
Shilole akiwasili mahamani hapo.
MSANII wa Bongo Fleva,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’
amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 14 na mahakama ya Mwanzo Wilaya
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya
utapeli kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye shoo.

…Akiwa na mumewe Uchebe.
Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu leo Machi 1, 2018, imethibitika
kuwa Shilole alilipwa kiasi cha Tsh. Milioni tatu kwa Mary Musa kwa
ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka mwaka jana 2017 katika
Ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam lakini
alishindwa kutokea kwenye shoo hiyo kama walivyokubaliana.

…Akiingia ndani ya chumba cha mahakama.
Kutokana na kitendo hicho, mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo
walipandwa hasira na kufanya fujo huku wakiharibu mali ukumbini hapo
hivyo kumsababishia mwandaaji ambaye ni Mary, hasara ya Tsh. Milioni 14
ambazo mahakama imeamua Shilole azilipe kama fidia kwa mlalamikaji.

Mlalamikaji Mary Mussa.
Baada ya tukio hilo, Mary alifungua kesi mahakamani hapo akiomba
kulipwa kiasi hicho cha fedha kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana
na Shilole kushindwa kufika lakini msanii huyo anadaiwa kupuuza wito wa
mahakama.

Shilole, Uchebe na wakili wao.
Akisoma hukumu hiyo, hakimu wa mahakama ya Mwanzo Kinondoni, A. P.
Mshingwa amesema Shilole amekuwa akitumiwa wito mara kwa mara na
mahakama afike kusikiliza kesi yake lakini amekuwa akikaidi kufanya
hivyo hadi mahakama ilipomuandikia wito mwingine kwenye
Gazeti la Uhuru lakini hakufika pia.
Shilole aliambatana mahakamani hapo na mumewe, Uchebe, na wakili
wake ambaye baada ya kufuatwa kwa mahojiano na Global TV, alikataa
kutaja jina lake wala kuzungumza chochote kuhusu kesi hiyo.

Wakiwa na wakili.
Mahakama imemuamuru azilipe pesa hizo haraka ndani ya wiki moja vinginevyo mali zake zitaanza kukamatwa.
KUTOKA GAZETI LA UHURU
PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS
Comments
Post a Comment