Mbaroni kwa Kukutwa na Magamba ya Kakakuona na Nyama ya Simba

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Ngerezya Chamukaga mkazi wa Kijiji cha Kanyara wilaya ya Sengerema kwa kukutwa na nyara mbalimbali za serikali, yakiwemo magamba 40 ya Kakakuona na vipande vitatu vya nyama ya Simba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi amesema Chamukaga alikamatwa Desemba 21 mwaka huu majira ya saa 1 usiku akiwa na nyara hizo za serikali.
Katika tukio jinine, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mukadam Mukadamu ameongoza oparesheni ya ukaguzi wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi za jirani katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Nyegezi, ambapo mabasi matatu yanayosafirisha abiria kuelekea jijini Dar es Salaam yamezuiliwa baada ya kubaini kuwa hayajakidhi vigezo.
Baadhi ya madereva wa mabasi yaliyofanyiwa ukaguzi wa leseni na kuwapima kilevi, wameupongeza utaratibu huo na kuomba uwe endelevu, huku abiria pamoja na wadau wengine wa usafiri wakisema ukaguzi huo wa kushtukiza unawafanya madereva wengi kuwa makini pindi wanapokuwa safarini na hivyo kupunguza ajali za mara kwa mara.

Comments

Popular posts from this blog