Posts

Diamond, Mobeto wamaliza fofauti zoa

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond amesema mazungumzo katika kesi yake Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto kati yake na mwanamitindo Hamisa Mobeto,  imekwenda vizuri. “Niseme tu mambo yameenda vizuri na kama mnavyojua mambo ya mahakamani ikitokea ninahitajika nitakuja,” amesema. Diamond alifika mahakamani hapo leo Februari 8, 2018  kusikiliza kesi inayomkabili ya matunzo ya mtoto Prince Abdul iliyofunguliwa na Mobeto. Amesema yeye na Mobeto hawana shida yoyote, ila kuna watu waliokuwa wakizungumza maneno na kumchochea Mobeto. "Tunahitaji kuweka mambo sawa. Tunahitaji kuwa katika mstari kwa sababu vitu vidogo vinaharibu upande wa mama na upande wa baba kwa hiyo tulikuwa tunaweka mambo sawa ili kesho na keshokutwa yasilete sintofahamu baina yetu,” amesema na Diamonda na kuongeza: “Ikitokea kuna mtafaruku baina ya mtoto, kila mtu anakuwa na mawazo yake, kwa hiyo ni lazima kumjenga mtoto na kuhakikisha kuwa mtoto anajengwa na k

ANGALIA WEMA SEPETU ALIVYOFIKA MAHAKAMANI NA WAKILI WAKE,KESI YAKE MAPYA YAIBUKA

Image
Kesi ya mrembo Wema Sepetu ya kukutwa na msokoto wa bangi imesikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Inspekta wa Polisi, Wille ameieleza mahakama kuwa hakuwepo wakati Wema akichukiliwa sampuli ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa serikali. Shahidi huyo aliyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati alipoulizwa maswali na Wakili wa Wema, Alberto Msando. Katika ushahidi wake, Inspekta Wille, alidai hakuwahi kupeleka sampuli za mkojo za washtakiwa wenzake Wema ambao ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas kwenda kuchunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Inspekta Wille alidai kuwa February 8, 2017 alifika katika ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali saa 5 asubuhi na kumkabidhi Mchunguzi Elia Mulima kichupa cha plastiki ambacho ndani kilikuwa na mkojo wa Wema. Wakili Msando alimuuliza Inspekta Wille kama alikuwepo wakati sampuli ya mkojo uliokuwamo ndani ya kichupa cha plastiki unachukuliwa ambapo I alijibu kuwa hakuwapo. Msando alimuhoji

ANGALIA AJIFUNGUA MTOTO KWENYE KORIDO HOSPITALINI

Image
JESICA HOGAN, mama wa watoto sita mkazi wa Riley, Kansas, Marekani, amejifungua mtoto pekee wa kiume katika korido ya hospitali ambayo alikuwa anawahishwa kwenda kujifungua. Mtoto huyo aliyeleta furaha katika familia hiyo ambayo ilikuwa na mabinti mtupu, anaitwa Max, ambaye alizaliwa akiwa salama na mwenye afya njema. Mwanamke huyo aliyejifungulia katika Hospitali ya Via Christi, ya Manhattan, Kansas, alisema alikuwa hana uhakika wa tarehe ya kujifungua, hivyo hakujua ni lini uchungu ungelianza. Alikuwa nyumbani wakati chupa ilipovunjika kunako saa tisa usiku ambapo mumewe, Travis, alimkimbiza hospitali. Mara tu baada ya kuingia katika korido ya hospitali hiyo, Jesica alihisi mtoto alikuwa ameanza kutoka, hivyo akaanza kuvua suruali yake wakati kichwa cha mtoto kilianza kujitokeza. Walianza kusaidia na mumewe hapohapo kwenye korido ambapo alilala chini kabla ya manesi kuja na kumsaidia. “Nilikuwa sifahamu hasa siku halisi ya kujifungua, lakini siku hiyo nilijua im

ANGALIA FARASI AFANYWA MSIMAMIZI HARUSINI,NI VITUKO VYA AJABU

Image
Maharusi wapya walikuwa washitakiwe kufuatia makosa ya kumtembeza farasi bila ruhusa maalum, baada ya Bibi harusi kuamua kumuweka farasi huyo kama mmoja wa wasimamizi wake. Mwanadada Alex Wells, mwenye umri wa miaka 28, alifanya uamizi huo alipokuw akifanya mipango ya harusi yake huko Nottinghamshire, Uingereza ambapo hata mume wake aliafikiana naye. Farasi huyu aliyejulikana kwa jina la Toffee, mwenye umri wa miaka 17 inasemekana pia kwa namna moja au nyingine ndiye aliyeruhusu harusi hiyo kufanyika kwani ni rafiki wa karibu sana wa Bi Harusi. Mume wa Alex, Graham Sales alikiri kukubaliana na hali hiyo kwani hata kwenye maisha ya kawaida ni kama anashindana na farasi huyo ili kupata muda na mkewe. Farsi huyu alikuwa na wakati mzuri wakati wa harusi hiyo kwani aliweza kushiriki katika kupiga picha za pamoja na mambo mengine.    

Breaking News: Tambwe Hizza wa Chadema Afariki Dunia

Image
Kada wa Chadema,  Tambwe Hizza, enzi za uhai wake. KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  Tambwe Hizza, amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake akiwa amelala, msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene,  amethibitisha  na kuongeza kwamba mwili wake umepelekwa Hospitali ya Temeke Dar es Salaam asubuhi hii. Kwa mujibu wa Chadema, marehemu Hiza alikuwa kwenye moja ya vikao vya chama hicho hadi jana saa tano usiku wa kuamkia leo. …Akiwa katika moja ya mikutano ya Chadema. Marehemu Tambwe Hizza amefariki akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na  alikuwa pia mmoja wa waratibu wa kampeni za chama  hicho katika jimbo la Kinindoni Hizza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa CUF, baadae alihamia CCM na kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM na 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA.

Uwoya, Aunt Ezekiel Wamchokonoa Shonza

Image
Wolper. DAR ES SALAAM: KITENDO cha wasanii wa filamu, Aunt Ezekiel Grayson Gwantwa ‘mama Cookie’ na Irene Pancras Uwoya kutupia picha mtandaoni zikionesha wakiwa wanaogelea huku maeneo nyeti ya miili yao yakiwa wazi, kimetafsiriwa na wadau mbalimbali ni kama ‘kuishika sharubu’ serikali. Mwanzoni mwa wiki hii, picha za wasanii hao wakiwa ndani ya majakuzi sehemu tofauti na kwa nyakati tofauti zimeleta hisia tofauti kwa jamii huku wengine wakienda mbele kwa kusema kitendo hicho ni kukaidi agizo la Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kupitia naibu waziri wake, Juliana Daniel Shonza aliyepiga marufuku picha za utupu mitandaoni. Aunt Ezekiel. Baada ya kuvuja kwa picha hizo, waandishi wetu waliwatafuta wasanii hao kupitia simu zao za mkononi ili kusikia utetezi wao juu ya jambo hilo. “Picha hiyo niko lokesheni (eneo la kuigizia), sasa sioni kama kuna tatizo kuonesha mtandaoni picha ya namna hiyo,” alisema Irene Uwoya. Kwa upande wa Aunt Ezekiel

EWURA Watangaza Bei Mpya Ya Mafuta Kutumika Februari 7, 2018

Image
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo Februari 7, 2018 huku bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa zikipanda. Taarifa kwa umma iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany imesema bei za rejareja zimeongezeka kwa petroli ikiwa ni Sh59 sawa na asilimia 2.70, dizeli Sh46 (sawa na asilimia 2.30), na mafuta ya taa kwa Sh24 (sawa na asilimia 1.17). Amesema bei za jumla nazo zimeongezeka ambazo kwa petroli ni Sh58.57 sawa na asilimia 2.85, dizeli kwa Sh46.48 (sawa na asilimia 2.44) na mafuta ya taa kwa Sh23.75 (sawa na asilimia 1.24). Mchany amesema ongezeko hilo linatokana na bei kuongezeka katika soko la dunia. “Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia Bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Januari 3. Bei za mafuta ya taa hazijabadilika kwa sababu hakuna yaliyoingizwa nchini kupitia ba

Mwigulu Avamia Shamba la Bangi, Alichokifanya

Image
WAZIRI wa mambo ya ndani nchini,Mwigulu Nchemba leo ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari  sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha. Mwigulu akishirikiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, (RPC)Charles Mkumbo pamoja na vikosi vya askari wa jeshi la polisi mkoani hapo walilazimika kuacha magari yao njiani na kutembea umbali wa kilomita 5 milimani kufika katikati ya msitu huo ambapo wamiliki wa mashamba hayo walitokomea kusikojulikana. Akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa zoezi hilo Mwigulu amesema kwamba serikali itaendelea na oparesheni pande zote za nchi na haitasita kuwakamata wahusika wote na kutaifisha magari yatakayotumika kusafirisha bangi. Aidha Waziri Mwigulu amewaambia askari waliokuwa wakishiriki katika zoezi hilo, Mwigulu mbali na kuwapongeza kwa kazi wanayofanya lakini amewaambia kwamba pamoja na kufanikiwa kuteketeza madawa ya kulevya yanayo

Kopa, Msagasumu Kupamba Shindano la Nyonga

Image
WAMAMA wa uswazi na ushuwani leo Alhamisi wanata-rajiwa kuon-eshana matu-mizi ya nyonga kwenye shindano litakalo-fanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar. Akizungumza na gazeti hili, mratibu wa tamasha hilo, Maimartha Jesse alisema shindano hilo litasind-ikizwa na burudani kutoka kwa Mfalme wa Uswazi (Msaga-sumu), Malkia wa Mipasho (Khadija Kopa), Jack Simela na wengineo. Sambamba na wasanii hao Maimartha alisema pia kutakuwa na burudani ya ngoma za Kibao Kata na Baikoko kutoka Tanga. Maimartha alisema upande wa ushereheshaji atakuwa yeye mwenyewe akisaidiana na Sakina Liyoka ambao kama kawaida yao watamwaga ubuyu mwanzo mwisho. Katika burudani zote hizo kiingilio kitakuwa shilingi 5000 tu. RICHARD BUKOS

Madiwani watatu Chadema wahamia CCM

Image
 Chadema katika Halmashauri ya Tunduma, wilaya ya Momba mkoani Mbeya kimepata pigo baada ya madiwani wake watatu kuhamia CCM. Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Ayub Mlimba (Mwaka Kati), Simon Mbukwa (Kaloleni) na Amos Nzunda (Mpemba) na walitambulishwa jana mchana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Jumaa Irando. Wakizungumza na Mwananchi madiwani hao waliohamia CCM wamesema wamechukua uamuzi huo baada ya kuona Chadema kimepoteza mwelekeo Tunduma, huku viongozi wake wakitoa amri za kibabe wakitaka wanachama kutozungumza chochote. “Unajua baraza la madiwani Tunduma linaundwa na Chadema, sasa tunapewa maagizo ya nini cha kuzungumza na kusimamia hata kama hayaendani na mahitaji ya wananchi wetu kwa lengo tu la watu wachache ndani ya chama,” alisema Nzunda. Mlimba alisema sababu ya kuhamia CCM ni kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli huku Mbukwa akieleza sababu yake kuondoa Chadema kuwa ni mvutano na mtafaruku

JPM Azindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi

Image
RAIS Dkt. Magufuli leo  Februari6,  2018 amezindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi (Comprehensive Training Center – CTC) kilichopo Mapinga katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani na kusema amesikia kilio cha wananchi wa Mpinga. Kituo hicho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 67.87 na kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi ya kisasa yatakayowawezesha askari kukabiliana na vitisho vya kisasa vya kiusalama. Baada ya uzinduzi huo Rais Magufuli aliweza kupata nafasi ya kuongea na wananchi wa eneo hilo na kusema amesikia kilio chao. “Nimesikia kilio chenu nataka niwahakikishie kwamba daraja hili ni muhimu, si muhimu tu kwa ajili ya kituo hiki bali ni muhimu pia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wanaokaa maeneo haya ninauhakika daraja hili kama litatengenezwa litapunguza gharama za ukaaji huku lakini pia litaweza kutumika kama ‘altenative route’ ikitokea siku moja daraja likakatika Mpigi pale juu ambapo lili

Msukuma Amtolea Povu la Mwaka Waziri wa JPM

Image
MBUNGE na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amemshambulia kwa maneno Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina juu ya ‘operation’ anazozifanya za kionevu za kupambana na uvuvi haramu kwa kumwambia aache kufanya kazi kwa mihemuko. Msukuma ameeleza hayo katika mkutano wa 10 kikao cha sita cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati akichangia uwasilishaji wa kamati ya kudumu ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji baada ya kupita miezi kadhaa tokea Waziri Mpina kutoa kauli yake kuachia madaraka endapo tatizo la uvuvi haramu litaendelea kuwa sugu nchini jambo ambalo kwa sasa Msukuma anadai kiongozi huyo analifanya bila ya kufuata sheria zilizopo kwa kuzuia watu wasivue dagaa na kupelekea kuwapa athari wananchi wanyonge na kumuomba aundiwe tume ya uchunguzi yeye timu yake. “Toka nazaliwa sijawahi kuona sheria hizi zinazotumiwa na Waziri wa Mifugo Mpina, umri wangu huu nimeshuhudia awamu zote za Mawaziri. Nafikilia kwamba ndio tunaanza kutunga sheria au hii i

DR.SLAA: SIKUWAHI KUSEMA NIMEACHA SIASA.

Image
Katibu mkuu wa zamani chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na balozi mteuli awamu ya tano, Dr. Wilbroad Slaa amesema kuwa hakuwahi kusema ameacha siasa bali alisema ameacha siasa za vyama vingi. Kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na runinga ya Clouds Media Group (CMG), leo jumanne Februari 2018, Dr. Slaa amesikika akiyasema hayo na kuongezea kuwa kutokuwa na chama haimanishi ameacha siasa. “Skuwahi kusema nimecha siasa na kama kuna mtu alikuwepo kwenye mkutano wangu pale Serena Hotel nilisema naachana na siasa za vyama vingi, na sina chama lakini haimanishi nimeacha siasa” Dr. Slaa. Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, amesema kila mtu ana mapungufu yake kwa wagombea waliokuwepo ila Magufuli ana afadhali. Pia amesema Bunge ni maazimio na huleta maana pale mijadala inapopigiwa kura na kuongeza kuwa bungeni sio kuongea kwa ukali. Akijibu swali aliloulizwa kuhusu kukimbilia Canada amesema kuwa ni nchi ambayo ina rekodi nzuri ya haki za b

CUF yamtaka Diwani wao kuacha kuandamana na mgombea wa Chadema

Image
Dar es Salaam. Katibu wa CUF  Ally Mkandu amemtaka Diwani wa kata ya mzimuni Ally Kondo kuacha kuongozana na mgombea wa Chadema Salum Mwalimu. Amesema kwamba diwani huo asipoacha kuongozana na mgombea huyo chama kitamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutumia katiba kumvua uanachama. Amesema hayo leo Februari 5 wakati akimnadi mgombea Ubunge  wa Kinondoni Rajabu Salum. Mkurugenzi wa Habari na uenezi Abduli Kambaya amewaambia wakazi wa mzimuni  kwamba mwaka 2015  CUF ilipata  ushindi kwa kufanya kazi kubwa kwenye kata ya mzimuni. ‘’Leo anajitokeza mtu anawashawishi mumchague mgombea mwingine  inauma sana’’amesema  Kambaya Naye mgombea  Rajabu Salum amesema kwamba ‘’Mimi nilikuwa meneja kampeni wa mgombea wa huyu aliyehamia  CCM( Maulid Mtulia)  hivyo mimi nilikuwa mwalimu wake’’ Amesema mgombea huyo sasa ameanza kutumia sera za Cuf  kwenye majukwaa. ‘’CCM na Chadema wameahidi kunipa kura kwa kuwa wagombea wao hawakushiriki kwenye kura za mao

Makamu wa Rais aguswa na Cover ya wimbo wa Nandy na Aslay

Image
Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa na wasanii Nandy na Aslay. MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwakaribisha nyumbani kwake wasanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ na Faustina Charles maarufu kama Nandy kwa ajili ya mazungumzo mafupi na chakula cha jioni. Katika mazungumzo yake na wasanii hao, Bi Samia alieleza kuvutiwa sana na marudio ya kibao cha SUBALKHERI kilichorudiwa na wakali hao wa Bongo Fleva hivi karibuni na kuwapa wosia wa kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi na kujiepusha na makundi mabaya.

Esma aweka wazi mahaba yake kwa Wema Sepetu

Image
Esma Abdul ‘Esma Platnumz’ MWANADADA Esma Abdul ‘Esma Platnumz’ ameonesha mahaba yake kwa staa mkubwa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akidai kuwa, amekuwa shosti wake kwa muda mrefu na hivyo hawezi kujitenga naye. Akipiga stori na gazeti hili, Esma alisema Wema ametoka naye mbali kiasi kwamba leo hii hawezi kumuweka pembeni na kujiweka zaidi kwa wifi wake wa sasa,  Zarina Hassan ‘Zari’. “Jamani Wema hata kidogo siwezi kumuweka pembeni, hata kama aliachana na kaka yangu lakini kwangu bado ana umuhimu. Kama kila anayeachana na kaka basi niwe naye mbali, nikifa inabidi nikazikwe Uganda au Sauzi maana Bongo sitakuwa na rafiki,” alisema Esma

JOKATE: 2018 NI NDOA NA FAMILIA PIA

Image
Jokate Mwegelo MWANAMITINDO ambaye ni kada wa CCM, Jokate Mwegelo baada ya kuanika kuwa mwaka huu ni sahihi kuingia kwenye maisha ya ndoa, ameibuka tena na kuanika kuwa 2018 ni mwaka wa kuwa na familia pia. Akiongea na Risasi Jumamosi Jokate alisisitiza kuwa mwaka huu ni wa neema kwake na kufafanua kuwa ana mpango wa kuanzisha familia yake. “Watu wajue tu kuwa mwaka huu nitaanzisha familia, sio kama ninawafumba lakini kwa uwezo wake Mungu wataona tu, wakae wakisubiri kwani lisemwalo lipo kama halipo linakuja,” alisema Jokate ambaye hakuweka wazi mwanaume atakayemuoa na kuanzisha naye familia

KISA BONGO FLEVA…AGNESS WA PICHA ZA UTUPU ASHAMBULIWA

Image
       Agness Mmasi MUUZA  nyago aliyejipatia umaarufu kwa kutupia picha za utupu mtandaoni, Agness Mmasi ameshambuliwa na mashabiki baada ya kujikita rasmi kwenye Muziki wa Bongo Fleva na kuachia Wimbo wa Danga unaoonekana  kukosa maadili. Akipiga stori na Mikito Nusu Nusu mara baada ya kuachia ngoma hiyo ambayo imejadiliwa sana kwa sababu ya maneno makali yaliyomo kwenye mashairi yake alisema, ngoma hiyo ameiimba kwa kuanika ukweli wa kile kinachoendelea kwenye jamii. “Nashangaa wanaonishambulia lakini ninachojua watu wengi   walikuwa hawaelewi nafanya kazi gani ya kunipa umaarufu, nikaona isiwe tabu bora nitimize ndoto yangu ya kuwa msanii wa muziki, sioni kama nimeimba maneno yasiyo na maadili ni vitu ambavyo vipo kwenye jamii, “alisema.

Figa Ya Sasha Yazua Utata

Image
Sasha Kassim. KALIO la muuza nyago wa video mbalimbali za wanamuziki Bongo, Sasha Kassim limezua utata kwa kudaiwa kuwa si halisi. Chanzo kimepenyeza ubuyu kuwa, Sasha amekuwa ‘akijiedit’ kupitia simu yake hivyo watu kumuona ana kalio kubwa tofauti na uhalisia. Sasha akionyesha figa yake bomba. “Wewe kutana naye hivi laivu halafu utaniambia,” alisema mtoa ubuyu. Alipoulizwa Sasha kuhusiana na hilo alisema; “Siwezi kuwazuia watu kuongea sifoji kitu mimi, siri kubwa ya shepu yangu ni mapozi kwenye picha na aina ya mavazi ninayovaa.”

RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya w