BREAKING NEWS : ASKARI MWINGINE WA JWT ALIYESHAMBULIWA DRC AFARIKI DUNIA
ASKARI
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyekuwa katika
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati
akipatiwa matibabu.
Askari
huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania waliojeruhiwa katika
shambulio lililofanywa Desemba 7 mwaka huu na waasi wa The Allied
Democratic Forces (ADF) katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa
Mataifa (MONUSCO), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania na
watano wa DRC.
Msemaji
wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alitangaza taarifa
hiyo ya kusikitisha katika Makao Makuu wa UN, Mjini New York jana
Desemba 22, 2017 usiku.
Katika
taarifa iliyotolewa na MONUSCO leo, imeeleza kwamba mwanajeshi wa 15 wa
Tanzania amefariki dunia akipatiwa matibabu mjini Kampala.
Umoja
wa Mataifa umetuma salamu za pole kwa wanajeshi, familia, ndugu, jamaa
na marafiki pamoja na serikali ya Tanzania kutokana na msiba huo.
Comments
Post a Comment