Posts

MHASIBU UBALOZI WA TANZANIA MSUMBIJI APANDISHWA KORTINI KISUTU

Image
Mhasibu Joyce Moshi akishuka ngazi za mahakama baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili. MHASIBU wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi (56) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka tisa ikiwemo ya utakatishaji fedha wa dola za Marekani 150,000. Moshi ambaye ni Mkazi wa Temeke alifikishwa mahakamani hapo leo na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Wakili wa Serikali, Saimon Wankyo alidai kuwa Oktoba 25, 2016 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Maputo nchini Msumbiji, alighushi barua ikionesha kwamba Ubalozi wa Tanzania Nchini Msumbiji Umeielekeza Benki ya MIllenium kupeleka Dola za kimarekani elfu kumi  katika akaunti inayomilikiwa na Joyce Moshi akijua yakuwa siyo kweli. Inadaiwa barua hiyo ilionyesha kuwa ubalozi umeelekeza Benki ya ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha dola za Marekani 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na

ZARI THE BOSS LADY , BWANA’AKE WAWAFUNGA MIDOMO WABONGO!

Image
              Mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ambaye pia ni mzazi mwenza wa Mbongo Fleva, ambao hivi karibuni ilisemekana wamemwagana kutokana na mgogoro mzito uliosababishwa na Mbongo Fleva huyo kuchepuka na kuzaa na mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto, hatimaye leo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wamewaziba watu midomo, baada ya kutupia video wakiwa pamoja kisiwani Zanzibar. Video hiyo iliwapa joto mashabiki na wakajikuta wamepigwa na butwaa, kwani stori zilishaenea kuwa wawili hao wameshapigana kibuti na imebaki stori, lakini baada ya wawili hao kutupia video hiyo ikajibu maswali yote kuwa wapo pamoja tena kwenye dimbwi zito la mahaba. N

Dida: Sijawahi Kuhongwa Chochote Na Mwanaume

Image
Khadija Shaibu ‘Dida’. MTANGAZAJI wa redio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefunguka kuwa katika maisha yake hajawahi kuhongwa chochote na mwanaume, mafanikio yake utafutaji kwa sababu hapendi kupewa wala kujibweteka anapambana na ataendelea kupambana kwani anaamini mwanaume hawezi kumfanya awe na maendeleo. na kujikuta hawana thamani tena, jamani pambaneni mbona inawezekana wanawake kufanikiwa bila kuwatumia wanaume na miili yetu!” alisema Dida.

Nape Apigilia Msumari Kauli ya Msekwa Kuhusu Ukomo wa Madaraka kwa Rais

Image
Nape Nnauye. MBUNGE wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amepigilia msumari kauli iliyotolewa na Spika wa zamani wa Bunge, Pius Msekwa kuhusu miaka ya uongozi na kusema misimamo hiyo ndiyo misimamo ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwalimu Julius Nyerere. Nape Nnauye ameweka video ya Pius Msekwa akielezea juu ya ukomo wa kiongozi madarakani na kusema chama hicho kilishafikiria miaka ya nyuma kuongeza miaka kutoka 10 na kuendelea lakini waliona miaka kumi inatosha kwa mtu kuongoza na kusisitiza ikiwa miaka 15 ikatokea mkapata kiongozi mbaya miaka hiyo itakuwa ni mingi sana. “Miaka 15 mkipata kiongozi mbaya ni mingi sana, nashauri ibaki miaka 10 kama kiongozi ni mbaya angalau tumvumilie kwa miaka 10 tu halafu basi ndivyo hoja ya miaka 10 ilivyopita si kama hiyo mingine hatukufikiri ilifikiriwa ndiyo maana naposikia kuna Mbunge mmoja anataka kupendekeza twende kwenye miaka saba kwa vipindi viwili ninataka kumjulisha kwamba hili si wazo jipya tulishafikiri na lilik

Miili ya Wanajeshi wa JWTZ Waliouawa DRC Yaagwa

Image
Miili ya askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imeagwa tayari kwa kurejeshwa nchini. Askari hao walikuwa kwenye operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa (UN). Habari zilizopatikana zilisema miili ya askari hao iliagwa jana. JWTZ katika taarifa kwa umma juzi iliwataja askari hao kuwa ni Koplo Maselino Paschal Fubusi na Praiveti Venance Moses Chimboni. Taarifa ilisema askari wengine 12 walijeruhiwa katika shambulio lililofanywa na kundi la wapiganaji la ADF. Taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya JWTZ ilisema askari hao walishambuliwa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi Oktoba 9, wakiwa umbali wa kilomita 24 mashariki mwa mji wa Beni. JWTZ ilisema UN inaandaa utaratibu wa kuirejesha miili ya askari hao na utakapokamilisha wataujulisha umma mapokezi, kuaga na mazishi yatakavyokuwa. Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani mauaji hayo ya

Hatari ya kuvalia viatu bila soksi

Image
               Ukivalia viatu vyako bila soksi unajiweka katika hatari ya makubwa zaidi kuliko kunuka kwa miguu pekee.Chuo cha tiba ya miguu nchini Uingereza kinasema karibuni kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya maradhi yanayosababishwa na kuvu kutokana na kuvuma kwa mtindo wa kuvalia viatu bila soksi, hasa miongoni mwa vijana.Mtaalamu Emma Stephenson anasema amekuwa akipokea wanaume wa kati ya miaka 18-25 walio na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovalia soksi au kuvalia viatu visivyowatosha vyema.Kutovalia soksi siku hivi kumekuwa mtindo maarufu wa mavazi, na mwanamuziki Sam Smith ni miongoni mwa watu wanaojitokeza hadharani wakiwa na viatu bila soksi.                   Wanaume wengi katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila soksi.Mwanamuziki Tinie Tempah amejishindia tuzo nyingi kwa sababu ya mitindo na mara nyingi katika maonesho ya mitindo ya Londo huketi viti vya mbele.Yeye pia huwa mara nyingi hav

HAWA NDIO WANAOKULA MEME YA UTEANDAJI WA RAIS MAGUFULI

Image
         Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli watu wengi wamekuwa wakihoji ni nani hasa anayenufaika na huu utawala.. Malalamiko mengi yamekuwa yakitolewa na watetea mafisadi wa ufipa kwamba zama za Rais Magufuli kila mtu anaisoma namba wala hamna mwenye nafuu. Lakini uchunguzi niliofanya umenipa majibu tofauti kabisa. Watu wafuatao wanakula mema ya Rais Magufuli kwa sana tu na hawataki kabisa atoke madarakani. 1. Wamachinga Kabla ya Rais Magufuli kuwa machinga ilikuwa ni balaa tupu ,kila siku walichezea vipigo na kuchukuliwa bidhaa na mgambo. Leo ndani ya utawala wa Rais Magufuli wamachinga wanafanya biashara ndani ya jiji bila shida yoyote. Kwa nini wasimpende Magufuli? 2. Wakulima Chini ya utawala wa Rais Magufuli kodi zote za ajabu ajabu zimefutwa hivyo kuongeza tija kwa wakulima. Mazao ya chai ,korosho, Pamba, mpunga, tumbaku yalikuwa na kodi zaidi ya kumi!!! Sasa kwa nini wasimpende Rais Magufuli?? 3. Wafugaji Kabla ya Rais Magufuli ku

Nafasi za Kazi Standard Bank Tanzania

Image
Job Details Risk Management: understanding all risks – from the economic to the political – that could affect our global business, and offering guidance to all parts of the bank Job Purpose To asses information provided and consolidate in an Application for Facilities (AFF),  with focus on the need and structure of facilities, asses counter-party credit risks associated with the bank’s CIB lending and investment activities at the Business and client interface, with the primary objective to contain credit risk within acceptable parameters and in compliance with the Credit Policy and Product Parameters. Manager, Credit Originati Overview Job ID: 27802 Job Sector: Banking Closing Date: Oct 16 2017 Country: Tanzania Region/State/Province/District: Dar es Salaam Region Location: Dar es Salaam Key Responsibilities/Accountabilities Provision of direct (specialist/ professional) credit assessment services at the Business and  customer interface: Identifies cr

Nafasi za Kazi Mamlaka ya Reli Ya Tanzania na Zambia (TAZARA)

Image
The Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA) is a statutory institution owned by the two Governments of the United Republic of Tanzania and the Republic of Zambia on a 50/50 shareholding basis. Incorporated by the Acts of Parliament of the two contracting states, the Authority’s registered office is in Dar es Salaam, Tanzania, with two regional administrative centres in Mpika, Zambia and Dar es Salaam. Some positions have fallen vacant and, in this regard, applications are invited from suitably qualified applicants, as follows. Corporation Secretary-1 Position Reporting to: Managing Director Duty Station: Head Office Job Purpose To advise Management on legal matters and provide legal and administrative services to the Council of Ministers, Board of Directors and the Authority in general as well as safe guard Authority interests and asset utilisation. Main Duties a) Providing legal, administrative and secretarial services to the Board of Directors and Counc

Waziri atoa miezi sita kwa wakuu wa shule

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa miezi sita kwa wakuu wa shule za msingi na sekondari nchini kuanzisha madawati ya ulinzi na usalama wa watoto kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wanafunzi. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike kitaifa iliyofanyika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara amewasisitiza wakuu wa shule za msingi na sekondari kuzingatia uwepo wa dawati la ulinzi na usalama wa mtoto kike katika shule zao ili kuwa salama na kuwa na mahali pa kueleza matatizo yao. Mh. Ummy ameongeza kuwa suala la kumlinda mtoto wa kike ni jukumu la kila mmoja katika jamii na kuwapongeza wadau wa maendeleo ya watoto kwa jitihada zao na kushirikiana na serikali kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu madhara ya mimba za utotoni, ukeketaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la kutokomeza ukeketaji Tarime Stela Mgaya amesema kuwa wamefanikisha kuwaondoa mangariba 63 kut

MKUU WA WILAYA YA MBULU,ATATUA MGOGORO WA KIMPAKA KATI YA MBULU NA BABATI.

Image
Mkuu wa wilaya ya Mbulu C helestino S. M ofuga jana tarehe 10/10/2017 ametatua mgogoro wa kimpaka kati ya wilaya ya Mbulu na babati ,ambako kulitokea machafuko usiku wa kuamkia jana na kusababisha kubomolewa kwa nyumba mbili.  Mgogoro huo wa Siku ulishatatuliwa na kamati za ulinzi na usalama za babati na Mbulu mnamo mwezi wa sita. Wakuu wa wilaya babati Raymondi mushi na C helestino S. Mofuga walitatua mgogoro huo baada ya kutuma watalaam kutafsiri mipaka ya wilaya hizo Mbulu.  Hata hivyo mgogoro huo uliibuka tena Jana baada ya wananchi kubomoa nyumba mbili kwa madai zimejengwa katika maeneo ya malisho.  Mkuu huyo  wa wilaya ya mbulu amekemea vikali t a bia za kuharibu Mali za watu wengine na kuwaagiza wote waliobomolewa kuripoti kwa mkuu wa wilaya ya babati kwa kuwa wapo babati kiutawala, ili hatua zichukuliwe dhidi ya wahalifu.  Pia mkuu wa wilaya ameagiza viongozi kusimamia mipaka kikamilifu ili kuepusha machafuko yasitokee.

BAMIA Husaidia Wagonjwa wa Vidonda vya Tumbo.

Image
Watu wanaosumbuliwa na maradhi kadha wa kadha ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia. Unafahamu kuwa kwa kula bamia unaweza ukawa umejiondoa katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali? Bamia ni chanzo kizuri cha Vitamin A na beta carotene ambavyo ni virutubisho vinavyosaidia kuboresha uwezo wa kuona. Bamia inasaidia kuweka kawaida kiwango cha sukari mwilini na nyuzinyuzi zake zinasaidia kurahisisha ufyonzwaji wa sukari mwilini. Pia hudhibiti pia kiwango cha lehemu mwilini na hasa pale inapokuwa mtu ametumia vyakula vingi vyenye mafuta. Husaidia pia kulainisha choo. Vilevile ni mboga ambayo kwa Waafrika huongeza hamu ya kula na hata kurahisisha kazi ya kumeza. Wataalamu wanaeleza kuwa ina virutubisho vinavyoweza kupambana na bakteria wanaoshambulia utumbo na kusababisha vidonda vya tumbo. Pamoja na haya yote bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa

Mtoto wa Mwalimu Mkuu Aanika Alivyomkuta Baba Yake Amejinyonga

Image
MTOTO Frank Benedicto (14) ni mtoto mkubwa wa Mkuu wa Sekondari ya Migukulama, Benedicto Lweikiza (45) aliyejinyonga juzi, amesema alitahamaki kumkuta baba yake akiwa amening’inia darini. Lweikiza alijinyonga hadi kufariki juzi saa tisa alasiri katika mtaa wa Kilabela Kata ya Nyatukala wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Mwalimu huyo alikuwa anafundisha Sekondari ya Migukulama iliyopo Kata ya Nyanzenda Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema. Mtoto wa marehemu huyo aliyekuwa akiishi na baba yake kwenye nyumba hiyo, anasoma kidato cha kwanza katika Sekondari ya Sima iliyopo wilayani hapo, alisema baada ya kutoka shuleni alikuta mlango wa nyumba yao upo wazi hivyo akadhani baba yake atakuwa kwa majirani. “Asubuhi niliagana vizuri na baba yangu wakati nikienda shuleni, jioni niliporudi ndipo nikakuta baba amejinyonga juu ya dari na kabla sijagundua kitu chochote nilikuta mlango wa nyumba upo wazi nikadhani yupo kwa majirani nilipoingia chumbani sikuamini nilichokiona

Majambazi Walivyomtwangwa Risasi Mwenzao Mbele ya Polisi

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah. ROBERT Massawe (51) , mkazi wa jijini Dar es Salaam, ambaye polisi wanadai ni mtuhumiwa wa uporaji na mauaji, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wenzake. Kabla ya kuuawa katika majibizano ya risasi, mtuhumiwa huyo anadaiwa alikamatwa akiwa na SMG yenye risasi 24, simu 19 zilizoporwa maeneo mbalimbali na laini za simu 58. Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issa h imesema mtuhumiwa aliuawa na wenzake saa tisa usiku wa kuamkia jana wilayani Rombo. Alisema mtuhumiwa pamoja na mkewe walikamatwa jijini Dar es Salaam na baada ya kuhojiwa na polisi inadaiwa alieleza matukio ya ujambazi aliyoshiriki na alikubali kuwaonyesha mahali alipoficha bunduki. Polisi imesema simu tatu kati ya 19 wamegundua ziliporwa Moshi na moja alikuwa akiitumia mkewe ambaye anashikiliwa Dar es Salaam. Kamanda Issah alisema aliwaeleza polisi kuhusu mpango wa kufa

Chadema Yapata Pigo Lingine

Image
Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimarisha kwa kuvuna wanachama watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na mikakati ya kuja kulikomboa jimbo la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama cha CHADEMA. Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao kutoka kata ya kitwiru mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya aliwapongeza wanachama kwa kutambua kazi inayofanywa na chama cha mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano DR John Pombe Magufuli. “Mimi nimefurahi sana nyie kurudi nyumbani maana mtakuwa na msaada mkubwa sana katika kukijenga chama hapa manispaa ya Iringa ili tuweze kulikomboa jimbo hili katika uchaguzi ujao na hii ndio mikakati yetu” alisema Rubeya. Rubeya aliwaambia wanachama hao kuwa sasa wapo katika mikono salama ya kisiasa tofauti na walipokuwa kwenye chama cha awali na kuwasihi wasiwe waoga katika kufanya kazi za kukijenga chama cha mapinduzi. “CCM ndio chama tawa

WEMA SEPETU AMSHUKIA VIKALI SOUD BROWN,AMPA MAKAVU IKISA MAMA YAKE

Image
     There is Limits to everything jamani… Sipendi kabisa wen people involve my Mother kwenye mambo ambayo hata hayamuhusu… Niachie mama angu Soudy… I dont like it wen u bother her like dat only for u to record her alafu uje kumuanika like this… Hivi kwani @soudybrown huna mama wa kumfanyia hivyo unavyofanya… Sasa basi jus like da way huwezi mfanyia mama ako basi usiwafanyie na mama wa wenzako… Have some Respect atleast… Like I said kuna limits katika kila kitu… Hayo mambo yako ya Shilawadu yabaki huku kwetu vijana.. Wazazi tuwaache kama walivyo… Umenikera sana kwakweli… Sijapenda hata kidogo.

TANGAZO: VIWANJA VINAUZWA DODOMA MJINI

Image
Viwanja vinauzwa vipo Dodoma maeneo ya Mnada wa zamani njia ya kwenda Kondoa, SQ.M 1 ni 15,000... Ni kilometa 5 kutoka Jamatini. piga simu hii kwa maelezo zaidi.  0754461753

DIAMOND PLATINUMZ NA RICK ROSS WAKINUKISHA,BABU TALEE ASHUHUDIA LIVE

Image
          Meneja @babutale @richforever na @diamondplatnumz wakielekezana Kitu Flani #location #MiamiUSA ras_vegaHatariii mnyamaaa amekutana na mnyamaaa unyamani  

Mifupa ya Binadamu Yakutwa Kwenye Bwawa Mkoani Shinyanga

Image
KAMANDA wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule amethibitisha kuokotwa kwa viungo vya mwili wa binadamu katika bwawa la maji la Jomu wakati watu wakitafuta maji huko Tinde mkoani Shinyanga. Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule alidai kuwa iku ya Jumatatu  watu walipoona viungo hivyo vya binadamu ilibidi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na wao walifika na kukuta viungo hivyo. “Fuvu la kichwa limepatikana hapo bwawani, taya ya binadamu, mbavu za binadamu kumi na nne. “Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo jeshi la polisi lilichukua hatua za haraka kufika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa awali tukishirikiana na daktari mtaalam wa viungo vya binadamu  “Katika tukio hilo tulikuta viungo hivyo ikiwa pamoja na mfupa mmoja wa sehemu ya paja, mifupa ya mikono na mifupa ya sehemu ya bega ya binadamu,” alisema Simon Haule. Aidha Kamanda Haule alisema kuwa uchunguzi wa tukio hilo

ALI KIBA NA MANGE KIMAMBI MAPYA YAIBUKA

Image
              Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake wa ‘Seduce me’ amefunguka na kusema kuwa Tanzania kila mtu ana haki na uhuru wake hivyo hata yeye anajisikia vizuri kuona watu maarufu wanapenda kazi zake na kudai ana haki ya kupendwa na Mange Kimambi Alikiba amedai kuwa Mange Kimambi ni moja kati ya mashabiki zake na kusema anashukuru sana kuona anapenda kazi zake na kumpa nguvu katika kazi zake hizo kwa kutoa ‘support’. Ni kama shabiki wangu na ‘appreciate’ anapenda muziki wangu kwa sababu mimi namuheshimu kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anani ‘support’ kwenye kazi zangu lakini pia kutokana na uhuru hivyo kila mtu ana haki na vilevile mimi nina haki ya kupendwa na mtu yoyote yule, hivyo nina haki ya kupendwa na Mange Kimambi pia” alisema Alikiba Mbali na hilo Alikiba alisema anajisikia vizuri kuona muziki wake unazidi kufika mbali zaidi duniani na kuendelea kufanya vizuri nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla. “Najisikia f