UTAPELI MPYA FEDHA KWENYE SIMU YAKO WATIKISA NCHINI!
IGP Sirro. BADO wizi wa fedha za kwenye mitandao ya simu unaendelea kutikisa nchini ambapo kwa sasa njia mpya imeibuka ambayo unaibiwa fedha kwenye simu yako ukiwa nayo mkononi. Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko baadhi ya wananchi walilalamikia utapeli huo na kusema wameibiwa fedha zao ambazo zilikuwa kwenye simu zao. Mmoja wa wananchi hao, Agatha John wa Mwenge jijini Dar alisema aliibiwa fedha zake shilingi 60,000 baada ya kupigiwa simu na mtu ambaye hamfahamu aliyemtaja jina lake kiufasaha na kumdanganya kwamba yeye ni ofisa wa mtandao wa simu anaoweka fedha zake. “Mtu huyo aliniambia kuna zawadi kemkem zitatolewa na mtandao huo kwa wateja ambao wana fedha zaidi ya shilingi 50,000 hivyo alinishauri nimtajie namba yangu ya siri ili fedha na zawadi ziweze kutumwa ndani ya siku tatu,” alisema Agatha. Aliongeza kwamba baada ya kumtajia namba zake za siri aliamini kwamba fedha zake zitakuwa salama kwa sababu simu na kadi yake anayo yeye, hivyo alidhani