Posts

RUBY ASALIMU AMRI KWA CLOUDS,HATIMAYE AOMBA RADHI

Image
Msanii wa muziki Bongo, Ruby amemaliza tofauti baina yake na Clouds Media Group. Muimbaji huyo ametumia kipindi cha XXL kuwaomba radhi wale wote aliowakwaza katika chombo hicho cha habari. “Yeyote, awe ni mwanakamati wa Clouds, team Clouds au awe ni shabiki wa nje I like to apologize guy to say sorry to my country, sorry to this management Clouds, I love them so much all I need is support mimi naamini kwamba ukiwa mjinga kwenye kila kitu utapata kujua vitu vingi sana,” amesema Ruby. “Nilikaa nikamuomba Boss wangu Ruge samahani, mimi ni mdogo wewe ni mkubwa, of course kwa chochote kile mimi ndio nakosea,” amesema. Clouds Media Group walikuwa wamesitisha kucheza nyimbo za msanii huyo kutokana na tofauti zao, hivyo sasa nyimbo zake zinachezwa na inaelezwa tangu November mwaka jana ilitolewa ruhusu kwa ngoma zake kuchezwa.

Lowassa, Mbowe Kuzindua Kampeni za Ubunge Jimbo la Kinondoni

Image
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kesho Januari 27, 2018 watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo inasema kuwa viongozi hao watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni kumtambulisha Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Salum Mwalimu. Uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika viwanja vya Mapilau kuanzia saa nane mchana mpaka saaa kumi na mbili jioni ambapo wageni rasmi watakuwepo Lowassa pamoja na Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA. Tarehe 17 Februari mwaka huu unatarajiwa kufanyika uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Siha na Kinondoni kutokana na wabunge wa majimbo hayo kujiuzulu nafasi zao za Ubunge wakiwa katika vyama vya upinzani na kuingia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa wanagombea nafasi hizo wakiwa chini ya CCM.

Lulu Diva Jeuri Hii Kaipata Wapi?…Anaishi Kwenye Mjengo wa Kifahari

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’. WAKATI wasanii wengine wakilia njaa kali sambamba na kuwa na maisha ya kawaida, hali ni tofauti kwa msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ambapo kwa sasa maisha yake yameonekana kumnyookea baada ya kunaswa akiishi kwenye mjengo wa kifahari pande za Mbezi Beach jijini Dar. Akisonga ugali. Gazeti hili kwa mara ya kwanza limefanikiwa kuunasa mjengo huo wa kifahari ndani ukiwa na vivutio mbalimbali. KAUNTA ZA VINYWAJI Ndani ya mjengo huo una kaunta mbili maalum kwa vinywaji laini ambapo ya kwanza ipo sebuleni na ya pili ipo jikoni huku pia kukiwa na friji kubwa la kisasa la milango miwili lenye thamani ya mamilioni. …Akifungua Friji lenye mapochopocho. SEBULE YA KISASA Ukiachana na sofa na fanicha za kisasa, upande wa sebuleni umepambwa kwa ‘wallpaper’ za aina yake sambamba na nakshinakshi kwenye meza maalum iliokaa mfano wa ‘dressing table.’ ENEO KUBWA LA PARKING Upande wa nje kuna eneo kubwa la pa

MOTO WAUA WATU 39 NA KUJERUHI 100 HOSPITALINI

Image
A person injured in a fire is carried from a hospital in Miryang, South Korea, Friday, Jan. 26, 2018. The hospital fire causes scores of casualties and injuries, according to a fire agency official. (Kim Dong-mi/Yonhap via AP) WATU 39 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika ajali ya moto uliyotokea katika Hospitali ya Sejong, Kusini Mashariki mwa Korea Kusini usiku wa kuamkia leo. Firefighters try to put out a fire at a hospital in Miryang, South Korea, Friday, Jan. 26, 2018. (Kim Dong-mi/Yonhap via AP) Taarifa za awali zimeeleza kuwa moto huo ulianzia kwenye chumba cha dharura cha hospitali hiyo ambapo maofisa wa usalama wameeleza kwamba huenda idadi ya waliokufa ikaongezeka kutokana na hali mbaya za baadhi ya majeruhi hao. Firefighters try to put out a fire at a hospital in Miryang, South Korea, Friday, Jan. 26, 2018. (National Fire Agency/Yonhap via AP) Zaidi ya majeruhi 100 wanasemakana wamo katika jengo la hospitali hiyo. Picha za mitandao

BREAKING : NABII TITO AJIJERUHI KWA KUJIKATA NA WEMBE TUMBONI

Image
Nabii Tito ameibua mengine baada ya kujijeruhi kwa kujikata na wembe tumboni ambapo kumepelekea ashonwe nyuzi 25 katika zahanati ya polisi Dodoma. Daktari wa hospitali hiyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameeleza kuwa Tito alifikishwa hospitali saa 9 mchana akiwa anavuja damu eneo la tumbo. Ni kweli Tito alifikishwa hapa majira ya saa 9 mchana, tulimfanyia matibabu kwa kumshona nyuzi 25 kutokana na ukubwa wa majeraha hayo” amesema Daktari. Hata hivyo kamanda wa polisi Dodoma, Gilles Muroto hana taarifa kutokea kwa tukio hilo. Nabii Tito sasa anashikiliwa na polisi kutokana na kauli zake zinazopingana na dini, amekuwa akihamasisha watu kunywa pombe, na wanaume kulala na wadada wa kazi akidai kuwa kufanya hivyo sio dhambi. Hivyo baada ya matibabu hayo nabii Tito alirudishwa polisi kwa mahojianao zaidi.

Penny: Sijaolewa, Nafasi Ipo Wazi!

Image
MTANGAZAJI wa kipindi cha Harusini kinachorushwa kupitia Magic Swahili, Pennieli Mungwila ‘Penny’ amefungukia vazi la harusi alilovaa na kuwaacha watu kwenye sintofahamu kuwa hajaolewa na kwamba nafasi bado iko wazi. Akizungumza na Star Mix, Penny alisema kuwa, gauni alilovaa ni kwa ajili tu ya kurekodi kipindi chake na sio kwamba ilikuwa ni harusi yake ya ukweli kama watu wengi walivyodhani. “Jamani nisije kukosa mume bure, gauni lile nilivaa kwa ajili ya kazi tu na si kwamba nilikuwa naolewa kweli kama watu walivyodhani,” alisema Penny.

Chuchu afunguka zawadi anayotaka kwa Ray

Image
BAADA ya kumzalia mtoto wa kiume na kuwa gumzo mitandaoni, muigizaji mkongwe wa filamu Bongo, Chuchu Hans amefungukia zawadi aitakayo kutoka kwa mzazi mwenziye ambaye naye ni msanii, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuwa ni busu tu. Akizungumza na Star Mix, Chuchu alisema kuwa baada ya kumzalia Ray hahitaji kupewa zawadi kubwa kwani hata busu litamtosha. “Unajua mimi nachojua zawadi ni zawadi tu hata kama Ray akiamua kunipa busu kwangu mimi linatosha kabisa wala asiwaze sana zawadi ya kunipa,” alisema Chuchu.

Kigwangala atoa siku saba kwa Kampuni za Uwindaji Nchini

Image
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala, ametoa siku saba kwa kampuni sita za uwindaji nchini kufika katika ofisi za wizara hiyo Dodoma, kujieleza kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya ujangili. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Dk. Kigwangala alisema kampuni hizo zina leseni halali za uwindaji, lakini ndani yake wamekuwa wakifanya vitendo ambavyo vinaashiria uvunjifu wa sheria na uhalifu dhidi ya wanyama. Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Berlette Safari Corporation Ltd,  Game Frontiers of Tanzania Ltd, Mkwawa Hunting Safaris Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris Ltd, Wengert Windrose Safari Ltd na Geenniles Safaris Ltd. Alisema wakurugenzi wa kampuni hizo na washirika wao wanatakiwa kufika ofisi za Wizara Dodoma kuhojiwa na kikosi kazi maalum kuhusiana na tuhuma hizo. “Waje hapa wazungumze na kikosi hiki wajieleze ni kwa nini tusichukue hatua za kisheria dhidi yao, lakini pia wajibu hoja mbalimbali zitakazohusisha makosa

Wema Aingia Matatani Kisa Mashoga

Image
Mrembo wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu. Mrembo wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amejikuta akiingia matatani kwa kudaiwa ‘kuwafuga’ wanaume wanaodaiwa ‘si riziki’ (mashoga) nyumbani kwake, Salasala. Kwa mujibu wa chanzo makini, mrembo huyo amekuwa akiishi na wanaume hao tata kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwakera majirani wanaomzunguka na kuwafanya wamshitaki serikalini. “Unajua hii tabia yake si ya leo, ameanza muda mrefu na amekuwa akiwakera majirani zake kwani wanahofia kuharibiwa watoto wao wa kiume kwa kufuata matendo yao,” kilidai chanzo. Kikizidi kushusha madai hayo chanzo hicho kilienda mbali zaidi kwa kusema mrembo huyo ni sikio la kufa kwani alikuwa akiishi na mashoga hao tangu alipokuwa anaishi maeneo ya Ununio jijini Dar hadi kumsababishia matatizo pia. “Kule Ununio alikuwa nao hawa mashoga, sijui ni marafiki zake au ni watu wa aina gani kwake. Watu wengi wanajiuliza kwanini anawakumbatia, wanakosa majibu. “Kama mnakumbuka vizuri hat

Walimu wapewa onyo Sumbawanga

Image
HALMASHAURI ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imewaonya walimu kutochangisha michango kwa wanafunzi na atakayebainika atachukuliwa hatua za kinidhamu kwani kufanya hivyo ni kukiuka agizo la serikali. Onyo hilo lilitolewa na Meya wa Manispaa hiyo, Justine Malisawa wakati akifunga baraza maalumu la madiwani lililoketi kwa ajili ya kupitisha bajeti ya Sh. bilioni 47.2 ya mwaka wa fedha 2018/2019, katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo. Alisema kuwa halmashauri hiyo kamwe haitakuwa tayari kumvumilia mwalimu yeyote ambaye atachangisha fedha wanafunzi kwa ajili yoyore, ikiwamo masomo ya ziada kwani serikali imekwisha piga marufuku suala hilo kupitia Rais John Magufuli. Malisawa alisema kuwa serikali imeshatangaza elimu bila malipo ni vizuri walimu katika halmashauri hiyo wakatekeleza nia hiyo ili kila mtoto aweze kupata elimu kwa usawa kwa kuwa baadhi ya wazazi hawana uwezo wa kugharamia elimu.

Breaking News: Tido Mhando Afikishwa Mahakamani

Image
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), Tido Mhando (kushoto), akiwa mahakamani na watuhumiwa wenzake. Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), Tido Mhando (kushoto), amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar leo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa TBC. Tido ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka ambapo moja ya mashtaka hayo ni uhujumu uchumi na kuisababishia TBC hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 887. Tido alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006). Kwa kipindi cha miaka mingi alikuwa akifanya kazi ya utangazaji wa radio ambapo alianza Utangazaji mwaka 1969 akiwa Radio Tanzania Dar es Salaam, (RTD), baadaye akafanya kazi Kenya, halafu Uingereza na hatimaye akarejea tena RTD kabla ya kuwa TBC. Kwa sasa Tido Muh

MAMA ALIA… NATESEKA ZAIDI YA WASTARA

Image
Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma. Hujafa hujaumbika! Wakati staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma akiendelea kuomba michango kwa Watanzania ili akatibiwe mguu nchini India, mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sidonia Ntabashigwa mkazi wa Salasala jijini Dar yupo hoi kitandani akisema, anaamini mateso anayopata ni makubwa mno kuliko hata ya msanii huyo. Mguu wa Bi. Sidonia Ntabashigwa uliokatwa. Akizungumza na Amani mama huyo alisema, anateseka kitandani kwa miaka miwili sasa na hawezi kutembea kwani mguu mmoja umevunjika na mwingine viungo vimehama sehemu yake. Mama huyo anaeleza kuwa, miaka miwili iliyopita akiwa katika stendi ya daladala Mbuyuni, Tegeta Dar, gari liliacha njia na kumgonga, ambapo alivunjika mguu ambao baadaye ulikatwa kwenye eneo la juu ya goti huku mguu mwingine ukiwa umegeuka yaani viungo vyake vikahama sehemu yake halisi. Mguu wa Wastara uliokatwa. “Sikuwa ni hili wala lile, nimejikalia kituoni nasubiri daladala n

Mwalimu atiwa mbaroni kwa kumuua mtoto wa miezi 7

Image
Mwalimu wa sekondari Stephen Wachira Wangara mwenye umri wa miaka 43, amefikishwa Mahakamani kwa kosa la kumuua mtoto wake wa miezi 7 kwa kumchinja na panga nchini Kenya. Mashahidi watano wa tukio hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Jimbo la Kirinyaga, Maina Muriuki wamemweleza Jaji Lucy Gitari wa Mahakama Kuu ya Kerugoya, jinsi mtuhumiwa alivyoua mtoto wake, Maina ameieleza Mahakama kuwa mwili wa mtoto huyo ulikuwa umewekwa ndani ya gunia ukiwa na damu, nje ya nyumba ya Wangara na pembeni ya mwili huo kuliwa na panga ambalo lilitumiwa kumuua mtoto huyo. Shahidi mwingine Joseph Muriithi amesema wakati wa tukio hilo alikuwa shambani kwa Wangara akifanya kibarua na alimwona mtuhumiwa akiwa na madoa ya damu na muda mfupi baadaye alisikia kelele kutoka kwenye nyumba ya mwalimu huyo. Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi March 1, 2018, ambapo itasikilizwa tena. Wangara ambaye ni mtuhumiwa ni baba mwenye watoto wawili na mwalimu katika shule

AMBAKA ASKARI MWENZAKE ‘AKIMRINGISHIA’ UUME MREFU

Image
  Luteni-Kanali Chris Davies anayeshitakiwa kumbaka askari mwanamke baada ya kupiga vileo na wenzake huko Canada. ASKARI wa Uingereza aliyewahi kuwa shujaa wa vita nchini Afghanistan, hivi majuzi alimbaka askari mwenzake wa kike baada ya kujigamba kwamba alikuwa na uume mrefu. Haya yalisema mahakamani ambapo Luteni-Kanali Chris Davies anashitakiwa kwa kumbaka askari ambaye ni mama wa watoto wawili na  umri wa miaka 53 katika tukio linalodaiwa kufanyika huko Kingston, Ontario,  Canada. Davies anasemekana kumwambia mwanamke huyo kwamba: “Nina uume wenye urefu wa inchi nane (sentimita 20.3) ambao unaweza kuubomoa ulimwengu wako.” Davies anadaiwa kumwambia mwanamke huyo kwamba: “Nina uume wenye urefu wa inchi nane (sentimita 20.3) ambao unaweza kuubomoa ulimwengu wako.”  Jina na utambulisho wa mwanamke huyo vimehifadhiwa. Mwanamme huyo anadaiwa alimfuata mwanamke huyo hadi hotelini kwake baada ya mwanamkehuyo ‘kubugia’ pombe mbalimbali za kutosha walipokuwa

MWANAMKE AMWAMBIA MUMEWE ANATAMANI WANAUME WENGINE

Image
ANITA CASSIDY (40) mwanamke ambaye amekuwa katika ndoa kwa miaka ipatayo kumi, alimwambia mumewe aitwaye Marc (46) kwamba anaona maisha na ndoa ya mume na mke yamemchosha na alitaka kuwa na wenza wengine wa kufanya nao mapenzi. Katika mazungumzo ya wawili hao ambao ni raia wa Italia, mumewe alikubali kwamba wote wawili kila mmoja angekuwa na wapenzi wengine.    Lakini, je, katika ndoa moja panawezekana kuwa na watu zaidi ya wawili? Anita Cassidy (katikati) akiwa na mpenzi wake wa kiume Andrea (kushoto) na mumewe Marc (kulia) wakichangia penzi la watu watatu. “Mwaka mmoja uliopita niliweka kila kitu bayana kwenye mtandao wa Facebook kwa picha niliyokuwa na mume wangu na watoto wetu wawili.  Marafiki zangu wakaanza kuniuliza kwamba mwanamme mwingine aliyekuwa katika picha alikuwa nani.  Niliwaambia alikuwa Andrea – mpenzi wangu wa kiume. … Watatu hao wakiwa pamoja kando ya bahari wakipunga upepo. “Nafahamu wengi watashangaa kwani walijua Marc ndiye mume w

Akukumiwa Kwa kumwingilia mwanaume kinyume cha maumbile

Image
Mahakama ya Mkoa wa Mwera imemuhukumu mshtakiwa Simai Khamis Salum mwenye umri wa miaka 30 mkaazi wa Uzini wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kutiwa hatiani kwakosa lakumuingilia mwanamme mwenziwe kinyume na maumbile. Imedaiwa Mahakamani hapo namuendesha mashtaka Rahima Kheir mbele ya hakimu Muhammed Ali Muhammed kwamba mnamo tarehe 2/3 /2015 huko Uzini bila ya ridhaa kwamakusudi amefanya kitendo hicho kwakijana mwenye umri wa miaka 20 jinalimehifadhiwa na kumsababishia maumivu makali huku akijua jambo hilo ni kosa kisheria. Akisoma hukumu Hakimu Muhammed amesema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mashtaka na kumuona nimkosa wakosa hilo ndipo Mahakama hiyo ilipomtia hatiani kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka saba pamoja na kumlipa fidia mtendewa yashilingi Milioni mbili ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hiyo.

Mawakili wa Sugu wajiondoa kwenye Kesi

Image
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya, Michael Mteite, amegoma kujitoa katika kusikiliza kesi inayowakabili Mbunge Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga. Mapema leo Alhamisi Januari 25,2018 Sugu na Masonga waliwasilisha ombi mahakamani wakimkataa hakimu huyo wakitaka ajitoe kusikiliza kesi kwa maelezo kuwa hawana imani naye. Hakimu Mteite amesema sababu zilizotolewa na akina Sugu hazipo kisheria na hazimfanyi kujitoa. Baada ya hakimu kukataa kujitoa, mawakili Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo wanaowawakilisha washtakiwa walitangaza kujitoa katika shauri hilo. Sugu, mwenzake wamkataa hakimu Sugu na Masonga wameiomba Mahakama kuwapatia wiki mbili za kutafuta mawakili wengine. Hakimu Mteite ameahirisha kesi hadi Februari 2,2018 na ameamuru washtakiwa kurejeshwa rumande.

Lowassa, Membe Uso kwa Uso Nyumbani kwa Gwajima

Image
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Bernard Membe walipokutana leo katika msiba wa mama mzazi wa Askofu Josephat Gwajima nyumbani kwake Salasala, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni  Mbunge wa Vunjo, James Mbatia;  Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema,  Bernard Membe  na Lowassa wakiwa kwenye msiba huo. WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa wamekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Bernard Membe leo katika msiba wa mama mzazi wa Askofu Josephat Gwajima nyumbani kwake Salasala jijini Dar es Salaam. Lowassa na Membe ni miongoni mwa viongozi waliochukua fomu kusaka ridhaa ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa 2015, ambapo jina la Lowassa lilienguliwa huku Membe akiingia hatua ya tano licha ya kushindwa katika hatua ya tatu bora.  Baada ya jina lake kuen

Mama wa Askofu Gwajima afariki Dunia

Image
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo Januari 21, 2018 amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi Ruth Basondole Gwajima ambaye amefariki asubuhi ya leo. Gwajima amesema kuwa mama yake mzazi amefariki akiwa na umri wa miaka 84 na kuwa mazishi ya mama yake mpendwa yatafanyika siku ya Alhamisi ya Januari 25, 2018 Salasala jijini Dar es Salaama. "Leo Saa mbili asubuhi mama yangu Mzazi, Bi Ruth Basondole Gwajima ametwaliwa na Bwana. Karudi Mbinguni akiwa na Umri wa Miaka 84. Kuna Furaha ya Ajabu Shujaa Wangu Amerudi kwao. Kwasababu katika maisha yake alimtumikia Mungu. Mazishi yatafanyika Alhamis Tarehe 25/01/2018; Salasala Dar es Salaam" alisema Gwajima. EATV.

Julitha Kabete Kukanyaga Miss World ni Mungu tu!

Image
Mrembo ambaye aliiwakilisha Tanzania katika mashindo ya Miss World 2017, Julitha Kabete. MREMBO ambaye aliiwakilisha Tanzania katika mashindo ya Miss World 2017, Julitha Kabete amesema kuwa mpaka kuweza kupata nafasi ya kwenda kuiwakilisha nchi yake sio kazi ndogo kama watu wanavyodhani kwani ameenda kuonesha ulimwengu kuwa hata taifa lake linaweza, haliko nyuma kitu ambacho kilimfanya asilale kwa ajili ya kuhakikisha anarudi na kitu ambacho kitaacha alama ya nchi yetu. Mrembo huyo amefanya mahojiano na Mikito Nusunusu na kuongea mengi kama ifuatavyo hapa chini: Mikito Nusunusu: Ni kitu gani kilikufanya uamue kwenda kushiriki Miss World nani alikusuma kufanya hivyo? <span style="display: inline-block; width: 0px; overflow: hidden; line-height: 0;" data-mce-type="bookmark" class="mce_SELRES_start"></span> Julitha: Miss World ilikuwa ndoto yangu tangu niko mdogo sana. Pia nilivyozidi kukua niliona kua plat