DR.SLAA: SIKUWAHI KUSEMA NIMEACHA SIASA.

Katibu mkuu wa zamani chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na balozi mteuli awamu ya tano, Dr. Wilbroad Slaa amesema kuwa hakuwahi kusema ameacha siasa bali alisema ameacha siasa za vyama vingi.
Kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na runinga ya Clouds Media Group (CMG), leo jumanne Februari 2018, Dr. Slaa amesikika akiyasema hayo na kuongezea kuwa kutokuwa na chama haimanishi ameacha siasa.
“Skuwahi kusema nimecha siasa na kama kuna mtu alikuwepo kwenye mkutano wangu pale Serena Hotel nilisema naachana na siasa za vyama vingi, na sina chama lakini haimanishi nimeacha siasa” Dr. Slaa.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, amesema kila mtu ana mapungufu yake kwa wagombea waliokuwepo ila Magufuli ana afadhali.
Pia amesema Bunge ni maazimio na huleta maana pale mijadala inapopigiwa kura na kuongeza kuwa bungeni sio kuongea kwa ukali.
Akijibu swali aliloulizwa kuhusu kukimbilia Canada amesema kuwa ni nchi ambayo ina rekodi nzuri ya haki za binadamu pia ni nchi yenye usalama mkubwa.
Hali kadhalika ameongelea nafasi aliyoteuliwa na Rais John Magufuli ya ubalozi kuhusu wanaouliza mbona hajaapishwa, amesema kuwa Uteuzi si kitu kipya wapo wengne waliteuliwa nyuma yake na bado hawajaapishwa.
Vilevile ameongeza kuwa wajibu wa viongozi wa dini ni kuleta maadili kwa sababu Siasa ni maisha.

Comments

Popular posts from this blog