Biblia ya Jomo Kenyatta Yatumiwa Kumwapisha Uhuru Kenyatta

Mzee Jomo Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kwanza wa Kenya mwaka 1964.
KATIKA hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Kenya na Makamu wake, imeelezwa kuwa, nakala ya Biblia iliyotumiwa kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta ni ile iliyotumiwa kumwapisha kwa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta ambaye ni baba’ke rais wa sasa wakati nakala ya Katiba ni iliyotiwa saini wakati wa kurasmishwa kwa Katiba ya sasa mwaka 2010 uwanjani Uhuru Park.
Biblia hiyo ilitumika mwaka 1964 kumwapisha Jomo Kenyatta, 2013 kumwapisha Uhuru kenyatta na leo Novemba 28, 2017 kumwapisha Uhuru Kenyatta katika Uwanja wa Kasarani.
Uhuru Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kenya mwaka 2013.
Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi amemwapisha Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Kenya kwa mhula wa miaka mingine mitano ijayo na William Ruto kuwa Makamu wake.
Rais Kenyatta: “Nitatekeleza majukumu yangu, na wajibu wangu katika Ofisi ya rais wa Kenya, na kwamba nitatenda haki kwa wote kwa mujibu wa Katiba hii kama ilivyo kwenye sheria, na sheria za Kenya bila woga, mapendeleo au ubaguzi au nia mbaya. Ewe mwenyezi Mungu nisaidie.”
Uhuru Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kenya, leo Novemba 28,  2017.
Rais Kenyatta ala kiapo cha utiifu.
Rais Kenyatta: “Naapa kwamba nitakuwa mwaminifu, kikamilifu, kwa Jamhuri ya Kenya, kwamba nitatii, nitahifadhi, kulinda na kutetea Katiba ya Kenya kama ilivyo kwenye sheria, na sheria nyingine zote za Jamhuri. Na kwamba nitalinda mipaka na heshima ya watu wa Kenya. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.”
Baadaye, alitia saini viapo vyote viwili, kisha cheti cha kuapishwa, kuthibitisha kwamba sherehe ya leo imefanyika ambapo pia Jaji Mkuu David Maraga pia aliweka saini yake kwenye stakabadhi zote tatu (vipao viwili) na cheti cha kuapishwa kwa Rais ikifuatiwa na Jeshi la nchi hiyo kupiga Mizinga 21 ikiwa ni heshima kwa Rais mpya, Uhuru Kenyatta

Comments

Popular posts from this blog