Simba Hawaukosi Ubingwa
KWA staili hii Simba inakosaje ubingwa wa Ligi Kuu Bara? Vigogo wa Simba wameibuka na kutangaza ofa mpya kwa wachezaji wa timu hiyo kwamba kila mechi watakayoshinda kila mchezaji atapata fedha ya maana. Simba hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kushinda michezo 12 ya ligi kuu kati 17, ikitoka sare michezo mitano huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, wachezaji hao wameongezewa morali ya kupata ushindi na kuwawekea motisha ya fedha kwa kila mechi watakayoshinda ya ligi kuu na michuano ya kimataifa Afrika. Simba hivi sasa inawategemea zaidi Emmanuel Okwi na John Bocco katika kupata ushindi. Mtoa taarifa huyo alisema, motisha hiyo ya fedha imegawanywa kwa mafungu, ipo inayowahusisha wachezaji wa kikosi cha kwanza, akiba na wanaokaa ambao wao wanapata sawa. “Kiukweli hivi sasa mabosi na viongozi wa Simba, wamedhamiria kuuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu, kwani wameandaa motisha kwa wachezaji kwa kil...