CUF yamtaka Diwani wao kuacha kuandamana na mgombea wa Chadema

Dar es Salaam. Katibu wa CUF  Ally Mkandu amemtaka Diwani wa kata ya mzimuni Ally Kondo kuacha kuongozana na mgombea wa Chadema Salum Mwalimu.

Amesema kwamba diwani huo asipoacha kuongozana na mgombea huyo chama kitamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutumia katiba kumvua uanachama.

Amesema hayo leo Februari 5 wakati akimnadi mgombea Ubunge  wa Kinondoni Rajabu Salum.

Mkurugenzi wa Habari na uenezi Abduli Kambaya amewaambia wakazi wa mzimuni  kwamba mwaka 2015  CUF ilipata  ushindi kwa kufanya kazi kubwa kwenye kata ya mzimuni.

‘’Leo anajitokeza mtu anawashawishi mumchague mgombea mwingine  inauma sana’’amesema  Kambaya

Naye mgombea  Rajabu Salum amesema kwamba ‘’Mimi nilikuwa meneja kampeni wa mgombea wa huyu aliyehamia  CCM( Maulid Mtulia)  hivyo mimi nilikuwa mwalimu wake’’

Amesema mgombea huyo sasa ameanza kutumia sera za Cuf  kwenye majukwaa.

‘’CCM na Chadema wameahidi kunipa kura kwa kuwa wagombea wao hawakushiriki kwenye kura za maoni ‘’amesema Salum

Mwananchi:

Comments

Popular posts from this blog