Posts

Chama cha Wafanyakazi chapingana na Makonda

Image
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu) kimelaani kitendo kikichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kuwavua madaraka hadharani watumishi wa umma wakisema ni kitendo cha kinyama. Akizungumza leo Februari 13, 2018 wakati akitoa tamko la chama hicho, Katibu Mkuu, Rashid Mtima amesema chama hicho hakitetei watumishi waovu, bali taratibu zinatakiwa kufuatwa katika kuwawajibisha Februari 10, 2018  watumishi wa idara za ardhi wa manipaa za Ubungo na Ilala walivuliwa madaraka hadharani hali iliyosababisha mmoja wao, Paul Mbembela (Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Ilala) kuzimia kwa muda. "Tunalaani, tunalaani, tunalaani sana kitendo kilichofanywa na Makonda. Sheria zinataka mtumishi anayekiuka kanuni na sheria za utumishi kushughulikiwa kwa siri hadi uamuzi wa mwisho utakapotolewa,” amesema. " Jambo baya zaidi tunalolaani hata mtumishi huyo alipozimia Makonda aliendelea kusema Dar es Salaam oyee, huu ni unyama.” Amesema kibin

Diwani Mwingine Chadema Atimkia CCM

Image
DIWANI wa Kata ya Hayderer (Chadema) wilayani Mbulu mkoani Manyara, Justin Masuja amejiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Februari 12,2018 katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti. Katika mkutano wa hadhara, Mnyeti aliwaomba madiwani wa upinzani kuhamia chama tawala ili watekeleze Ilani ya CCM ambayo ndiyo ipo madarakani. Masuja alieleza kwamba amejiunga na CCM ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

Mwanamke abambwa na cocaine kwenye makalio

Image
Polisi nchini Ureno wamemkamata mwanamume mmoja kwenye uwanja wa ndege huko Lisbon, ambaye alikuwa amebeba kilo moja ya cocaine kwenye makalio bandia. Vyombo vya habari nchini humo vilisema kuwa raia huyo wa Brazil aliwasili kwa ndege kutoka mji wa Belém do Pará, kaskazini mwa Brazil. Haijulikani ni vipi polisi walifanikiwa kugundia hilo. Mwanamume mwingine ambaye anashukiwa kuwa angepokea dawa hizo alikamatwa kwenye kituo cha treni cha mji huo. Wanaume hao watakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya. Mwezi uliopita polisi nchini Ureno na Uhispania walikamata cocaine ndani ya mananasi yaliyokuwa yamessfirishwa kutoka Amerika ya Kusini.

KAULI YA KWANZA DIAMOND PLATINUMZ NA HAMISA BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI

Image
February 13, 2018 stori inayoshika headlines ni ya Kimahakama ambapo Nyota wa muziki wa Bongo fleva na President wa WCB, Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wamerudi tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuweka rekodi baada ya usuluhishi wao kuhusu matunzo ya mtoto wao. “Hivyo tutaangalia jinsi ya kumtunza mtoto wetu ikiwezekana tunategemea baadaye anaweza kuwa kiongozi fulani . Nawashauri wababa kwamba wazazi wakike na kiume wajitahidi kuweka majivuno pembeni bila kumuathiri mtoto. Hivyo lazima kuweka majivuno pembeni kwani mwisho wa siku anayeathirika ni mtoto.” Diamond Platnumz <span data-mce-type="bookmark" style="display: inline-block; width: 0px; overflow: hidden; line-height: 0;" class="mce_SELRES_start"></span>

RAMAPHOSA AONGOZA JAHAZI KUMUNG’OA ZUMA MADARAKANI, AMPA SAA 48

Image
Rais Jacob Zuma. RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu, wadhfa wake huo huku Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa akiongoza shinikizo hilo la kumng’oa kiongozi huyo mkongwe barani Afrika.Kwa mujibu shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, hatua hii inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala cha nchini humo ANC. Taarifa zinaeleza kuwa, ANC kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani japo mpaka sasa haijulikani kwamba Rais Zuma alipokeaje ujumbe huo. Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama hicho kumng’oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuchukua muda mrefu na wenye madhara zaidi kwa Chama cha ANC. Rais Zuma ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa, alishindwa

ANGALIA BINTI WA MIAKA 11 AJIFUNGUA SIKU YA HARUSI YAKE,NI MAJANGAZI

Image
Binti wa miaka 11 wa nchini Bulgaria ambaye alijifungua mtoto wa kike siku ya harusi yake huku akiwa amevaa shela lake la harusi amesema hataki tena kuendelea na shule na anataka atumie muda mwingi kucheza na mtoto wake. Kordeza Zhelyazkova mwenye umri wa miaka 11 wa nchini Bulgaria alijifungua salama wiki iliyopita mtoto wa kike mwenye uzito wa kilo 2.4 ambaye alimpa jina la Violeta lakini alitoroka hospitali na mtoto wake usiku huo huo aliojifungua mtoto wake ili awahi kumalizia sherehe za harusi yake. Kordeza ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi, alisema kuwa alikutana na mumewe mpya mwenye umri wa miaka 19 Jeliazko Dimitrov kwenye viwanja vya michezo vya shule yake baada ya Jeliazko kumuokoa kutoka kwenye kipigo cha wahuni wa mitaani. Kordeza anadai alianza kufanya mapenzi na Jeliazko bila kutumia kondomu na anakiri alikuwa hajui kondomu ni kitu gani wakati huo. Kordeza alipata mimba ndani ya wiki moja baada ya kuanza kufanya mapenzi na mpenzi wa

Simba Hawaukosi Ubingwa

Image
KWA staili hii Simba inakosaje ubingwa wa Ligi Kuu Bara? Vigogo wa Simba wameibuka na kutangaza ofa mpya kwa wachezaji wa timu hiyo kwamba kila mechi watakayoshinda kila mchezaji atapata fedha ya maana. Simba hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kushinda michezo 12 ya ligi kuu kati 17, ikitoka sare michezo mitano huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, wachezaji hao wameongezewa morali ya kupata ushindi na kuwawekea motisha ya fedha kwa kila mechi watakayoshinda ya ligi kuu na michuano ya kimataifa Afrika. Simba hivi sasa inawategemea zaidi Emmanuel Okwi na John Bocco katika kupata ushindi. Mtoa taarifa huyo alisema, motisha hiyo ya fedha imegawanywa kwa mafungu, ipo inayowahusisha wachezaji wa kikosi cha kwanza, akiba na wanaokaa ambao wao wanapata sawa. “Kiukweli hivi sasa mabosi na viongozi wa Simba, wamedhamiria kuuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu, kwani wameandaa motisha kwa wachezaji kwa kila me

KISA MNYETI, HECHE ASUBURI KAULI YA JPM

Image
MBUNGE wa Tarime Vijijini, John Heche amedai litakuwa jambo la ajabu kwa Watanzania kunyamazia ubaguzi unaofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ikiwa walikuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi. Heche ametoa kauli hiyo mchana wa leo ikiwa ni muda mfupi baada ya taarifa za Mkuu huyo wa Mkoa kusambaa akiweka wazi wilayani Mbulu  kwamba hayuko tayari kutoa msaada kwa diwani wa chama cha upinzani kwa kuwa yeye anatekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani. “ Kama Watanzania walikua mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi itakua jambo la ajabu kunyamazia ubaguzi na chuki ya Mnyeti dhidi ya Watanzania wengine, nasubiri kusikia kauli ya Chama chake na rais aliemteua Mnyeti.” alisema Heche.

Haya ndio mambo matatu waliozungumza Zitto Kabwe na Mh.Lissu Ubelgiji

Image
Jana Jumapili Februari 11, 2018 Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe alimtembelea Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu ambaye yupo kwenye matibabu nchini Ubelgiji. Zitto Kabwe amesema kuwa walipokutana waligusia mambo makubwa matatu ambayo ni juu ya Gharama za matibabu yake, Suala la uchunguzi wa shambulio lake na maendeleo ya afya yake na mbinu za kuleta mabadiliko nchini. Kuhusu suala la matibabu Mhe. Zitto Kabwe amesema Lissu anasikitika kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka leo sio tu halimhudumii Lakini pia hata stahili zake za msingi kama Mbunge hapewi. Licha ya kutibiwa kwa misaada ya wasamaria wema, lakini ana mahitaji mengine kama mwanadam na wajibu kama mzazi. Sheria ya Bunge imeweka wazi kuwa Mbunge anapokuwa ametibiwa nje ya nchi Bunge humgharamia maisha yake. “Suala la Gharama za matibabu yake.,Lissu anasikitika kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka leo sio tu halimhudumii Lakini pia

Ajali Mbaya Yaua Sita Papo Hapo- Tanga

Image
WATU watano wamefariki dunia papo hapo na wengine sita kujeruhiwa vibaya, baada ya basi kubwa kugongana na Hiace katika eneo la Kabuku wilayani Handeni. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Leonce Rwegasira alisema ajali hiyo ilitoke saa 5:30 asubuhi katika eneo hilo la Kabuku. Alitaja magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi la Kampuni ya AJ Safari lililokuwa likitoka Lushoto kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Khalifa Mussa Omary mkazi wa Chamanzi Dar es Salaam lenye namba za usajili T 497 BJB mbalo limegongana na Hiace iliyokuwa ikitoka Mkata kwenda Segera yenye namba T591 AKE. Aliwataja waliokufa kuwa ni pamoja na dereva wa Hiace aliyefahamika kwa jina moja la Shabaan, wengine majina yao hayajatambulika na maiti zao zimehifadhiwa Kwenye Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe. ACP Rwegasira alisema majeruhi ambao hawakuchukuliwa majina yao kutokana na uharaka wa kuwasaidia kuwafikisha katika Kituo cha Afya Kabuku kwa

'Maafisa Habari, TEHAMA ni Mawakala wa Mabadiliko’

Image
February 12, 2018 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara,Raphael Joseph Nyanda akifungua Semina kwa Maafisa hao wa Mkoa wa Mara na Arusha. Ndugu Wakili Mtebe, Meneja Mradi wa PS3, akiwakaribisha wageni wakati wa Ufunguzi. Mkuu wa Mawasiliano kutoka OR TAMISEMI, Bibi Rebecca Kwandu, akiteta jambo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa muda mfupi kabla ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo. Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Joseph Nyanda, amewakumbusha Maafisa Habari na Maafisa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, maarifa na ubunifu, kwakuwa wao ni mawakala wa mabadiliko. Dkt. Peter Kilima, Mkurugenzi wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi kutoka PS3, akizungumza wakati wa Mafunzo hayo Akifungua kikao cha siku nne mkoani humo kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Ndugu Nyanda amewatahadharish

Rais Magufuli afanya uteuzi huu

Image
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) na Bw. Waziri Waziri Kindamba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amesema kuwa Uteuzi wa Dkt. Omari Rashid Nundu na Bw. Waziri Waziri Kindamba umeanza tarehe 01 Februari, 2018. Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Omari Rashid Nundu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya iliyokuwa Kampuni ya Simu Tanzania (Tanzania Telecommunication Company Limited – TTCL) na Bw. Waziri Waziri Kindamba alikuwa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo. Pamoja na kufanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwahamisha wafanyakazi wote na maafisa wa umma (Employees and Public Officers) wa iliyokuwa TTCL kwenda TTCL Corporation. Pia Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Ma

BREAKING : ANGALIA MTOTO WA KIUME AFUMANIWA NA BABA YAKE MZAZI CHUMBANI

Image
Kijana mmoja aliyetajwa kwa jina la Dullah, mkazi wa Chamwino, Kibao cha Shule mkoani Morogoro amedaiwa kufumaniwa akijaribu kumlawiti Baba ake mzazi. tukio hilo lakusikitisha lilitokea jumatatu iliyopota usiku nyumbani kwa mzee mmoja maarufu (jina linahifadhiwa kwasababu za kimaadili) anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70. Habari zinasema kijana huyo inadaiwa baada ya kutaka kufanya unyama huo, baba yake alipiga yowe kuomba msaada ambapo baadhi ya wananchi walimwita mwandishi wetu ambaye alipofika eneo la tukio alikuta kundi la wananchi wakijadili, huku mtuhumiwa akiwa amekimbia.

UTAPELI MPYA FEDHA KWENYE SIMU YAKO WATIKISA NCHINI!

Image
IGP Sirro. BADO wizi wa fedha za kwenye mitandao ya simu unaendelea kutikisa nchini ambapo kwa sasa njia mpya imeibuka ambayo unaibiwa fedha kwenye simu yako ukiwa nayo mkononi. Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko baadhi ya wananchi walilalamikia utapeli huo na kusema wameibiwa fedha zao ambazo zilikuwa kwenye simu zao. Mmoja wa wananchi hao, Agatha John wa Mwenge jijini Dar alisema aliibiwa fedha zake shilingi 60,000 baada ya kupigiwa simu na mtu ambaye hamfahamu aliyemtaja jina lake kiufasaha na kumdanganya kwamba yeye ni ofisa wa mtandao wa simu anaoweka fedha zake. “Mtu huyo aliniambia kuna zawadi kemkem zitatolewa na mtandao huo kwa wateja ambao wana fedha zaidi ya shilingi 50,000 hivyo alinishauri nimtajie namba yangu ya siri ili fedha na zawadi ziweze kutumwa ndani ya siku tatu,” alisema Agatha. Aliongeza kwamba baada ya kumtajia namba zake za siri aliamini kwamba fedha zake zitakuwa salama kwa sababu simu na kadi yake anayo yeye, hivyo alidhani

Nape Nnauye awakomalia usalama wa Taifa

Image
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameibuka na kuituhumu Idara ya Usalama wa Taifa nchini haifanyi kazi zake ipasavyo inavyohitajika na badala yake wamekalia kusikiliza simu za watu wanavyoongea pamoja na kufanya mambo ambayo hayalindi uchumi wa Tanzania. Nnape ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge mjini Dodoma na kuishauri kamati hiyo ipeleke mapendekezo ili waweze kupitia upya sheria ya Usalama wa Taifa na kuiwezesha mikono yao iende mbali, kukumbuka jukumu lao la la kuhakikisha wanalinda uchumi nchi katika kipindi hichi, ambacho demokrasia ya siasa inahama na kuelekea kwenye demokrasia ya uchumi ambapo muda mwingi wanapaswa kuutumia huko na sio pengine. Kutoka na hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni George Mkuchika amemjibu Nape na wabunge wengine kwamba kazi ya Idara ya Usal

Hoja ya biashara ya ngono, madanguro yajibiwa na Serikali

Image
Serikali imesema ina andaa mikakati itakayowezesha kudhibiti biashara ya ngono na uwepo madanguro nchini, hasa kwenye maeneo ya mijini. Hayo yamesemwa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe, Khalifa Mohammed Issa aliyehoji juu mpango serikali katika kudhibiti biashara ya ngono na madanguro ili kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini. Akijibu swali la Issa, Dkt. Ndugulile alisema Serikali inaandaa mikakati mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kuhusu madhara ya biashara ya ngono kwa jamii pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaojihusisha na baishara hiyo, pamoja na kudhibiti uwepo wa madanguro. Katika hatua nyingine, Dkt. Ndugulile alisema serikali inaendelea kuchukua hatua katika kudhibiti mila na desturi potofu zinazochangia maambukizi mapya ya VVU, ikiwemo ukeketaji na urithishaji wa wajane kwa ndugu w

Akiwa Safarini, Mbasha Akombwa Kila Kitu Mchana Kweupe

Image
 ALIYEKUWA mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiwa safarini Arusha amekombwa kila kitu na majambazi nyumbani kwake Tabata Kimanga mchana kweupe. Mtu wa karibu na Mbasha aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, Mbasha alichanganyikiwa baada ya kurudi na kukuta amekombwa kila kitu cha ndani na majambazi. Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la Mikito Nusunusu, lilimtafuta Mbasha ambaye alikiri kuibiwa kila kitu na kusema kuwa mpaka sasa amesharipoti polisi na uchunguzi bado unaendelea. “Yaani sina la kusema walioniliza wamefanya kazi kwani wamechukua kila kitu cha ndani na kwa kweli wamenirudisha nyuma sana hata sielewi naanzia wapi,” alisema Mbasha. Wakielezea tukio hilo majirani wa eneo hilo walisema kuwa mitaa hiyo mida ya mchana huwa ni tulivu sana kwani watu wengi huwa wanakwenda makazini ndio maana hata majambazi hao wakafanikiwa kuiba kila kitu bila kushtukiwa. “Si unajua nyumba zetu ni za mageti makubwa mtu kujua moja kwa moja kuwa kwa f’lan kaingia mt

Akiwa Safarini, Mbasha Akombwa Kila Kitu Mchana Kweupe

Image
 ALIYEKUWA mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiwa safarini Arusha amekombwa kila kitu na majambazi nyumbani kwake Tabata Kimanga mchana kweupe. Mtu wa karibu na Mbasha aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, Mbasha alichanganyikiwa baada ya kurudi na kukuta amekombwa kila kitu cha ndani na majambazi. Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la Mikito Nusunusu, lilimtafuta Mbasha ambaye alikiri kuibiwa kila kitu na kusema kuwa mpaka sasa amesharipoti polisi na uchunguzi bado unaendelea. “Yaani sina la kusema walioniliza wamefanya kazi kwani wamechukua kila kitu cha ndani na kwa kweli wamenirudisha nyuma sana hata sielewi naanzia wapi,” alisema Mbasha. Wakielezea tukio hilo majirani wa eneo hilo walisema kuwa mitaa hiyo mida ya mchana huwa ni tulivu sana kwani watu wengi huwa wanakwenda makazini ndio maana hata majambazi hao wakafanikiwa kuiba kila kitu bila kushtukiwa. “Si unajua nyumba zetu ni za mageti makubwa mtu kujua moja kwa moja kuwa kwa f’lan kaingia mt

Hatma ya Zitto mikononi mwa Spika

Image
KUADHIBIWA ama kutoadhibiwa na Bunge kwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) kuko chini ya Spika Job Ndugai baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kukamilisha uchunguzi wa shauri lake. Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo anakabiliwa na tuhuma za kudharau mamlaka ya Spika kutokana na kauli yake kwamba, "Bunge limewekwa mfukoni na serikali." Akiwasilisha bungeni mjini hapa jana taarifa ya shughuli za Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kipindi cha kuanzia Januari 2017 hadi Januari 2018, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Almas Maige, alisema tayari wameshakamilisha uchunguzi wa shauri hilo. Pia alisema kamati yake imeshamshauri Spika hatua za kuchukua kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016. Maige ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), alisema kuwa katika mkutano wa nane wa Bunge, baada ya Spika kupokea na kuikabidhi serikali taarifa za kamati mbili alizoziunda Julai tano kwa ajili ya kufan

Chanzo Cha Maumivu Ya Tumbo Mara Kwa Mara!

Image
Maumivu ya tumbo. MAUMIVU ya tumbo ni tatizo linaloweza kumpata mtu yeyote, mwanamke au mwanaume, mkubwa au mdogo. Maumivu haya husumbua kwani huwa hayaishi, yaani yanatulia kwa muda flani na kurudi tena, aina hii ya maumivu pia inaweza kuwa ya moja kwa moja, yaani hayatulii na wakati mwingine mgonjwa hupata nafuu kwa kujikunja au kushikilia tumbo. Maumivu yanaweza kuwa upande wa juu wa tumbo au upande wa chini na yanatulia kwa vipindi na kurudi yakiwa makali au madogo lakini hayaishi. JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA Kama tulivyoona, humtokea yeyote mwanamke au mwanaume, utokeaji wake hutofautiana kwa jinsi. Kwa mwanaume vyanzo vya maumivu haya vinaweza kuwa hernia au ngiri au matatizo kwenye korodani, lakini kwa wote vyanzo vinaweza kuwa vidonda vya tumbo, matatizo ya mkojo, kidole tumbo, matatizo ya utumbo mkubwa, kukosa au kufunga kupata haja kubwa, gesi kujaa tumboni. Yapo mengine kama kuwa na mawe kwenye mfumo wa mkojo au kifuko cha nyongo, matatizo ya ini na mengi