Mkurugenzi wa NEC amfungukia Mh.Mbowe
Baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe kulalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutokutenda haki katika uchaguzi mdogo uliokuwa ukifanyika mwezi uliopita, Mkurugenzi wa Tume hiyo, Kailima Ramadhani ameibuka na kusema kuwa hawezi kujibu matusi ya kiongozi huyo.
Siku chache zilizopita, Mbowe katika mkutano wake na wanahabari alilalamikia Tume hiyo kutotenda haki huku akisema kuwa Chama cha Mapinduzi(CCM) kilipendelewa.
Hata hivyo Mbowe alieleza kuwa wizi uliokuwa unafanywa katika uchaguzi huo ulikuwa ni wa kitoto sana huku akielez kuwa walituma barua kwa Mkurugenzi wa NEC hakujibu na alipopigiwa simu hakujibu.
Baada ya Mbowe kutoa malalamiko hayo, Kailima ameibuka na kujibu madai hayo kuwa “Nimesikitishwa sana na kiongozi wa ngazi za juu kutamka matusi hadharani. Mimi nimeenda jandoni siwezi kujibu matusi hayo.”
Hata hivyo Kailima ameeleza kuwa NEC inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu, maadili na miongozo ya uchaguzi wakati wote hivyo wanapomjibu mtu huwa wanazingatia maeneo hayo.
Comments
Post a Comment