Mama Diamond Ajitoa Kwa Zari, Mobeto
DAR ES SALAAM: Mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim (pichani) amejitoa kwenye gogoro linaloendelea kati ya ‘wakweze’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na Hamisa Mobeto. Kabla ya kauli ya mama Diamond juu ya warembo hao mapema wiki hii, wikiendi iliyopita kuliibuka ubuyu kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram kuwa, ugomvi kati ya Zari na Mobeto ulikuwa umeibuka upya baada ya kupoa kwa siku kadhaa. Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko ulibaini kwamba, ugomvi baina ya wawili hao ulirejea upya baada ya Mobeto kukutana na Diamond kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii na kukubaliana juu ya malezi ya mtoto wao, Abdulatif Nasibu ‘Prince Dully’. Ilisemekana kwamba, kuna maneno aliyoweka Zari kwenye Mtandao wa Snapchat yakiashiria kutokuwepo kwa maelewano kati yake na Diamond kufuatia tukio hilo lililoonekana kumweka jamaa huyo karibu na Mobeto. Kama hiyo haitoshi, kuna ubuyu kuwa