Nabii Amnunulia Binti Yake wa Miaka 4 Gari la Mil. 926
Mtoto Israella Bushiri.
NABII wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering, Shepherd Bushiri,
amemfanyia sapraizi mwanayae wa kike, Israella Bushiri mwenye umri wa
miaka 4, baada ya kumnunulia gari aina ya Maserati Levante lenye thamani
ya Sh milioni 926, kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.
Gari alilonunuliwa na baba yake.
Gari lenyewe.
“Ninaona ni kama jana tu wakati mtoto huyu alipozaliwa na kumbeba mikononi mwangu, lakini leo naweza kumweka mabegani mwangu na akatulia mwenyewe pasipo kushikiliwa, nitamsaidia kwa kila ninaloweza akue na kufikia malengo flani,” aliandika Bushiri.
Comments
Post a Comment