Kajala amkimbiza mke wa P Funk

 


 Muigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amedaiwa kusababisha mke wa prodyuza mahiri Bongo, Paul Matthysse, Samira afungashe virago vyake tayari kwa kurudi kwao.

Mke huyo wa P Funk amedaiwa kufikia uamuzi huo baada ya mwanaume huyo kuonekana kurudisha majeshi kiaina kwa Kajala aliyewahi kuwa mchumba’ke zamani huku picha na video mbalimbali za kimalovee zikivuja.

Mtu wa karibu na mke wa P Funk alivujisha kuwa, Samira amefikia hatua hiyo baada ya kushuhudia matukio mbalimbali ya P Funk na Kajala na kukosa majibu yaliyonyooka. “Unajua P Funk kila alipokuwa akielezwa kuhusu Kajala alikuwa hanyooshi maelezo ingawa machoni alionesha kumpenda Kajala.

“Mkewe ambaye kwa sasa ni mjamzito, ameishi kwenye kipindi kigumu sana. Anashindwa kumuelewa P Funk kwani watu kibao wanampigia na kumuambia wamemuona mumewe akiwa na Kajala,” alidai mtu huyo wa karibu. Akizidi kushusha data, mtu huyo wa karibu na Samira alidai kuwa, mara kadhaa P Funk amekuwa akielezwa kuhusu …usaliti wake kwa Kajala lakini alikuwa akijitetea kwa kutumia kigezo cha kumlea mtoto aliyezaa na Kajala (Paula).
“Yani Samira alikuwa akimbana P Funk lakini mara kadhaa P (P Funk) alikuwa anasema hakuna lolote zaidi ya yeye kwenda kumcheki mtoto hususan anapokuwa shuleni,” alisema mtu huyo.

Akizungumzia picha zilizovuja, rafiki huyo wa Samira alisema shosti wake alivumilia zile picha za awali zilizomuonesha P Funk akiwa supermarket na Kajala lakini zilivyokuja kuvuja video wiki hii, ameona isiwe tabu afungashe virago vyake.

“Hii video ya wiki hii ni balaa, anaonekana kabisa Kajala akiwa mbele ya gari, P Funk akiwa nyuma ya gari, anainuka na kumbusu Kajala huku mtoto wao Paula akishuhudia, yani pale ni live bila  chenga,” alisema rafiki huyo wa Samira na kuongeza: “Anaondoka nafikiri itakuwa Jumamosi au Jumapili ya wiki hii lakini tayari ameshafungasha kila kilicho chake kwenda kwao Arusha.

Risasi Jumamosi lilivutia waya Samira ambapo alipopatikana na kuulizwa kuhusu suala la yeye kufungasha virago, alijibu kwa kifupi kwa hasira. “Ndio…na nyinyi nikiondoka inawahusu nini? Niacheni nimechoka jamani.”

Kajala na P Funk ambao walikuwa wapenzi kabla ya P Funk hajamuoa Samira, hawakupatikana walipotafutwa juzi lakini hata hivyo, kwa nyakati tofauti Kajala amekuwa akikanusha kuwa hajarudiana na P Funk na kumtaka Samira asijishtukie. Samira na P Funk wamedumu kwenye ndoa kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kupata watoto wawili.

Comments

Popular posts from this blog