'Maafisa Habari, TEHAMA ni Mawakala wa Mabadiliko’


Ndugu Wakili Mtebe, Meneja Mradi wa PS3, akiwakaribisha wageni wakati wa Ufunguzi.
Mkuu wa Mawasiliano kutoka OR TAMISEMI, Bibi Rebecca Kwandu, akiteta jambo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa muda mfupi kabla ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Joseph Nyanda, amewakumbusha Maafisa Habari na Maafisa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, maarifa na ubunifu, kwakuwa wao ni mawakala wa mabadiliko.


Dkt. Peter Kilima, Mkurugenzi wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi kutoka PS3, akizungumza wakati wa Mafunzo hayo
Akifungua kikao cha siku nne mkoani humo kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Ndugu Nyanda amewatahadharisha maafisa hao kuwa endapo watazembea kutekeleza wajibu wao wa msingi kwa weledi, watu wengine watapotosha umma.
“Kila mmoja miongoni mwenu anayo dhamana ya kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali, lakini mkikaa kimya ninyi kama sauti za taasisi zenu, watu wasio wema watapotosha maudhui hayo na mwisho wa siku kuchafua taswira ya Serikali” amesisitiza Nyanda.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi Rebbeca Kwandu, amewasisitizia maafisa hao kubadilika katika utendaji wao mara baada ya mafunzo ya mfumo huo juu ya uendeshaji wa tovuti.
Athuman Pemba Mmoja ya Watoa mada, akiwa anaendelea na Utoaji mada mara baada ya Ufunguzi.

“Mwanzoni tulipoanzisha tovuti hizi, hatukuwa na mwongozo ambao ni dira ya uendeshaji.  Hata hivyo mara baada ya OR-TAMISEMI kuandaa mwongozo huu kwa kushirikiana na wadau wetu PS3, ni imani yangu tutabadilika,” alisema Bi. Kwandu, na kuongeza kwamba uwepo wa tovuti bila ya uwepo wa habari haina maana.
Akizungumza kwa niaba ya Mradi wa PS3, Mkuu wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi, Dkt. Peter Kilima, amekiri kwamba Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA ndio roho ya taasisi, hivyo ushirikishwaji hasa kwenye vikao vya maamuzi itakuwa ni fursa kwao kuchuja na kuujuza umma mambo mazuri ya nchi.
Awali akitoa Salaam za Idara ya Habari (Maelezo), Mkurugenzi Msaidizi wa Habari na Picha, Rodney Thadeus, aliesema kwamba ili kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali, ni lazima Maafisa Habari wawe na zana za utendaji kazi, na zana zenyewe katika mustakabali wa sasa kwa ngazi za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ni tovuti.
“Wafadhali PS3 wametuwezesha kuwa na mfumo wa Government Website Framework (GWF).  Tumieni hizi tovuti kama tools (zana) za kuujuza umma.
Mafunzo haya ya siku nne ni ya awamu ya kwanza kwa Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA kutoka mikoa ya Mara na Arusha, na mafunzo kama haya yatafanywa pia kwa maafisa kutoka mikoa mingine yote iliyobaki ya Tanzania bara.



Baadhi ya Washiriki wa mafunzo wakifatilia kwa Makini Hotuba ya Ufunguzi. Mafunzo ya mwongozo wa tovuti za Serikali yameandaliwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa PS3 ambao unafadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani (USAID).  Takribani Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA 418 kutoka Ofisi za Mikoa na Halmashauri Tanzania bara wanatarajiwa kupatiwa mafunzo hayo.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo anayeshughulikia Habari na Picha Rodney Thadeus  akitoa Salama za Idara wakati wa Semina hiyo.
 

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo anayeshughulikia Habari na Picha Rodney Thadeus  akitoa Salama za Idara wakati wa Semina hiyo.
   Bibi Rebecca Kwandu, Mkuu wa Mawasiliano Serikalini kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, akitoa Malengo ya Mafunzo hayo kwa Mikoa ya Mara na Arusha.
Chanzo:Atley Kuni- OR TAMISEMI

Comments

Popular posts from this blog