Matukio Mabaya, Yawaongoze Kufanya Maamuzi Magumu!


NI vigumu sana kumuacha mtu umpendaye. Unapompenda mtu mara nyingi hufikirii kufanya maamuzi yoyote hasi. Akili yako kamwe haimuwazii mambo mabaya mwenzi wako.

Matamanio ya moyo wako ni kuona mnazidi kupendana. Mnazidi kuweka upendo mbele katika kila jambo linalowatokea katika maisha yenu. Upendo unawafanya muwe kitu kimoja katika maamuzi. Upendo unawapa faraja katika maisha yenu.

Upendo unawafanya mchukuliane kwa kila hali, mathalani masuala ya ugonjwa na matatizo mengine. Shida yako ni shida yake, ya kwake pia inakuwa yako. Upendo unapowazunguka wapendanao wanakuwa wanaishi katika ulimwengu wao.
Mkiishi katika misingi ya upendo, ni nadra sana kuona ugomvi kwa wapendanao. Pamoja na hayo, kuna wakati huwa yanatokea matatizo mbalimbali katika uhusiano ambayo kimsingi wakati mwingine yanapoteza ladha ya uhusiano.

Hii inaweza kujidhihirisha kipindi tu mnaanza uhusiano, wakati mwingine huwa inatokea mkiwa tayari kwenye kilele cha safari yenu. Mfano inaweza kutokea mkiwa katika hatua ya uchumba au inaweza kutokea mkiwa tayari kwenye ndoa.

Katika kushughulikia haya, kwa hatua hizi mbili muhimu kila moja ina namna yake ya kufanya maamuzi. Mnapokuwa katika uchumba, unashauriwa kuchuja uzito wa matukio husika na kama ukiona ni mazito na yanakukosesha furaha, ni bora kusitisha safari mapema.

Usikubali kuendelea na safari ambayo inaonesha ina changamoto nyingi kuliko suluhu. Maisha yana changa-moto nyingi hivyo ni vyema linapo-kuja suala la uhusiano liwe la faraja zaidi kuliko changamoto za maisha, uhusiano usigeuke kuwa kaa la moto.

Mtu anayeku-saliti waziwazi, unamueleza habadiliki, unamfumania kila uchwao. Au pengine ni mlevi kupindukia, unahangaika kumre-kebisha lakini wapi. Anawa-tongoza mpaka marafiki zako, anawafuata mpaka ndugu zako na kuwataka kimapenzi wa nini huyo?

Mvumilie kwa muda lakini ukiona majanga ni mengi zaidi kuliko furaha ya moyo, muache aende. Utampata mtu ambaye ana moyo na utu. Mwenye upendo wa dhati ambao unaweza kufunika mambo yote mabaya na mkaishi vizuri.

Mnapokuwa kwenye ndoa kidogo ni tofauti. Uvumilivu unahitajika katika kiwango cha mwisho kabisa. Kama mtu umeishi naye katika kipindi cha urafiki, uchumba na baadaye mkawa wanandoa ni dhahiri kwamba mmeshibana vya kutosha.

Mnapokutana na changamoto mbalimbali katika ndoa, uvumilivu ndio suala linalopaswa kupewa kipaumbele kwa asilimia zaidi ya mia. Changamoto kama ya usaliti, uongo na mambo mengine madogo madogo yanaweza kutokea na mkayabeba.

Matatizo yoyote yanayoweza kutokea, yanapaswa kupitia kwenye hatua mbalimbali za utatuzi. Mfano unaweza kukaa chini na mwenzako, mkafanya mazungumzo ya kirafiki na mkaondoa tofauti zenu. Mnaweza kuwaona wazee kama limewazidi au hata viongozi wa dini na mkafikia muafaka.
Pamoja na kupitia hatua zote hizo bado nisisitize kwamba historia ya matukio mabaya ndio inayopaswa kukuongoza katika kufanya maamuzi magumu yakiwemo ya kuachana. Kuna mahali unafika, kila mnalofanya hamuoni mlango wa kutokea.

Na bahati mbaya sana mnafikia kwenye eneo baya ambalo sasa ni rahisi hata kuuana. Imani imetoweka. Mke hamuamini mume, mume hamuamini mke. Historia ya matukio mabaya ndio imetawala kwenye uhusiano wenu. Mnaishi kwa miezi au hata miaka mkiwa maadui, ugomvi umeshindwa kupata suluhu.

Mke anafanya yake, mume naye anajiachia kivyake. Mnakutana nyumbani kwenu kama vile chumba cha kupumzikia tu. Kila mtu anapata ‘tiba’ ya mwili mahali kwingine. Mnaogopana kwa kila kitu, mnaishi kwa machale machale, hiyo sasa ndio ninayosema iwaongoze kufanya maamuzi magumu.

Kama uzito wa ugomvi wenu umefikia kiasi cha kutoaminiana, mnahisi mnaweza kuuana wakati wowote hayo sasa si maisha tena. Ni bora mkafanya maamuzi magumu ya kuachana na kila mmoja akaitafuta amani ya moyo wak

Comments

Popular posts from this blog