SHUGHULI YA NDOA YA ALIKIBA IMEANZA KENYA – Picha

ILE siku iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu kushuhudia ndoa ya Staa wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ hatimaye imewadia na leo Aprili 19, 2018 mkali huyo anafunga ndoa yake na mrembo Aminah Rikesh Khaleef mjini Mombasa nchini Kenya.


Tayari wapenzi hao wanaofunga ndoa, Mashehe, ndugu na marafaiki wameshafika eneo ambapo ndoa hiyo inafungwa na tayari shughuli imeshaanza kama picha zinavyoonyesha.
Watu wa karibu wa msanii huyo wameonekana mjini Mombasa, Kenya kwa ajili ya kuhudhuria ndoa hiyo. Baadhi ya picha tayari zimeanza kusambaa mitandaoni zikiwaonyesha watu hao akiwemo msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti na dada yake Alikiba, Zabibu na wengine.


Tazama video ushuhudie mwenyewe.

Comments

Popular posts from this blog