mawazo yangu hayatakufa. Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie" alisisitiza Zitto Kabwe

Mwisho wa wiki iliyopita, Mbunge wa Kigoma Mjini kwa triketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliizungumzia kwa mapana zaidi taarifa ya CAG na kuonyesha mambo ambayo serikali imetuhumiwa kufanya ikiwa pamoja na upotevu wa fedha zaidi ya Trilioni 1.5 ambayo haina maelezo imetumikaje.

Comments

Popular posts from this blog