Waziri Mkuu atoa agizo kwa TAKUKURU


Waziri Mkuu .Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa ameaagiza TAKUKURU kumkamata Meneja wa TBA wilaya ya Butiama mkoani Mara kutokana na uzembe na kutumia fedha za Serikali kinyume na maelekezo.

Waziri Mkuu amefanya maamuzi hayo baada ya Serikali kupeleka fedha zaidi ya milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmashauri lakini mpaka sasa fedha ujenzi huo haujaanza na fedha hizo kutumika katika miradi mingine ambayo haijapangwa na Serikali.

"Tumeleta fedha milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmshauri lakini mmezipeleka kwenye shughuli nyingine, kwanini hajajenga jengo hili ikiwa fedha zimeshaletwa? Tumeleta fedha milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya, DAS na nyumba ya watumishi lakini mmejenga nyumba moja tu ya DC, nyumba zingine mbona hamjaanza kujenga?

Waziri Mkuu baada ya kukosa majibu yanayoridhisha kutoka kwa viongozi hao ndipo alipoagiza TAKUKURU kumchukua moja ya mtumishi wa halmshauri hiyo na kusema kuwa serikali haiwezi kuwavumilia watumishi na namna hiyo.

"Meneja TBA upo? Umepata fedha toka mwezi wa nne mwaka jana mpaka leo hii 21 Januari 2018 miezi mingapi ishapita? Msingi wa jengo upo? Kamanda wa PCCB hebu ondoka na huyu bwana, mchukue huyu hatuwezi kuchelewesha kazi, tumeleta fedha kujenga jengo la halmashauri watumishi wanahangaika wewe una hela mpaka leo unazo tu. Kwanini tuwe na watumishi wa namna hii? Alihoji Majaliwa.

Comments

Popular posts from this blog