Posts

Madaktari wasimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili.

Image
Picha ya mtandao Madaktari(baadhi) Hospitali ya Kenyatta wamesimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili. Walibaini kosa hilo wakiwa tayari wamempasua mgonjwa huyo na kugundua hakuwa na tatizo la kuvilia damu walilotakiwa kulitibu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare, amevieleza vyombo vya habari ya kuwa kulikuwa na wagonjwa wawili, mmoja ndiye aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwani alikuwa na damu iliyovimba ndani ya kichwa. Tare ameeleza kuwa waliohusika na kwa sasa tayari wanafanyiwa uchunguzi kupitia sakata hilo ambao ni daktari wa upasuaji wa ubongo, muuguzi, na mtalaamu wa dawa za usingizi. Hatahivyo ameomba radhi na kueleza kuwa mgonjwa halisi aliyekuwa anatakiwa kupasuliwa kichwa tayari ameshafanyiwa upasuaji huo na afya yake tayari imeanza kuimarika.

Mkurugenzi wa NEC amfungukia Mh.Mbowe

Image
Baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe kulalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutokutenda haki katika uchaguzi mdogo uliokuwa ukifanyika mwezi uliopita, Mkurugenzi wa Tume hiyo, Kailima Ramadhani ameibuka na kusema kuwa hawezi kujibu matusi ya kiongozi huyo. Siku chache zilizopita, Mbowe katika mkutano wake na wanahabari alilalamikia Tume hiyo kutotenda haki huku akisema kuwa Chama cha Mapinduzi(CCM) kilipendelewa. Hata hivyo Mbowe alieleza kuwa wizi uliokuwa unafanywa katika uchaguzi huo ulikuwa ni wa kitoto sana huku akielez kuwa walituma barua kwa Mkurugenzi wa NEC hakujibu na alipopigiwa simu hakujibu. Baada ya Mbowe kutoa malalamiko hayo, Kailima ameibuka na kujibu madai hayo kuwa “Nimesikitishwa sana na kiongozi wa ngazi za juu kutamka matusi hadharani. Mimi nimeenda jandoni siwezi kujibu matusi hayo.” Hata hivyo Kailima ameeleza kuwa NEC inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu, maadili na miongozo ya uchaguzi wakati wot...

Simba Inakutana Na Nguli Wa Afrika

Image
MWAKA 2003, Simba ikiwa na kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji vijana na wazoefu ilifanikiwa kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini safari yao haikuwa nyepesi . Katika hatua ya awali Simba iliitoa Botswana Defence Force XI ya Botswana, Raundi ya Kwanza ikaitoa Santos ya Afrika Kusini. Baada ya hapo ikakutana na Zamalek ya Misri ambao ndiyo walikuwa mabingwa watetezi. Beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawassa anasimulia kwa ufupi juu ya mchezaji aliyekuwa staa wa Zamalek, Hossam Hassan. Pawassa anasema: “Kipindi hicho ndiyo Zamalek ilikuwa imetoka kupewa ubingwa, tukapangwa kukutana nao katika Raundi ya Pili ambayo ni ya mtoano kabla ya kuingia Hatua ya Makundi. “Kwanza kabla ya kuelekea mchezo huo tulipewa presha kubwa sana kwa kuwa Zamalek walikuwa katika ubora wa juu, nakumbuka kabla ya mchezo huo nilipata takribani SMS zaidi ya 250, lakini nyingi kati ya hizo zilikuwa ni kuhusu Hossam Hassan. “Niliambiwa naenda kukutana na mche...

Shilole Ahukumiwa kwa Utapeli, Mahakama Kukamata Mali Zake!

Image
Shilole akiwasili mahamani hapo. MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 14 na mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya utapeli kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye shoo. …Akiwa na mumewe Uchebe. Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu leo Machi 1, 2018, imethibitika kuwa Shilole alilipwa kiasi cha Tsh. Milioni tatu kwa Mary Musa kwa ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka mwaka jana 2017 katika Ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam lakini alishindwa kutokea kwenye shoo hiyo kama walivyokubaliana. …Akiingia ndani ya chumba cha mahakama. Kutokana na kitendo hicho,  mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo walipandwa hasira na kufanya fujo huku wakiharibu mali ukumbini hapo hivyo kumsababishia mwandaaji ambaye ni Mary, hasara ya Tsh. Milioni 14 ambazo mahakama imeamua Shilole azilipe kama fidia kwa mlalamikaji. Mlalamika...

Wimbo wa Kibamia wamponza Roma Mkatoliki, afungiwa miezi sita

Image
 Msanii Roma Mkatoliki  Msanii wa Bongo Fleva, Roma Mkatoliki amefungiwa miezi sita kutojihusisha na Muziki ikiwa ni kutekeleza azma ya Serikali kwa kile kinachodaiwa kukiuka maadili ya jamii za kitanzania kwenye wimbo wake wa "KIBAMIA". Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amesema kuwa Roma amedharau wito wa serikali ambapo leo aliitwa ili ahojiwe   kutokana na wimbo wake huo ikiwa ni hatua ya pili mara baada ya Baraza la Sanaa Nchini Basata kumuita na kumtaka arekebishe baadhi ya sehemu katika wimbo huo. "Tumempigia simu mara kadhaa hajapokea, tumemtumia meseji anasoma lakini hajibu chochote hivyo hiyo ni dharau na hatuendelei kudili na mtu mmoja wasanii ni wengi ambao wanahitaji msaada kutoka kwetu" alisema Shonza.

Rais Shein aongeza Wizara, Apangua Baraza la Mawaziri

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi huku akiongeza wizara moja zaidi. Kwa mujibu wa taarifa Ikulu ya Zanzibar, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais huku shughli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale. Mabadiliko hayo yanaifanya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo: 1. OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI i. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Issa Haji Ussi Gavu 2. OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA i. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora –Haroun Ali S...

Breaking News: Mlipuko Watokea Mahakama Ya Kisutu

Image
Muonekano mahakama ya Kisutu baada ya kutokea mlipuko uliosababishwa na umeme. Mahakama ya Kisutu imekumbwa na hitilafu ya umeme leo baada ya mvua kunyesha na kusababisha mlipuko na sintofahamu mahakamani hapo. Hitilafu hiyo ya umeme inadaiwa kutokea kwenye moja ya vyumba katika mahakama hiyo.

CDF Mabeyo Awatahadharisha Watanzania

Image
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewahadharisha Watanzania na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo. Ameeleza kuwa hivi sasa vipo viashiria vinavyotishia usalama wa nchi, na kwamba hatua zinachukuliwa ili kudhibiti hali hiyo. Jenerali Mabeyo amewaomba Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli dhidi ya wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi za umma, kwa kuwataja hadharani watu wanaojihusisha na vitendo hivyo Mabeyo amesema vita dhidi ya wizi na ufisadi, iliyoanzishwa na Rais Magufuli, si ya mtu mmoja, bali kila Mtanzania anapaswa kushiriki, kwani mali zinazoibwa na baadhi ya Watanzania, zinapaswa kuwanufaisha watu wote.

Hii ndio Mikoa vinara wa vifo vinavyosababishwa na wivu wa mapenzi

Image
Mikoa ya Singida na Tabora imebainika kuwa vinara wa matukio ya mauaji baina ya wanandoa katika miaka ya 2016 na 2017, kwa kuwa na matukio 314 kutokana na wivu wa mapenzi na ugomvi wa kifamilia. Takwimu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kupitia Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa kwa gazeti la Habari Leo, zinaonesha kuwa, mwaka 2016 kulikuwa na mauaji 151 baina ya wanandoa. Mwaka 2017 mauaji hayo yaliongezeka na kufikia 163 ambayo ni nyongeza ya mauaji 12 sawa na asilimia 7.9. Zinasema Mkoa wa Singida ulikuwa na matukio 27 ukifuatiwa na Tabora uliokuwa na mauaji 26 baina ya wanandoa. Mikoa mingine iliyofuata kwa wingi wa matukio ya wanandoa kuua wenza wao na idadi kwenye mabano ni Geita (25), Mwanza (21), Kagera (20) Mbeya 19 na Shinyanga (18). Mwaka 2016 Mkoa wa Shinyanga uliongoza kwa wanawake saba kuua waume zao, ukifuatiwa na Tabora sita huku mikoa ya Singida na Iringa ikiwa ...

Matukio Mabaya, Yawaongoze Kufanya Maamuzi Magumu!

Image
N I vigumu sana kumuacha mtu umpendaye. Unapompenda mtu mara nyingi hufikirii kufanya maamuzi yoyote hasi. Akili yako kamwe haimuwazii mambo mabaya mwenzi wako. Matamanio ya moyo wako ni kuona mnazidi kupendana. Mnazidi kuweka upendo mbele katika kila jambo linalowatokea katika maisha yenu. Upendo unawafanya muwe kitu kimoja katika maamuzi. Upendo unawapa faraja katika maisha yenu. Upendo unawafanya mchukuliane kwa kila hali, mathalani masuala ya ugonjwa na matatizo mengine. Shida yako ni shida yake, ya kwake pia inakuwa yako. Upendo unapowazunguka wapendanao wanakuwa wanaishi katika ulimwengu wao. Mkiishi katika misingi ya upendo, ni nadra sana kuona ugomvi kwa wapendanao. Pamoja na hayo, kuna wakati huwa yanatokea matatizo mbalimbali katika uhusiano ambayo kimsingi wakati mwingine yanapoteza ladha ya uhusiano. Hii inaweza kujidhihirisha kipindi tu mnaanza uhusiano, wakati mwingine huwa inatokea mkiwa tayari kwenye kilele cha safari yenu. Mfano inawez...

Linah asema hufanya kusudi kuwapagawisha vidume awapo jukwaani

Image
Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga maarufu kama 'Ndege Mnana' amefunguka na kuweka wazi kuwa huwa anafanya makusudi kuvaa nguo za nusu utupu 'fupi' akiwa kwenye show ili aweze kuwapagawisha watoto wa kiume walioko katika tamasha ambalo anashiriki. Linah amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati. "Mashabiki zangu wengi ni watoto wa kiume hivyo wakiona vichuchu vimesimama wanapata raha sana, muda mwingine nawatega kwa mavazi kwenye 'show' ili waburudike hivyo siwezi kubadili mavazi yangu kwa sababu mimi ni msanii ila ikitokea natakiwa kwenda sehemu ya kuvaa mavazi marefu ntafanya sina jinsi", amesema Linah. Kwa upande mwingine, Ndege Mnana amesema wakati mwingine huwa anapata wakati mgumu kutokana na mavazi yake akiwa jukwaani kwani akimuuita ...

Linah Aanika Idadi ya Wanaume Aliyotembea Nao

Image
MWANADADA anayekimbiza kwenye muziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amefunguka na kutaja idadi ya wanaume ambao ametembea nao na kufaidi penzi lake tangu awe maarufu. “Kwa haraka haraka nishatoka kimapenzi na wanaume watano hivi toka hivi watu wamenifahamu kama Linah, sina idadi kubwa sana, japo siwezi kuwakumbuka wote wengine nimeshawasahau kabisa. Kuna watu wana idadi kubwa ya watu wametembea nao sema tu ni kwa sababu si wasanii, “ amesema Linah. Linah amesema hayo wakati akifanya mahojiano yake na EATV kwenye kipindi cha Kikaangoni na kuongeza kuwa idadi hiyo ya wanaume ni baada ya kupata jina, lakini aliyowahi kutoka nao kimapenzi kipindi cha nyuma kabla ya umaarufu hawakumbuki ila ni kati ya 10 au 15. Linah amesema anavutiwa kimahaba na wanaume wenye rangi ya ngozi nyeusi tofauti na wengine wanavyochagua watu wa kuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi. “Mimi napenda wanaume weusi, warefu si unajua mimi mfupi (shoti), sipendi wanaume weupe japo nishawa...

Treni ya abiria yapata ajali

Image
Treni ya kubeba abiria iliyokuwa safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora imepata ajali katika eneo la kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza kaskazini magharibi mwa Tanzania, taarifa zinasema. Watu watatu wamejeruhiwa Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela ameambia BBC kwamba watu watatu wamejeruhiwa. "Sababu ya ajali bado haijafahamika lakini, timu ya kutathmini ajali iko njiani kuelekea eneo la tukio," amesema. Ajali ilitokea majira ya saa saba na dakika hamsini mchana eneo la katikati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza. "Tathmini kamili ya ajali itatolewa pale ambapo mabehewa yatakuwa yameinuliwa." Bw Mapondela amesema eneo hilo si kwamba ni baya na halina historia ya kupata ajali yoyote ile, ndio maana ni vigumu kusema nini hasa kinaweza kuwa chanzo cha ajali.

TCRA yasitisha nyimbo zisizokuwa na maadili

Image
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA] imepokea Orodha ya nyimbo zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa [BASATA].

Kisutu: Yaliyojiri Kesi ya Tido Mahakamani Leo

Image
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando,  amesomewa maelezo ya awali ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Februari 28,2018 mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa. Tido  anayetetewa na wakili Ramadhani Maleta amekubali maelezo binafsi kwamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC mwaka 2006 hadi 2010,  alikuwa msimamizi wa shughuli za TBC japo si zote, pia amekubali kutoa maelezo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuwa alifikishwa mahakamani Januari 26, 2018. Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya,  moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni. Anadaiwa pia  Juni 16, 2008 akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), akiwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na kutangaza vipindi vya televisheni kati ya TBC na ...

Breaking News: Sugu, Masonga Wahukumiwa Jela kwa Kumkashifu JPM

Image
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, wamehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya  kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. Mahakama imetoa uamuzi huo leo Jumatatu, Feb. 26, 2018 na hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mhakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Maiko Mteite,  baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka. Pia mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha miezi mitano Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,  Emmanuel Masonga,  kwa kosa hilo. Washtakiwa hao wanatajwa kutenda kosa hilo Desemba 30, 2017 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya wakati wakiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara.

Shy-Rose Bhanji Akanusha Kupinga Utawala wa JPM

Image
ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Bhanji amekanusha taarifa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa anapinga utawala wa Rais Dkt. John  Magufuli. Taarifa hiyo ilionekana imeandikwa kwenye akaunti yake rasmi ya Instagram lakini  amesema ilikuwa imedukuliwa na watu wasiojulikana ambao wali-post ujumbe huo wenye nia ya kumchonganisha na Rais. “Account yangu ya Instagram ilikuwa hacked na watu wasiojulikana ambao walipost vitu ambavyo sihusiki navyo. Naomba radhi kwa Rais wangu JPM na wote waliokerwa na jambo hilo,” ameandika ShyRose.

TAUSI AFUNGUKA KUACHA ‘NIDO’ NJE

Image
KOMEDIANI mwenye jina kubwa Bongo, Tausi Mdegela amefungukia ishu ya kuacha matiti ‘nido’ zake nje kisha kutupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram alipokuwa akiogelea kwenye jakuzi kuwa, ni hali ya kawaida kwa maana hawezi kuogelea akiwa amevaa suti, bali lazima avae nguo za kuogelea. Akizungumza na Over Ze Weekend Tausi alisema kuwa, hakuona cha ajabu kama watu walivyochukulia, lakini ni jambo la kawaida kwani mtu hawezi kuogelea akiwa amevaa vitenge na ndivyo ilivyokuwa kwake na hakuna na maana nyingine.   “Nilivaa mavazi ya kuogelea, nisinge-weza kuvaa vitenge au suti nikaogelea maana watu wanachunguza sana,” alisema Tausi asiyeishiwa na vituko. Imelda Mtema, Ijumaa Wikienda.

ZAMARADI AWA MTANGAZAJI WA KWANZA KUINGIA WASAFI RADIO NA TV

Image
BREAKING NEWS : WASAFI TV wamefanikisha Kumchukua @zamaradimketema ….pichani wakiwa Zanzibar kwaajili ya usaili wa watangazaji wa kituo hichO    

ANGALIA PICHA ZARI THE BOSS LADY ALIVYOTIKISA VALENTINE PARTY JIJINI LONDONI

Image
Mrembo Zari The Bosslady wikiendi hii alikuwa mmoja wa wageni katika sherehe ya Valentine Party ambayo ilifanyika katika klabu ya usiku ya Rio Nightclub, iliyopo katika wilaya ya Wood Green, Kaskazini mwa mji wa London. Zari alitokelezea akiwa na gauni lake fupi na viatu virefu vyote vikiwa na rangi nyekundu. Zari alikuwa ameambatana na muandaji wa sherehe hiyo, Lady Naaa huku Naj akiwa miongoni mwa wageni wengine waliohudhuria sherehe hiyo. Katika sherehe hiyo Rayvanny na Barakah The Prince walitumbuiza.