Kigwangala atoa siku saba kwa Kampuni za Uwindaji Nchini
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala, ametoa siku saba kwa kampuni sita za uwindaji nchini kufika katika ofisi za wizara hiyo Dodoma, kujieleza kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya ujangili. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Dk. Kigwangala alisema kampuni hizo zina leseni halali za uwindaji, lakini ndani yake wamekuwa wakifanya vitendo ambavyo vinaashiria uvunjifu wa sheria na uhalifu dhidi ya wanyama. Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Berlette Safari Corporation Ltd, Game Frontiers of Tanzania Ltd, Mkwawa Hunting Safaris Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris Ltd, Wengert Windrose Safari Ltd na Geenniles Safaris Ltd. Alisema wakurugenzi wa kampuni hizo na washirika wao wanatakiwa kufika ofisi za Wizara Dodoma kuhojiwa na kikosi kazi maalum kuhusiana na tuhuma hizo. “Waje hapa wazungumze na kikosi hiki wajieleze ni kwa nini tusichukue hatua za kisheria dhidi yao, lakini pia wajibu hoja mbalimbali zitakazohusisha makosa