Walimu wapewa onyo Sumbawanga


HALMASHAURI ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imewaonya walimu kutochangisha michango kwa wanafunzi na atakayebainika atachukuliwa hatua za kinidhamu kwani kufanya hivyo ni kukiuka agizo la serikali.

Onyo hilo lilitolewa na Meya wa Manispaa hiyo, Justine Malisawa wakati akifunga baraza maalumu la madiwani lililoketi kwa ajili ya kupitisha bajeti ya Sh. bilioni 47.2 ya mwaka wa fedha 2018/2019, katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Alisema kuwa halmashauri hiyo kamwe haitakuwa tayari kumvumilia mwalimu yeyote ambaye atachangisha fedha wanafunzi kwa ajili yoyore, ikiwamo masomo ya ziada kwani serikali imekwisha piga marufuku suala hilo kupitia Rais John Magufuli.

Malisawa alisema kuwa serikali imeshatangaza elimu bila malipo ni vizuri walimu katika halmashauri hiyo wakatekeleza nia hiyo ili kila mtoto aweze kupata elimu kwa usawa kwa kuwa baadhi ya wazazi hawana uwezo wa kugharamia elimu.

Comments

Popular posts from this blog