Posts

Haji Manara; kitendo cha Klabu yangu kufungwa kwa penanti ni aibu ya mwaka

Image
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kitendo cha klabu yake ya Simba jana kufungwa kwa njia ya penati na kuondolewa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup ni aibu ya mwaka. Haji Manara alisema hayo jana baada ya waliokuwa mabingwa watetezi wa (Azam Sports Federation Cup) Simba kupigwa na Green Warriors na kuondolewa katika michuano hiyo kwa penati 4-3 "Shame!! Aibu!!!Fedheha!!! Haivumiliki!!!Tumewakera fans wetu zaidi ya twenty millions... nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba..Aibu ya mwaka" aliandika Haji Manara

Mwalimu atiwa mbaroni kwa kubaka wanafunzi wake

Image
Mwalimu mbaroni akidaiwa kubaka wanafunzi wake tisa MWALIMU wa Shule ya Msingi Itiryo, Samweli Bisendo (29),  amekamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa kubaka wanafunzi tisa wa shule yake iliyopo wilayani Tarime. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, alisema kuwa mwalimu huyo anadaiwa kutenda unyama huo kwa nyakati tofauti hadi alipobainika. "Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mwalimu wa shule ya msingi Itiryo, Samweli Mariba Bisendo (29) kwa tuhuma ya kubaka watoto wapatao tisa ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Itiryo,” alisema Kamanda Mwaibambe na kuongeza kuwa matukio hayo yalifanyika kati ya Novemba 30 na Desemba 6,mwaka huu. “Alikamatwa wakati akiwa anajiandaa kutorokea nchi jirani ya Kenya," alisema Mwaibambe. Aidha, Mwaibambe alipongeza ushirikiano kutoka kwa wananchi ambao ndiyo waliowezesha jitihada za polisi kuzaa matunda  katika  kumkamata mwalimu huy...

Nabii Amnunulia Binti Yake wa Miaka 4 Gari la Mil. 926

Image
Mtoto Israella Bushiri. NABII wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering, Shepherd Bushiri, amemfanyia sapraizi mwanayae wa kike, Israella Bushiri mwenye umri wa miaka 4, baada ya kumnunulia gari aina ya Maserati Levante lenye thamani ya Sh milioni 926, kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa. Gari alilonunuliwa na baba yake. Bushiri alitumia ukurasa wake wa Facebook ku-share picha na kuandika maneno ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya pekee aliyomjalia kumpata binti yake huyo. Gari lenyewe. Nabii huyo ambaye mara nyingi anafanya kazi zake za uinjilishaji nchini Afrika Kusini aliandika: “Ninaona baraka zako Mungu kwa zawadi hii ya pekee uliyonipa katika maisha yangu. Ninasherehekea kuzaliwa kwa Mungu wangu na mwokozi wangu Yesu Kristo, na kuzaliwa kwa binti yangu wa kwanza, Israella Bushiri. “Ninaona ni kama jana tu wakati mtoto huyu alipozaliwa na kumbeba mikononi mwangu, lakini leo naweza kumweka mabegani mwangu na akatulia mwenyewe pasipo kushikiliwa, nit...

Hamisa Mobetto: “Ungejiamini Wako angetulia”

Image
Kutokana na kile ambacho kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii kati ya Zari the bosslady  na Hamisa Mobetto ambao wanadaiwa kuwa wanarushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii kutokana na who wawili kuhost party usiku wa December 21,2017 Kampala Uganda na kusemekana kuwa Zari alijaza watu wengi kuliko Hamisa Mobetto. Hamisa Mobetto aonyesha kuendelea kurusha vijembe kwa Zari kupitia mtandao wake wa snapchat ambapo Hamisa ameandika “Tembo gani anang’olewa pembe kila siku” na Zari kumjibu “vikatuni kumi wanakusanya michango ya kusaidia watoto, vinyago kwenye mitandao ya kijamii,walioshindwa na maisha wakajikusanya kumshusha mtu mmoja,lakini mkashindwa#TheGeneral”

SIMBA KAMA MANCHESTER UNITED, WAVULIWA UBINGWA WA KOMBE LA FA

Image
Kikosi cha timu ya Simba SC. Siku mbili baada ya Manchester United ya England kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Ligi dhidi ya Bristol City inayoshiriki Ligi Daraja la Pili, mabingwa wa Kombe la FA nchini Tanzania, Simba nao wamevuliwa ubingwa wa michuano hiyo kwa kufungwa na Green Warious. Simba imevuliwa ubingwa huo usiku huu wa Ijumaa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulipo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa njia ya penati 4-3. Hatua hiyo ilifika baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida, ndipo mwamuzi Israel Nkono akaamuru zipigwe penati. Kipa wa Green, Shaban Dihile ndiye aliyekuwa shujaa kutokana na kuonekana kuwa imara langoni huku wachezaji wa Simba, Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein ‘Zimbwe JR na Jonas Mkude wakikosa penati na kuchangia timu hiyo ya Ligi Daraja la Pili kusonga mbele dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom. Waliopata penati za Simba ni Erasto Nyoni, Shiza Kichuya na John Bocco.

BREAKING NEWS : ASKARI MWINGINE WA JWT ALIYESHAMBULIWA DRC AFARIKI DUNIA

Image
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyekuwa katika Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati akipatiwa matibabu. Askari huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania waliojeruhiwa katika shambulio lililofanywa Desemba 7 mwaka huu na waasi wa The Allied Democratic Forces (ADF) katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania na watano wa DRC. Msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alitangaza taarifa hiyo ya kusikitisha katika Makao Makuu wa UN, Mjini New York jana Desemba 22, 2017 usiku. Katika taarifa iliyotolewa na MONUSCO leo, imeeleza kwamba mwanajeshi wa 15 wa Tanzania amefariki dunia akipatiwa matibabu mjini Kampala. Umoja wa Mataifa umetuma salamu za pole kwa wanajeshi, familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na serikali ya Tanzania kutokana ...

Mbaroni kwa Kukutwa na Magamba ya Kakakuona na Nyama ya Simba

Image
JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Ngerezya Chamukaga mkazi wa Kijiji cha Kanyara wilaya ya Sengerema kwa kukutwa na nyara mbalimbali za serikali, yakiwemo magamba 40 ya Kakakuona na vipande vitatu vya nyama ya Simba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi amesema Chamukaga alikamatwa Desemba 21 mwaka huu majira ya saa 1 usiku akiwa na nyara hizo za serikali. Katika tukio jinine, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mukadam Mukadamu ameongoza oparesheni ya ukaguzi wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi za jirani katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Nyegezi, ambapo mabasi matatu yanayosafirisha abiria kuelekea jijini Dar es Salaam yamezuiliwa baada ya kubaini kuwa hayajakidhi vigezo. Baadhi ya madereva wa mabasi yaliyofanyiwa ukaguzi wa leseni na kuwapima kilevi, wameupongeza utaratibu huo na kuomba uwe endelevu, huku abiria pamoja na wadau wengine wa usafiri wakisema ukaguzi h...

MWENYEKITI UVCCM APOKELEWA KWA KISHINDO DAR

Image
Mwenyekiti mpya Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),Kheri James akizungumza nawaandishi wa habari ukumbi wa Vijana Kinondoni, Dar es Salaam Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Kilakala (kushoto) akiteta jambo na Kheri James. Baadhi ya vijana wa UVCCM waliohudhuria katika hafla hiyo. MWENYEKITI mpya Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amepokelewa kwa kishindo na vijana wa UVCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akitokea mkoani Dodoma. Hafla hiyo imefanyika jana katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kheri alichaguliwa rasmi kuwa mwenyekiti Desemba 13 mwaka huu katika uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma na kuibuka mshindi kwa kupata kura 319. Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo, Kheri alisema ni wakati wa vijana wa jumuiya hiyo kuwa ngangari katika kupambana na rushwa inayoharibu taswira ya nchi kwani rushwa haijengi bali itawafanya vijana kuwa wasindikizaji tu kati...

Zitto Akutana na Kufanya Mazungumzo na Mbowe

Image
Zitto na Mbowe. Katika kikao chake cha juzi, ambacho kiliamua kugomea ushiriki wa uchaguzi wa marudio, Kamati Kuu ya ACT Wazalendo iliuagiza Uongozi wa Taifa wa Chama kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini na kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini kwetu, kwa kuanzisha mazungumzo na vyama vyote vya Upinzani nchini ili kuona njia bora zaidi ya mapambano ya pamoja ya kukabiliana na vitendo vya chama tawala cha kuvuruga chaguzi huru na za haki nchini. Wakati Katibu Mkuu wa chama chetu, ndugu Dorothy Semu, anaendelea na utaratibu rasmi wa kulitekeleza hilo, nilipewa wajibu wa kuanzisha mazungumzo ya Viongozi wa Juu wa vyama hivyo. Jana, nimezungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, ndugu James Mbatia aliye hospitalini KCMC baada ya ajali (namuomba Mola ampe afya njema), pamoja na kukutana na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, ndugu Freeman Mbowe. Nafurahi kwamba mazungumzo yetu yameanza vizuri. ...

Fanya Haya, Hisia Za Mapenzi Ziendelee!

Image
TUNAISHI kwenye ulimwengu unaoenda kasi sana kiasi kwamba usipokuwa makini, unaweza kujikuta ukimpoteza mtu uliyempenda sana maishani kwa sababu tu ya kujua namna ya kwenda naye sawa wakati ukiendelea na mchakamchaka wa kukimbizana na maisha! Inafahamika kwamba mapenzi ni hisia lakini ni wachache wanaoweza kueleza jinsi ya kufanya hisia za mapenzi ziendelee kuwa hai. Siku hizi ndoa nyingi zinaendelea kuwepo kwa sababu ya kudra tu, unakuta mume na mke wanaishi kwa sababu ya mazoea tu lakini si kwa sababu ya mapenzi! Wengine wanakwambia kabisa, ‘mapenzi yalikuwa wakati tunaanzana’! Wanaishi tu ilimradi siku zinaenda, ilimradi wanawalea watoto lakini si kwa sababu ya upendo kati yao. Wengine wanafikia hatua hata ya kulala mzungu wa nne au kutengana vyumba kabisa! Kwa nje mnawaona kama wanapendana lakini kumbe ndani kuna ufa mkubwa kati yao, hakuna tena mapenzi kati yao. Cha ajabu, utakuta watu hawahawa ambao leo wanaishi kimazoea, wakati wanaanzana walikuwa w...

Mo Rasmi Aanza Kumwaga Fedha Simba.

Image
Mohammed Dewji ‘Mo’ MFANYABIASHARA maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameanza rasmi kazi ya kuihudumia Klabu ya Simba. Mo ameanza kuihudumia klabu hiyo baada ya kupita kwenye mchakato wa kumtafuta muwekezaji wa Klabu ya Simba kwa ofa yake ya shilingi bilioni 20 na kupata hisa kwa asil­imia 50 huku 50 zikibaki kwa wanachama. Hata hivyo, bado kuna majadiliano na serikali ambayo inataka mwekezaji wa klabu asizidi asilimia 49. Wachezaji wa timu ya Simba. Awali, mfanyabiashara huyo alikuwa anaihudumia timu hiyo kama mwanachama kabla ya kukabidhiwa na wanachama klabu hiyo na kuwa mwekezaji. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka ndani ya timu hiyo, mfanyabiashara huyo ameanza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo mshahara, posho na mahitaji mengine. Mtoa taarifa huyo alisema, kambi ya maan­dalizi ya mechi ya hatua ya pili ya Kombe la FA dhidi ya Green Warriors aliwezesha yeye kwa kuiweka timu ya Escape Two Hotel, Mbezi Beach jijini Dar...

TUNDU LISSU: BADO NINA RISASI MOJA MWILINI

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema mwili wake bado una risasi moja licha ya kutolewa nyingine 15, huku akiweka bayana kuwa kitu anachokikosa zaidi ni kazi yake ya ubunge. Mwanasheria mkuu huyo wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari mara baada ya kufika nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, pia aligusia faraja aliyoipata baada ya kutembelewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi tangu Septemba 7 na ambaye huenda akahamishiwa nje ya bara la Afrika kwa matibabu zaidi, ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Azam, Baruan Muhuza. “Hali yangu ya afya inaendelea vizuri bado nipo hospitali maana yake bado ni mgonjwa lakini niwaeleze Watanzania na wananchi wote wanaofuatilia afya yangu kwamba naendelea vizuri sana,” alisema na kuongeza, “Hivi tunavyozungumza sina jeraha la risasi, risasi 16 zil...

TAZAMA PICHA ZA KWENYE USIKU WA WA ZARI ALL WHITE PARTY UGANDA.

Image
  Zari All White Party ni moja kati ya show zinazofanya vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na watu wanaohudhuria show hizo kuwa nadhifu zaidi. Usiku wa kuamkia Ijumaa hii moja ya show hizo ambazo huandaliwa na Zari The Bosslady, imefanyika katika ukumbi wa Guvnor nchini Uganda. Japo Zari alikutana na upinzani mkali kutoka kwa hasimu wake Hamisa Mobetto ambaye na yeye alikuwa na show yake kwa upande wa pili lakini hilo halikuweza kuzuia watu kumiminika katika party hiyo ambapo DJ wa Diamond, Romy Jones alihudhuria pia.

Kigwangalla Awakutanisha Wema na Jokate

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla jana Desemba 21, 2017 aliteua majina mengine ya Kamati ya Kitaifa ya kuandaa mwezi maalum wa maadhimisho ya Urithi wa Tanzania. Miongoni mwa wajumbe walioteuliwa ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jokate Mwegelo na Wema Sepetu ambao wataungana na wajumbe 23 aliowateua awali kuunda Kamati ya Kitaifa ya Kuandaa Mwezi Maalumu wa Maadhimisho ya Urithi wa Tanzania.  

FIFA YATANGAZA MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018

Image
FIFA limetangaza makundi ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwakani nchini Urusi. Makundi ya Kombe la Dunia 2018 Katika makundi hayo makundi yanayoonekana hatari zaidi ni Kundi C ambako kuna Ufaransa, Australia, Peru na Denmark na Kundi F linaloundwa na Ujerumani, Mexico, Sweden na Jamhuri ya watu Korea. Mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo utafanyika kati ya Mwenyeji, Urusi dhidi ya Saudi Arabia tarehe 24 juni 2018 kunako dimba la Luzhniki.

WEMA SEPETU ATANGAZA RASMI KURUDI CCM

Image
  Wema Sepetu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. MSANII maarufu wa Bongo Movie, Wema Sepetu leo Ijumaa, Desemba 1, 2017 ametangaza rasmi kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai kuwa ni kukosa amani ndani ya chama hicho. Wema ambaye ni alikuwa mshindi namba moja wa Taji la Miss Tanzania 2006, amesema Chadema ni kama nyumba inayomkosesha amani hivyo hana haja ya kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo.Amesisitiza kwake amani ni jambo kubwa sana hivyo anandoka ndani ya Chadema na kurejea nyumbani alikokulia kwa maana ya CCM. Wema na mama yake mzazi, Mariam Sepetu walihamia Chadema mwezi Februari mwaka huu baada ya kuhusishwa kwenye sakata la biashara ya madawa ya kulevya ambapo mpaka sasa kesi yake bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Vurugu Zatanda Kenyatta Akiapishwa, Polisi Wafunga Mtaa Kuzuia Mkutano wa NASA

Image
Polisi wakiimarisha ulinzi eneo hilo. MTAA wa Jacaranda jijini Nairobi, Kenya, leo umefungwa na polisi ili kuzuia mkutano wa umoja wa vyama vya upinzani nchini humo, National Super Alliance (NASA) uliopangwa kwa ajili ya kuwakumbuka wafuasi wake 27 waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa marudio uliofanyika zaidi ya wiki moja iliyopita. Mataili yakiwa yamechomwa moto. Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo ambapo Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa kwa kipindi cha pili katika uwanja wa michezo wa Kasarani. Chumba vya kutunzia maiti katika jiji hilo pia kimefungwa na polisi ambapo watu hawatakiwi kufika hapo. Hali ilivyokuwa eneo la tukio. Polisi waliokuwa na zana zote za kuzuia fujo wamekuwa wakirusha mabomu ya machozi sehemu nyingi yakiwemo maeneo ya wafuasi wa NASA ambao wamefunga barabara kadhaa jijini humo. Wafuasi wa NASA wakipambana na polisi. Mpinzani mkuu nchini humo, Raila Odinga, amepinga mipango ya kumwapisha katika nafasi ya urais, a...

DIAMOND PLATINUMZ AIBUA MAPYA,AWASHA MOTO UPYA,WEMA SEPETU,ZARI THE BOSS LADY NA HAMISA KUMEKUCHA KUPITIA WIMBO WAKE MPYA- "SIKOMI"

Image
Wakati msanii wa muziki wa Bongo Flava, Diamond Platnumz ameachia ngoma mbili kwa wakati moja ambazo ni Sikomi na Niache, ngoma ya kwanza imekuwa na nguvu na mapokeo makubwa kutokana na ujumbe uliyomo ndani yake.Katika ngoma hiyo ‘Sikomi’ Diamond amezungumzia maisha yake ya kimahusiano na wanawake maarufu kama Wema Sepetu, Penny na baby mama wake, Zari The Boss Lady.Wimbo huo wenye dakika 3:58 Diamond anaeleza baada ya kupambana kwa kipindi kirefu hadi kuja kutoka kimuziki aliamini pengine maisha yake ya kimahusiano yangekuwa vizuri kitu ambacho anakiri hakijamtokea tangu pale alipokutana na mrembo kutoka Bongo Movie. Licha ya kutomtaja mrembo huyo bila shaka anamzungumzia Wema Sepetu kwani ndiye mrembo pekee wa Bongo Movie aliyeanza kudate naye na couple yake kuwa na nguvu zaidi.Hata hivyo katika verse ya pili ya ngoma hiyo ndipo ameweka wazi kuwa anayemzungumzia ni Wema Sepetu kwa kueleza licha ya kumpenda sana lakini bado aliusumbua moyo wake. MOYO ALIUPATI...

Mmiliki wa shule ashitakiwa kwa mauaji

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi imewasomea shitaka la mauaji watu watatu wanaotuhumiwa kumuua kijana Humphrey Makundi aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo Moshi. Watuhumiwa hao ni mmiliki wa shule ya Scolastica, Edward Shayo mwenye miaka 63, mlinzi wa shule hiyo Hamis Chacha mwenye miaka 28 na Laban Nabiswa mwenye miaka 37. Upande wa Jamhuri katika shitaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi, Julieti Mawore umewakilishwa na Mwanasheria Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea, Faygrace Sadallah. Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka mbele ya mahakama hiyo, Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshitakiwa wa kwanza, Hamis Chacha wa pili Edward Shayo na wa tatu Laban Nabiswa, walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi. Aidha washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shitaka la mauaji huku akiwataka kusubiri kufany...

Biblia ya Jomo Kenyatta Yatumiwa Kumwapisha Uhuru Kenyatta

Image
Mzee Jomo Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kwanza wa Kenya mwaka 1964. KATIKA hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Kenya na Makamu wake, imeelezwa kuwa, nakala ya Biblia iliyotumiwa kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta ni ile iliyotumiwa kumwapisha kwa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta ambaye ni baba’ke rais wa sasa wakati nakala ya Katiba ni iliyotiwa saini wakati wa kurasmishwa kwa Katiba ya sasa mwaka 2010 uwanjani Uhuru Park. Biblia hiyo ilitumika mwaka 1964 kumwapisha Jomo Kenyatta, 2013 kumwapisha Uhuru kenyatta na leo Novemba 28, 2017 kumwapisha Uhuru Kenyatta katika Uwanja wa Kasarani. Uhuru Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kenya mwaka 2013. Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi amemwapisha Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Kenya kwa mhula wa miaka mingine mitano ijayo na William Ruto kuwa Makamu wake. Rais Kenyatta: “Nitatekeleza majukumu yangu, na wajibu wangu katika Ofisi ya rais wa Kenya, na kwamba nitatenda haki kwa wote kwa mujibu wa Katiba hii kama il...