Madaktari wasimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili.
Picha ya mtandao
Madaktari(baadhi) Hospitali ya Kenyatta wamesimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili.
Walibaini kosa hilo wakiwa tayari wamempasua mgonjwa huyo na kugundua hakuwa na tatizo la kuvilia damu walilotakiwa kulitibu
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare, amevieleza vyombo vya habari ya kuwa kulikuwa na wagonjwa wawili, mmoja ndiye aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwani alikuwa na damu iliyovimba ndani ya kichwa.
Tare ameeleza kuwa waliohusika na kwa sasa tayari wanafanyiwa uchunguzi kupitia sakata hilo ambao ni daktari wa upasuaji wa ubongo, muuguzi, na mtalaamu wa dawa za usingizi.
Hatahivyo ameomba radhi na kueleza kuwa mgonjwa halisi aliyekuwa anatakiwa kupasuliwa kichwa tayari ameshafanyiwa upasuaji huo na afya yake tayari imeanza kuimarika.
Comments
Post a Comment