SIMBA KAMA MANCHESTER UNITED, WAVULIWA UBINGWA WA KOMBE LA FA


Kikosi cha timu ya Simba SC.
Siku mbili baada ya Manchester United ya England kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Ligi dhidi ya Bristol City inayoshiriki Ligi Daraja la Pili, mabingwa wa Kombe la FA nchini Tanzania, Simba nao wamevuliwa ubingwa wa michuano hiyo kwa kufungwa na Green Warious.

Simba imevuliwa ubingwa huo usiku huu wa Ijumaa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulipo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa njia ya penati 4-3.

Hatua hiyo ilifika baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida, ndipo mwamuzi Israel Nkono akaamuru zipigwe penati.

Kipa wa Green, Shaban Dihile ndiye aliyekuwa shujaa kutokana na kuonekana kuwa imara langoni huku wachezaji wa Simba, Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein ‘Zimbwe JR na Jonas Mkude wakikosa penati na kuchangia timu hiyo ya Ligi Daraja la Pili kusonga mbele dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Waliopata penati za Simba ni Erasto Nyoni, Shiza Kichuya na John Bocco.

Comments

Popular posts from this blog