KISA MNYETI, HECHE ASUBURI KAULI YA JPM

MBUNGE wa Tarime Vijijini, John Heche amedai litakuwa jambo la ajabu kwa Watanzania kunyamazia ubaguzi unaofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ikiwa walikuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi.

Heche ametoa kauli hiyo mchana wa leo ikiwa ni muda mfupi baada ya taarifa za Mkuu huyo wa Mkoa kusambaa akiweka wazi wilayani Mbulu  kwamba hayuko tayari kutoa msaada kwa diwani wa chama cha upinzani kwa kuwa yeye anatekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani.

Kama Watanzania walikua mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi itakua jambo la ajabu kunyamazia ubaguzi na chuki ya Mnyeti dhidi ya Watanzania wengine, nasubiri kusikia kauli ya Chama chake na rais aliemteua Mnyeti.” alisema Heche.

Comments

Popular posts from this blog