Treni ya abiria yapata ajali

Treni ya kubeba abiria iliyokuwa safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora imepata ajali katika eneo la kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza kaskazini magharibi mwa Tanzania, taarifa zinasema.

Watu watatu wamejeruhiwa

Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka

Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela ameambia BBC kwamba watu watatu wamejeruhiwa.

"Sababu ya ajali bado haijafahamika lakini, timu ya kutathmini ajali iko njiani kuelekea eneo la tukio," amesema.

Ajali ilitokea majira ya saa saba na dakika hamsini mchana eneo la katikati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza.

"Tathmini kamili ya ajali itatolewa pale ambapo mabehewa yatakuwa yameinuliwa."

Bw Mapondela amesema eneo hilo si kwamba ni baya na halina historia ya kupata ajali yoyote ile, ndio maana ni vigumu kusema nini hasa kinaweza kuwa chanzo cha ajali.

Comments

Popular posts from this blog