Lazaro Nyalandu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amejiuzulu uanachama na vyeo vyote alivyokuwa navyo ndani ya chama hicho, pamoja na kuachia nafasi ya ubunge, kwa kile alichoeleza kwamba ni kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa ndani ya chama hicho.Akizungumza na waandishi wa habari leo, Nyalandu amesema ameamua kuachia nyadhifa zote ndani ya chama hicho, kuanzia leo, Oktoba 30, 2017 na kama itawapendeza viongozi wa Chadema, anaomba kujiunga na chama hicho. Hiki ndicho alichokiandika Nyalandu: NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara